Wahitimu wa vyuo waokolewe

Wahitimu wa vyuo waokolewe

Kumbuka hao watu wamekuwa trained kuwa maofisa na ndio maana wanabehave hivyo.....

Unapokuwa trained kama mtu wa aina fulani unategemewa kufanya majukumu ya huyo mtu.....

Huwezi ukasomea degree ya u daktari halafu uje kuwa mkulima au mhasibu. Hiyo ni kupoteza muda na pesa.

Kama tunajua watu wakisoma hawaajiriki then kwann tusiamue tu kusitisha hizo trainings za wasomi wa vyuoni tutumie hiyo pesa kufanyia mitaji ya biashara maana pesa ya miaka mitatu ya tuition fee plus accommodation ni pesa mingi sana.....

ndo maana nakuambia mm mwenyewe ni graduate lakini nimevua madaluga nimeweka chini nimeshika Jembe ma nyundo
 
Suluhisho la hili tatizo ni ajira za kudumu ziondolewe, mtu aajiriwe kwa miaka 5 tu, baada ya hapo wakajiajiri....nadhani ikiwa hivyo itatatua hii changamoto ya ukosefu wa ajira, pia uchumi utakwenda kwa kasi kwa sababu sekta binafsi zitakuwa nyingi zikiongozwa na wasomi.
No me nasema suluhu ni tuwekewe mfumo wa kulipa kwa lisaa la kuwa productive..... Na kuwe na shifti. Mfano ofisi moja inakuwa na wahasibu wa wili au wanne. Wanafanya kazi kwa hayo masaa yao then habari zingine zinaendelea.
 
Sekta ya mahoteli iliyumba: Serikali ilipoamua shughuli zake zote zifanyikie kwenye majengo yake. Yale mambo ya kutoka ofisini kwenda hoteli fulani kufanya semina/warsha/kongamano/mkutano kwa hela ya walipa kodi, yakafikia mwisho. Wenye mahoteli wakalalamika serikali inataka kuua sekta. Serikali ikasema, lini na wapi tulikuwa na mkataba kwamba sekta binafsi mjenge hoteli na serikali itakuwa mteja wenu? Baadhi ya hoteli zikafungwa. Baadhi zikageuka hosteli. Na nyingine zikajipanga upya na zikarudi hewani.

Vivyo hivyo sekta ya Miliki (Real Estate). Baada ya serikali kuhamia Dodoma, majengo mengi ya umma yakabaki wazi. Ikatoka amri taasisi zote za umma zihame majengo binafsi. Baadhi ya wamiliki wakaanza kulalamika agizo litaua sekta ya miliki. Lakini hatimaye sasa sekta inajitutumua irudi vema kwenye soko huria.

Sekta ya mabenki nayo mteja wake mkubwa alikuwa serikali. Serikali ilikuwa inatunza pesa zake benki za biashara, na kisha inakopeshwa pesa zake yenyewe. JPM alipoingia madarakani akasema hiyo ni biashara kichaa. Serikali isikope hela zake yenyewe. Mabenki yakatikisika kwa muda, lakini yakarudi kwenye mstari kwamba yaikopeshe serikali hela za watu wengine, siyo za serikali.

Sekta ya ajira kinachohitajika ni kusema waziwazi kwamba: soma, soma, soma we! Lakini hakuna mkataba wa kwamba utaajiriwa na serikali. Soma udakitari, uhandisi, sayansi, ualimu, ufundi, uvuvi, kilimo, nk., usitegemee utaajiriwa na serikali. Hiyo ilikuwa zamani. Kwa sasa serikali iko na watumishi wengi, ambao baadhi wanaweza hata kuhamishiwa sekta binafsi. Kazi muhimu ya serikali ni kutunga sera, na kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi, na kuwa refarii wa mtifuano katika sekta binafsi. Siyo kazi ya serikali kufanya biashara kushindana na sekta binafsi. Hapo itakuwa refa-mchezaji, na kuleta ukiritimba, vitu ambavyo hufifiza ushindani, ufanisi na ubunifu.

Pengine ni rahisi kusema hivyo kwa sisi tulioajiriwa sekta ya umma tayari, lakini kwa fikra tunazoziona kwa vijana wanaosaka elimu ya juu, kampeni mahususi inatakiwa kuwaambia kwamba serikali siyo mwajiri wa kumtegemea atasharabu wahitimu wote. Soma kwa manufaa yako, usitegemee kuja kuajiriwa sekta ya umma. Ukiona hailipi, achana na elimu ya juu. Soma elimu itakayokuwezesha kupambana na mazingira yako. Na elimu hizo ziko nyingi, kwa gharama nafuu, kwa ubora wa hali ya juu, na soko lililo tayari. Lakini zinataka juhudi na maarifa, pamoja na ung'ang'anizi (persistence) ya kijana husika.
 
Wiki ijayo wanamwagika mtaani graduate 100,000 mtaani kuungana na wenzao. Hadi kufikia 2025 barmaid wengi sana watakuwa na degree!

Wenye kazi hasa serikalini ongezeni sana nidham, uajibikaji na ukondoo. Ukianza harakati utafukuzwa tu kama waliotia nia ubunge na udiwani 2020.


Nasikitika sana, wadogo zangu wawili na mke wangu ni graduate wote, lakini hawajawahi hata kuitwa interview popote mwaka wa pili sasa!


Waajiriwa wengi serikalini wamezaliwa mwaka 1980 kuja juu. Tunatarajia wataendelea kwenye utumishi kwa miaka 20 mbele!! Wewe si utakuwa umepoteza sifa ya kuajirika! Wanaajiriwa umri usiozidi miaka 45!!!!


Ambao mnazaa watoto zaeni wachache, mkapa kazaa wawili, mtoto wa mkapa kazaa wawili licha ya utajiri walio nao. Wewe kapuku unazaa utawaajiri?



Nawasihi na kuwaarifu vijana wenzangu kuwa ajira hazipo isipokuwa kwa watoto wao.


Ova
ajira nikose hata watoto niwe na wawil? Tajiri na mali zake maskini na watoto wake
 
sijui kama umenielewa

Dhana ya jamaa ni kwamba sisi tuliofeli shule tukaishia form 4 Tukaenda kusoma udereva, Jeshini na veta ndio tunakula maisha.

While yeye kasoma hadi chuo kikuu anasugua gaga

ndio namuuliza kama naona kufeli ni fursa basi hajachelewa anaweza kwenda kusoma udereva, Veta labda Jeshini umri unaweza kuwa umemkimbia
Ila hajaongea kwa ubaya ila wamejipima wakaona uhalisia wa jinsi hali ilivyo mbaya.
Haimaanishi kwamba amewachukia madereva mnaoendesha mashangingi ila ametumia kama reference ili waongeze juhudi zaidi
 
Hii mada ni muhimu sana,na inasikitisha sana,nikisikia vijana wanaambiwa wakitoka vyuoni wakajiajiri,huwa napatwa hasira sana,
Hivi mnajua kwamba,mfano watu waliopo kwenye ajira kuanzia miaka 5,wakiambiwa sasa waache hizo ajira,wengine wachukue na wao waende kitaa "wakajiajiri"asilimia kubwa watachanganyikiwa,full msongo,
Sasa Kama Hawa wanaogopa,kwenda kitaa kujiajiri,maana wanaona Giza Totoro,sembuse madogo waliotoka vyuoni na masalia ya boom kiduchu!!!!!
Hapa serikali na wadau inabidi tuje na mkakati madhubuti wakuwapatia Hawa vijana ajira wanapohitimu,tuzalishe wahitimu wazuri hata tuwauze kwenye mataifa mengine kama India,na Nigeria zinavyofanya,USA,kumejaa ma IT,madokta,wahandisi kutoka,naija na India,mi nafikiri tuige wachina,Malaysia,Philippine,china sasa hv ipo dunia nzima inafanya miradi,
Ebu fikiri,tungekuwa na kandarasi,Rwanda,Burundi,Malawi,Congo,na zote zinaajiri vijana kutoka hapa hm,
Tutafute bidhaa moja,tuiuze dunia nzima,
Kama Samsung kwa Korea,au Tecno kwa mchina,
Kuwauza nchi nyingine hilo sahau kabisa.
Hizo nchi ulizotaja zenyewe zina ukosefu wa ajira kitambo sana vyuma vilishakaza tangu miaka ya 90's,kuna wasomi wengi sana kuliko fursa zilizopo.
Kingine hakuna nchi itakubali kuchukua wataalamu wa nchi ya tanzania viwango vya uelewa/elimu na teknolojia viko chini sana,uvivu maneno mengi sana kuliko kazi,sasa nani atakubali amchukue daktari wa huku aende kumpasua mgonjwa kichwa badala ya miguu eti umtoe mtaalam bongo aende kufanya kazi India au china.
 
Suluhisho la hili tatizo ni ajira za kudumu ziondolewe, mtu aajiriwe kwa miaka 5 tu, baada ya hapo wakajiajiri....nadhani ikiwa hivyo itatatua hii changamoto ya ukosefu wa ajira, pia uchumi utakwenda kwa kasi kwa sababu sekta binafsi zitakuwa nyingi zikiongozwa na wasomi.
Au tuajiri kwa rotation kila baada ya miezi 6 wanaingia watu wengine wengine wanaenda likizo ya malipo nusu.

Badala ya watu kukaa mwaka mzima kazini wakichati maofisini huku wengine wakisota mtaani.
 
Au tuajiri kwa rotation kila baada ya miezi 6 wanaingia watu wengine wengine wanaenda likizo ya malipo nusu.

Badala ya watu kukaa mwaka mzima kazini wakichati maofisini huku wengine wakisota mtaani.
Hapo utatafuta ugomvi na watu
 
Hizo ni theories mkuu ukianza kuwatafuta ndio utajua ilivyo ngumu.
Si kweli mkuu, fungua uzi ili upate ukweli...'wale wote mabingwa katika idara ya afya na hawana ajira wanyooshe mikono juu',wale wenye ujuzi uliotukuka wako mzigoni iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri. wale waliofuata vyeti ndio wako nje ya ulingo
 
Back
Top Bottom