Waislam (batamiki) kuisalia dua chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislam (batamiki) kuisalia dua chadema

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Jidulamabambase, Sep 29, 2011.

 1. Jidulamabambase

  Jidulamabambase Member

  #1
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BATAMIKI kufanya dua ikiwa CHADEMA haitaomba radhi

  Kauli CHADEMA kuwatuhumu masheikh kuwa wanatumika kuipa ushindi CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, zimechukua hatua mpya baada ya Baraza la Taasisi za Mikutano ya Kiislamu (BATAMIKI) kuipa CHADEMA siku tatu kuomba radhi kwa kuwahusisha viongozi hao kwenye masuala ya siasa na harakati za kuwania ubunge jimboni humo.

  BATAMIKI imesema iwapo CHADEMA haitafanya hivyo katika kipindi kilichotolewa, litafanya dua maalumu ya siku saba kumwomba Mwenyezi Mungu awadhalilishe viongozi wa chama hicho na kuwaondoa katika nyadhifa walizonazo.

  Awali, uongozi wa CHADEMA ulipewa wiki moja kuomba radhi kwa Watanzania na Waislamu kutokana na kitendo cha wabunge na wafuasi wake jimboni humo kumdhalilisha Mkuu wa wilaya hiyo, Fatma Kimario na kumvua hijabu. Hata hivyo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Profesa Abdallah Safari, alidai Fatma hakuwa amevaa hijabu bali mtandio na kwamba, chama chake kinaamini masheikh wanatumiwa na CCM katika uchaguzi huo ili kuipa ushindi.

  Profesa Safari, ambaye awali alikuwa CUF na alijiunga CHADEMA baada ya kuangushwa katika uchaguzi wa mwenyekiti wa chama hicho na Profesa Ibrahim Lipumba, alidai masheikh walipaswa kuwa na subira.

  Katibu Mkuu wa BATAMIKI, Sheikh Sadiq Godigodi, alisema jana kuwa, dua itafanyika kutokana na uongozi wa CHADEMA kushindwa kuwaomba radhi Watanzania na Waislamu.

  "CHADEMA kutoa tamko kupitia Profesa Safari kuwa masheikh wanatumika kuipa ushindi CCM, si la kweli.

  "Sheikh ni kiongozi wa Kiislamu ana mamlaka ya kutoa tamko kuhusu tendo lolote baya analoliona linafanyika kinyume cha utaratibu, ikiwemo kudhalilishwa kwa Uislamu,'' alisema.

  Alisema suala la masheikh kukemea si la kisiasa, bali lipo katika misingi ya heshima na kuutukuza utu wa Mwislamu.

  "DC amedhalilishwa, viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuomba radhi na si kutoa majibu yasiyokuwa na mantiki, huku wakipotosha maana kuhusu hijabu,'' alisema.

  Kwa mujibu wa Sheikh Godigodi, Kuruani inaeleza hijabu kama vazi la staha na linalotambulisha heshima ya mtu mbele ya jamii.

  Alisema Sura ya 33 aya ya 59 katika Kuruani inasema: "Ewe mtume waambie wake zako na mabinti zako wote wa Kiislamu wajiteremshie vizuri shungi zao mpaka kifuani mwao kufanya hivyo kutawafanya wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe.''

  Kutokana na hilo, alisema BATAMIKI inamtaka Profesa Safari asitumike kwenye jambo lolote linalohusu dini ya Kiislamu, kwa kuwa viongozi wake wamekwishakosea na wanachotakiwa kukifanya ni kuwaomba radhi Waislamu.

  Akizungumzia dua maalumu, Sheikh Godigodi alisema itasomwa kuanzia Jumanne na masheikh kutoka Uganda, Kenya na Tanzania.

  "Endapo hadi Ijumaa CHADEMA hawatakuwa wameomba radhi Jumanne ijayo dua itasomwa kwa mikoa ya Tanga na Dar es Salaam na Zanzibar,'' alisema.

  Aliwataja masheikh watakaosoma dua hiyo kuwa Idrisa Adamu Waridi (Mombasa, Kenya), Mohamed Ismai (Lamu, Kenya), Mahmoud Lugaia (Uganda) na Rajabu Amran (Tanzania).

  Katika hatua nyingine, CHADEMA imeanza kumshutumu mbunge wa Singida Kaskazini Tundu Lissu, kwa kushindwa kuomba msamaha kwa Waislamu kuhusu Fatma kuvuliwa hijabu.

  Habari kutoka ndani ya CHADEMA zinasema katika kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika hivi karibuni mjini Tabora, iliamuliwa Lissu alimalize hilo kwa kuwaomba msamaha Waislamu.

  "Unajua suala hili limefika hapa kutokana na baadhi ya viongozi kuwa wabishi na kuendeshwa chama katika misingi ya ubabaishaji. Wajumbe tulishakubaliana kwa kuwa tulishakosea tulipaswa kuomba radhi na kutoa sababu ambazo nahisi zingeeleweka kwa jamii na si kama ilivyo sasa,'' kilisema chanzo hicho.

  Alisema hatua iliyofikiwa ni matokeo ya ubishi wa Lissu na kuona CHADEMA inaonewa wakati mambo mengine sisi wenyewe ndio tunaojitakia.

  Source:
  Wavuti - Habari

  My take, Mtajulikana na kila mtu kuwa hamna mwelekeo, mmepotoka na mtaliangamiza taifa hili, mnataka wakristo pia watoe tamko ili mpate pa kusemea kuwa CHADEMA ni chama cha kikrsto! Mlachemshije!
   
 2. Jidulamabambase

  Jidulamabambase Member

  #2
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DUA la kuku halimpati mwewe! Hivi tanzania kuna serikali?
   
 3. T

  Topical JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Slaa na Mbowe watakuwa kama Lyatonga baada ya dua..hiyo..angalizo
   
 4. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,676
  Trophy Points: 280
  Jamani njaa nomaaaaaaaaaa.
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Wanatumia reverse psychology yote hiyo ni kutengeneza mazingira ya kusaidia CCM waibe kura lakini nadhani wamegonga mwamba nadhani Mrema na Mtikila na Mkapa wangeshaudead mpaka sasa,wangemwombea kikwete anayefanya watu kunywa chai ni jambo la anasa
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hizi taasisi zingine too much eti Taasisi za Mikutano ya Kiislamu (BATA MILK), kesho tutasikia Taasisi ya Maandamano ya kiislamu TAMAKI nayo imetoa tamko.
   
 7. T

  Topical JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wewe unaona lyatonga mzima angalia picha yake kwa feedback..
   
 8. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Magwanda kushnei, ngoja muoteshwe hydrocele. Mimi waislamu huwa nawaogopa sana hasa tangu wamfanyie Mrema kwakweli sina hamu nao tena.
   
 9. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,872
  Likes Received: 1,560
  Trophy Points: 280
  Hyo dua yao itacklizwa na MUNGU huyuhuyu au?
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huu ni upupu wacha wasome tuone hiyo J4 hata wakae wiki 3 wanasoma tuone .Mungu wao hana nguvu maana wanampigania wao ila Mungu ana nguvu ndiye hutupigania sisi .Hawa jamaa ni mufilisi kabisa .
   
 11. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Kweli njaa ni nouuuuuuma!
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Subiria balaa lake...Slaa atafanana kama Lyatonga..kwishne
   
 13. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Dua lao la kuku litawarudia wenyewe hawa washirikina, hakuna kosa walilofanya chadema, muhalifu kuvuliwa mtandio imekuwa nongwa, sasa wezi wakivaa mitandio waachwe. wewe topical na hao washirikina wenzio ndio mtakuwa kama Lyatonga
   
 14. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mungu wao sheikh yahya
   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Masheikh kuna kipindi nadoubt kuhusu uelewa wao, hivi inakuwje mambo madogo kama haya yanawachanganya kiasi hicho! Mbona hawamsemi huyo DC hana ndoa na anazini mpaka akapata watoto hao wote wanne? Kwa mujibu wa dini ya kiislamu mwamamke/mwanaume akioa/kuolewa na mtu wa dini tofauti akawa hajasilimu kisheria hawana ndoa hata kama watafunga ndoa ya bomani machoni pa Mungu wanazini, wameichunguza ndoa ya DC mpaka wanakimbia kigezo kidogo hicho cha hijjabu tena haikuwa hijjabu bali ushungi!!! Wanakimbilia kuomba dua utafikiri wao WANAPOKEA DUA NA KULAANI! Wao wanaomba na Allah anatenda, wasitishe watu. Ni dua za watu watatu ndizo hazina pazia kwa Allah 1.0 Dua ya mama kwa mtoto 2.0 Dua ya muumini aliyefunga kabla hajafuturu na 3.0 Dua ya mtu aliyedhulumiwa, sasa wao wako wapi katika mafungu hayo mpaka watishe watu. Wacha waombe, Allah atajibu kama ni dua yao ina mingi. Maombi mengi hayajibiwi kutokana kutokana na sababu nyingi mojawapo ikiwa ni uchafu wa waombaji kwa maana ya madhambi.
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hawa ni wapuuzi kama kweli wana uwezo huo basi wasome dua iliMahakama ya Kadhi iwepo na kesho Tanzania iingie OIC waache njaa zao hapa .Hawana kazi these are jobless wanatakiwa kuwa jela hawa muda huu wanatumia vibaya funds za waislam wenzao .CCM imeona hakuna vyama vya msimu sasa wameanza mambo hayo hahahaha.Bado sana .

  Kuombea Chadema sijui ujinga gani means kila mwanachama wa Chadema na mpenzi wake atakuwa kama waatakavyo au wameona moto mkali kwa viongozi hawa hongeki wala kubabaika ndiyo wameingia msituni ?

  Waislam bwana ndiyo maana nakubaliana na George Bush sometimes .Hawa wantakiwa wakae kwenye sayari yao wenyewe si kukaa na sisi watu Duniani .

  Wanakera mno for sure .
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wamemfanya Mungu kama test tube.
   
 18. m

  mtznunda Senior Member

  #18
  Sep 29, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Subir muone na hao wanaotukana uislamu humu jf mungu atawalaan inshallah
   
 19. W

  We know next JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama kweli hao Batamiki wameseam hayo, basi watakuwa wameteleza ulimi. Mungu anayejulikana hapa Dunia si yule anayepoke maombi ya kuwazulu watu na akayatekeleza, Yeye hupokea maombi ya msamaa na mema tu. Kama kweli watafanya dua hilo, basi kuna Mungu mwingine ambaye mimi si mfahamu ambaye ukimuombea mtu mabaya kweli hutokea!
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Utachukia sana lakini watakuwepo...pangeni kule kwenye jumuiya zenu kuwamaliza..kama mtaweza?
   
Loading...