Kuna kazi za kutumia akili nyingi sana
Kuna kazi za kutumia akili nyingi nguvu kidogo
Kuna kazi za kutumia akili kidogo nguvu nyingi
Kuna kazi za kutumia nguvu nyingi
Sasa hapo,kijana anatakiwa aangalie ni ipi itakayomfaa kwa muda husika
Ni kweli kabisa mkuu.Tuwe na moyo wa kuto dharau kazi kabisa.
Kuna kipindi niliangalia juzi kinaitwa POINTLESS ni maswali maswali kwa huko mbele.
Jamaa aliulizwa unafanya nini ukiachana na Mechanics unayosoma.Jibu lake ni
Bartender na anasema inampa hela ya kujiendeleza na kukidhi hali za maisha kwa mujibu wa ENGLAND.
Niliwahi pia kutana na IRISH mmoja alikuwa mwalimu wangu kwangu kwa 1Month.
MSc in Computer Science and BSc in Doctor of Medicine.
Nje ya shughuli hizo zote bado pia anachora sana na kutembelea familia za watu wanaotumia dawa za kulevya kwa kila week.
Wenzetu wana shughuli nyingi sana ambazo ki africa nyingi tunaziita za kipuuzi.Lakini hayo yote hutokana na dharau na kutothamini umuhimu wa kila jambo hata kama ni dogo kwa kiasi gani.
Ukiweza kufanya jambo fanya..maana malengo ya kusoma ni kujikomboa kiuchumi,afya,malazi na mavazi.
Sasa kama unaona unao uwezo wa kufanya kazi katika makundi kama uliyo sema hapo juu mkuu.Kikubwa heshima na nidhamu kwa kila unachofanya.
Weka uaminifu wa kazi zako na utulivu.Hakuna pesa nyepesi hela haimfuati mtu anayelala ana asiyetaka kuitumia akili yake..