Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,604
- 188,819
Hivi humu kunaonekana Watu wengi sana wanashida ya Pesa nini!? Maana mtu badala ajibiwe hoja yake,anajibiwa tafuta pesa Mkuu!!Sawa ila Tafuta pesa brother.
Haya hebu tuijdali hii hoja yako vizuri:
Mosi, wengi walisoma kwenye mfumo huo unaosema wewe wa kulipiwa kila kitu lakini bado wana matatizo makubwa. AU wewe huwaoni wasomi wetu wengi wenye umri kuanzia miaka 45 na kuendelea waliosoma kipindi cha Mzee Nyerere na Mzee Mwinyi ?
Pili, wengine wanasoma kuanzia shule hadi chuo-kikuu kwa pesa za wazazi wao lakini tatizo bado kubwa. Wanatafutiwa na ajira kabisa, lakini tatizo bado ni kubwa. AU mwenzangu huwaoni jinsi walivyo huko maofisini ?
Tena walikuwa wanataka wapikiwe mayai kutoka ulaya,ya bongo hawakuyataka,Hao wa 1957 walikuwa wanalipiwa hadi nauli za kwenda na kurudi likizo. Shuleni na vyuoni maisha yalikuwa matamu.. na ukimaliza chuo unapangiwa kazi sio kuomba.
Siku hizi wanafunzi wa chuo inabidi wafanye vibiashara vidogo vidogo ili kwenda sawa na gharama za chuo. Siku ya kumaliza unapewa invoice ya HESLB huku ajira hakuna. Mnaosifia zamani wote ni wa kupuuzwa.
Tatizo kama hili halitatuliwi na mtu mmoja ndugu RRONDO, ni kubwa na lina mizizi mirefu. Kama mtoto hataandaliwa vizuri chini (Elementary, Primary & Secondary levels) usitegemee kama atafanya makubwa chuo kikuu. Atafaulu na kupata madaraja ya juu lakini uwezo wa kukabiliana na mazingira yake utakuwa hafifu sana...Wewe kama mwalimu wa chuo ulichukua hatua gani kutatua hii changamoto? Hatua ulizochukua zilifanikiwa kiasi gani?
Kama tatizo liko wazi, linafahamika na linatibika kwanini utafute mchawi ???Hapa wakulaumiwa ni nani hasa mkuu?
Nakubaliana na wewe, uwezo wa kuzungumza na kuandika hutofautiana. Lakini hii haimaanishi kwamba mtu aliyesoma ashindwe kabisa kuwasilisha mawazo yake kwa kupitia hoja. Lakini pia mtu asipokuwa mzungumzaji mzuri basi hata utendaji wake huzungumza, kitu ambacho Tanzania ya leo kinapotea sana. Kinachoshanganza, hata ukizungumza na mtu (One to One) unakuta anapata shida....Usisahau kitu kinaitwa personality, kuna watu kulingana na walivyoumbwa, kuongea huwa ni tatizo hata kama wana hoja.
Jamii ya wasomi nchi yoyote ni mchanganyiko wa wazungungumzaji wazuri, waadishi wazuri au wenye sifa zote mbili.
Kwa maoni yangu ni vizuri tukawapima wasomi wetu kwa kuzingatia ujuzi wa walichosomea maana kuna fani nyingine hazimhitaji mtu kuwa mzungumzaji mzuri ili kuleta matokeo.
Wahitimu wengi wa vyuo vikuu vya kitanzania hawawezi kufanya mijadala mizuri. Kama wakifanya basi itakuwa ni mijadala ya kisiasa ambayo ni ya ndani ya nchi, lakini ukiwachukua leo hii ukawaweka vijana wa UDSM (Top Brass ya nchi) wafanye mjadala na vijana wa Pretoria, Zimbabwe, Abuja au Accra ni wachache sana watakaofanya vizuri. Hili nimeliona kwa macho yangu na kulithibitisha.........Unazungumzia hawa wanaomaliza TEKU na St. John?
Wanafunzi wa UDSM wao wanaona sifa kuongea broken English ila kudebate hawawezi kabisa maana uelewa wao ni mdogo mno. Utakuta mtu kajuwa Kiingerza miaka 6 iliyopita akiwa chuoni, leo hii hajuwi Kiswahili. Kwa kweli wanachekesha mno.Nimeangalia kwa makini sana huu mjadala na kama mtu niliyewahi kufundisha chuo nimeshangazwa sana na uwezo wa hawa wanafunzi wa Kiafrika. Kipindi wanafanya huu mjadala walikuwa ni wenye umri mdogo sana, lakini uwezo wao wa kujenga na kujibu hoja, kuzungumza lugha ngeni kwa ufasaha, ujasiri, pamoja na uwezo wa kumheshimu mzungumzaji mwingine umenishangaza.
Nafahamu fika kwamba hizo hoja zao walizijadili vizuri kabla ya mjadala, lakini kilichonifurahisha ni uwezo wao wa kuvaa vizuri uhusika na kuzijenga hoja ipasavyo. Nasikitika kusema kwamba wahitimu wetu wengi wa vyuo vikuu wanashindwa kujenga hoja kwa namna hii na kuzungumza lugha kwa ufasaha: Iwe ni Kiingereza au Kiswahili.
Kuna sehemu kubwa sana, sisi kama taifa tunakwama: Nasikika zaidi kusema kwamba hawa ndugu wa mwaka 1957, waliweza kufanya mjadala mzuri unaoeleweka kuliko wabunge wengi wa Tanzania wa mwaka 2021. Kibaya na kinachosikitisha ni kwamba wanasiasa wetu wamekuwa ni watu wanaoogopa mno mijadala, tena hadi wengine ni PhD....
Tuna kazi ya ziada kama taifa....
Kimtazamo wangu hapa kuna mawili: Kuna vijana wengi wanajitahidi sana, wanakuwa na uelewa mzuri wa vitu lakini utaalamu (Skills) wa kujieleza hawakujengewa tokea wanasoma shuleni. Siyo rahisi kuwa na mzungumzaji mzuri kama hukujengewa msingi mzuri. Hoja hii ameitoa Mkaruka hapo juu.Wanafunzi wa UDSM wao wanaona sifa kuongea broken English ila kudebate hawawezi kabisa maana uelewa wao ni mdogo mno. Utakuta mtu kajuwa Kiingerza miaka 6 iliyopita akiwa chuoni, leo hii hajuwi Kiswahili. Kwa kweli wanachekesha mno.
Kwani Hawa wanaotuongoza wengi wao ni wasomi wa miaka gani?Vyuo vikuu vya Tanzania sio chem chem ya fikra teena!!,kama ilivyokuwa60s,70s,80s and 90s Bali vimekuwa ni chem chem ya kijipwndekeza ili wapate teuz za UDC na URAS
Sabaya kasoma Saint Johns, nikishaona mtu kasoma sijui St John au Kampala au IMTU huwa nam-discredit mapema