Waislam msiende liliondo- redio kheir

muhogomchungu

JF-Expert Member
Jan 9, 2011
375
3
Jana kulikuwa na mjadala na kuwataka waislam kuacha kwenda liliondo. walisema hio ni dawa ya kiini macho. walisema kama kuna mtu amepowa kwa dawa hiyo ajitokeze waziwazi kabla ya kupoa akiuumwa nini na sasa apime aonyeshe kwamba kama kweli amepoa.
waliwataka waislam kuachana na kabisa dawa hiyo wanayoita ni DECI
 
Mbona ndio wanaoöngoza" hapa uswazi kwe2 tmk wote wametimkia huko, hata kitimoto haitoki' tukiuliza eti wameenda kurekebisha mda loliondo. Poleni sn
 
ina maana kama watu hawaponi kwa nini wanaendelea kuongezeka kule loliondo?naona hapa mmebase kidini zaidi , but wewe .. Babu hajaweka matangazo wala hajaita mtu kwenda kwake
 
Kwani wameitwa? kwanza wasiende watatumalizia dawa yetu! ingekuwa wao...usingetia mguu hadi uitwe Juma, rahima, ramadhani n.k ndio maana hata ile mboga 'hawali'!!!!!
 
Kwani wameitwa? kwanza wasiende watatumalizia dawa yetu! ingekuwa wao...usingetia mguu hadi uitwe Juma, rahima, ramadhani n.k ndio maana hata ile mboga 'hawali'!!!!!

mboga ? Hivi kweli kama babu babu anakula yule mdudu hapa inakuwaje yaani. I mean dawa ya babu .ila kama mtu ni mgonjwa hutajali kitu.hawa wanaopayuka hapa hawaumwi
 
Too late wameshaenda wengi,mahita mmojawapo.

Hizi dini tulizorithi au kupokea zinatupeleka pabaya sasa!

Watu wanajitafutia tiba mbadala, wengine wako busy na vipaaza sauti wakiwakataza! tuone itakavyokuwa.

HUU UDINI UNATUFUNDISHA NINI HAPA TANZANIA?
 
Jana kulikuwa na mjadala na kuwataka waislam kuacha kwenda liliondo. walisema hio ni dawa ya kiini macho. walisema kama kuna mtu amepowa kwa dawa hiyo ajitokeze waziwazi kabla ya kupoa akiuumwa nini na sasa apime aonyeshe kwamba kama kweli amepoa.
waliwataka waislam kuachana na kabisa dawa hiyo wanayoita ni DECI

Wanaakili za kitoto kabisa hawa wao ni waislamu gani?wamekunywa dawa waislamu wanaojiita waislam toka oman,Watu wamekwisha kujitangaza hawasikilizi wala hawafuatilii habari hawa jamaa wanaojiita waislam,kwenye vyombo vya habari mbona wamejitangaza,TV,Magazeti,Redio na mitaani pia mimi nisingekwenda kama kumuona mwenye kisukari cha kuchoma sindano kupona na mwenye Ukimwi kuacha kutumia ARV baada ya kurudi toka kwa mchungaji.
kilichopo hapa hawa jamaa na ubinafsi wao ndio unaowasukuma kusema hivyo,kwa kuwa ni mkristo anayetoa tiba ndio maana hawataki waislamu watibiwe na mkristo si waache hospitali za wakrito na waenda za waislamu?Walie tu serikali yenye mkono mrefu imeshindwa sembuse wao,waende na wao wakanywe kikombe bana wasijivunge.
 
Mataifa yote yatakiri kuwa Yesu ni jina kuu kuliko majina yote, sioni sababu ya waislamu kusuiwa kwenda pale kukutana na uponyaji, maana kwa babu unapokea dawa na unaombewa, sasa wasitake kuwazuia watu acha watu washuhudie uweza na nguvu ya Mungu.. maana kwa jina la Yesu wagonjwa wanapona na wenye shida wanafunguliwa..... hawana akili hao jamaa waliotoa hilo tamko mbona hata siku moja wakristo hawajawahi kutumia vyombo vyao vya habari kuwakataza wakristo wasiende pale Mwembechai kwa sheikh yahya?
 
Jamani hivi maadili ya vyombo vya habari yamepotelea wapi? Nani anatoa fursa ya hivi vyombo kukampeni udini? Jamani ruanda na burundi ilianza kwa kampeni za ukabila kwenye vyombo vya habari
ndugu zangu wenye dini mbalimbali udini hautatupeleka pa zuri mi nadhani babu hajasema watu wa dini fulani ndio wanapata tiba tu bali watu wote. Nadhani waandishi wa habari kwenye vyombo kama hivyo walisomea chini ya mti kwani hawako neutral kabisa ni wabinafsi na si ajabu walisoma kwa bahati mbaya kizazi cha dizaini hiyo kinatakiwa kilipuliwe na mabomu kiishie kabisa kwani watatupeleka pabaya!
 
sasa watu kwenda loliondo wao inawauma nini? kwani quran inakataza mitishamba?
 
Kama ni kweli wamesema hivo basi waislam wamekosa sera angeenda kufanya research aone walivyojaa kwa babu duh yaani kweli waislam wanaitaji maombi kwa maana hizi sio akili zao. Ukitaka kuwauliza reason kwanini waislam wasiende watakupa sababu ambazo hazina maana kabisa maana najua wanachopinga hapo ni kwa kuwa Yesu ndo anatumika hapo na wao wanasema hakuna Yesu
 
Mataifa yote yatakiri kuwa Yesu ni jina kuu kuliko majina yote, sioni sababu ya waislamu kusuiwa kwenda pale kukutana na uponyaji, maana kwa babu unapokea dawa na unaombewa, sasa wasitake kuwazuia watu acha watu washuhudie uweza na nguvu ya Mungu.. maana kwa jina la Yesu wagonjwa wanapona na wenye shida wanafunguliwa..... hawana akili hao jamaa waliotoa hilo tamko mbona hata siku moja wakristo hawajawahi kutumia vyombo vyao vya habari kuwakataza wakristo wasiende pale Mwembechai kwa sheikh yahya?

Wakati wa DECI mlikusanyana pale Sabasaba Kilwa Road mkasema maneno haya haya. Oooh Yesu anagawa utajiri, kwa Mungu yanawezekana! mwisho ukweli ukajulikana kuwa ilikuwa ni SCAM! Nashangaa wale maaskofu walioshadidia hili hawakuwaomba radhi!

Leo unakuja ushetani mwingine watu mnaleta stori zilezile! Soon ukweli utajulikana msije mkabadilisha kauli hapa!

La msingi, nani aliyepimwa na kuthibitika ana HIV antumia ARV akaenda huko kwa babu akapona? Apimwe tuthibitishe kuwa kapona! Msitulee stori za imani imani hapa!
 
Hili hawawezi kulizuia, watu wanashida nyingi wao wanasema wasiende? Ili iweje wakati mmeshindwa kuwatibu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom