Wahusika wekeni taa za kuongoza magari Ubungo Kibo, maisha ya watu yapo hatarini

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Ni takribani mwezi mmoja tangu itokee ajali ya lori la mafuta Ubungo Kibo, Dar es Salaam iliyobabisha taharuki kwa wakazi wa eneo hilo sambamba na hasara kwa wafanyabiashara.

Ajali hiyo iliyotokea Agosti 6, 2023, iliharibu pia miundombinu ya barabara kiasi cha kuvunja taa za kuongozea magari.

Tangu itokee ajali hiyo, hadi leo Septemba 2, 2023, hazijawekwa taa zingine hali ambayo ni hatari kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Mara kadhaa nimeshuhudia magari na pikipiki zikipita hapo bila ya tahadhari hasa nyakati za usiku jambo ambalo ni hatari, pia ajali moja ishawahi kutokea nimeshuhudia.

Tunaomba wahusika waliangalie hili, waweke taa za kuongoza magari ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.
 
Nilikua natamani kuandika huu uzi baada ya kuponea chupuchupu kuliwa Za uso na mwendokasi ..

Jamani yale Mataa nadhani ni week ya 3 sasa .. labda wahusika hawapiti njia ile hawana taarifa.
 
Back
Top Bottom