- Source #1
- View Source #1
Kumekuwepo na chapisho linalosambazwa kwenye mitandao ya kijamii likiwa na nukuu inayodai kuwa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeingia katika mazungumzo na Serikali kwa lengo la kuangalia namna ya kuanza mchakato wa maridhiano, hatua inayolenga kujenga Tanzania yenye umoja, mshikamano na nguvu kiuchumi.
Katika chapisho hilo, inadaiwa kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya Kamati Kuu kujadili kwa kina umuhimu wa maridhiano katika kujenga taifa lenye umoja na mshikamano, pamoja na kuweka mazingira bora kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Kwa kutumia ufuatiliaji kwa njia ya mtandao, imebainika kuwa chapisho linalodai kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza mchakato wa maridhiano si la kweli, kwa kuwa hakuna taarifa rasmi kutoka CHADEMA iliyothibitisha kuwa chama hicho kimeanza mchakato huo.
Katika msimamo uliotolewa na CHADEMA, makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche, alisema: “Hakuna mazungumzo ya aina yoyote yatakayofanyika mwenyekiti wetu akiwa gerezani.”
Aidha, ufuatiliaji wa taarifa kwenye mitandao rasmi ya CHADEMA umebaini kuwa hadi sasa chama hicho hakijatoa taarifa kwa umma inayothibitisha kuwa kimekubali kuanza mchakato wa maridhiano. Badala yake, chama hicho kimeendelea kusisitiza msimamo wake kuwa kipo tayari kushiriki mchakato wa maridhiano iwapo Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, atakuwa huru.
Ikumbukwe kuwa hadi sasa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, anakabiliwa na kesi ya uhaini.