Wahitimu wa vyuo waokolewe

New york City

Senior Member
Jul 24, 2020
175
566
Kwa miaka ya karibuni imekuwa ni kazi kumpata HOUSE GIRL kuliko mtu mwenye MASTERS au BACHELOR. Hii imetokana na ongezeko la idadi kubwa ya vijana wanaomaliza vyuo kila mwaka kutoka vyuo mbali mbali vya elimu ya juu.

Hii imesababisha sintofahamu kwa wazazi juu ya future za watoto wao ambao wako mashuleni na wale ambao wamemaliza vyuo tayari.

Jambo la kushangaza zaidi ni baadhi ya kada kuwa na watu wenye elimu ndogo wanaolipwa mishahara ambayo inafanya wasomi wa juu wadharauliwe, embu imagine msomi anendesha BODABODA alafu dereva wa VX la waziri ni form four tena failure, Mwanajeshi anadrive BIMA graduate anaendesha bajaji ya BOSS, na kada nyingine nyingi

Wito wangu kwa serikali ni kurekebisha mifumo ya utoaji ajira ambayo itawafavour GRADUATES

Graduates pia wanaweza kuwa Madereva, Askari, Wanajeshi, wasaidizi wa viongozi, n.k

Lakini pia ni muda sasa wa kupitisha sheria ambayo itawataka taasisi kubwa zote Tanzania kuwa na Internships angalau asilimia 10 ya waajiriwa wote katika Taasisi fulani wawe interns nadhani tutapunguza ugumu wa maisha kwa hawa Graduates wanatia huruma kwakweli.
 
Wiki ijayo wanamwagika mtaani graduate 100,000 mtaani kuungana na wenzao. Hadi kufikia 2025 barmaid wengi sana watakuwa na degree!

Wenye kazi hasa serikalini ongezeni sana nidham, uajibikaji na ukondoo. Ukianza harakati utafukuzwa tu kama waliotia nia ubunge na udiwani 2020.

Nasikitika sana, wadogo zangu wawili na mke wangu ni graduate wote, lakini hawajawahi hata kuitwa interview popote mwaka wa pili sasa!

Waajiriwa wengi serikalini wamezaliwa mwaka 1980 kuja juu. Tunatarajia wataendelea kwenye utumishi kwa miaka 20 mbele!! Wewe si utakuwa umepoteza sifa ya kuajirika! Wanaajiriwa umri usiozidi miaka 45!!!!

Ambao mnazaa watoto zaeni wachache, mkapa kazaa wawili, mtoto wa mkapa kazaa wawili licha ya utajiri walio nao. Wewe kapuku unazaa utawaajiri?

Nawasihi na kuwaarifu vijana wenzangu kuwa ajira hazipo isipokuwa kwa watoto wao.

Ova
 
Unaonekana una kaujinga fulani kichwani kwako lakini unakaficha kwa elimu yako ndogo

Kwani Ukimaliza Form4 Unashikiwa viboko kwenda form 5 kwann usiende udereva na ww, kwanini usiombe jeshi, Kwa nini usiende kusoma ufundi stadi Veta, kwanini usiwe mjasiliamali

Wewe uliona fursa ipo kwenda kusom Form 5 ukafika hadi chuo kikuu? Endelea na elimu maana naona kila mkipass mitihani mnaenda level ingine, Msiwe mnakwamia Degree , endeleeni hadi masters na huko mbele

Kila mtu anachagua maisha yake yaweje
 
Kwa miaka ya karibuni imekuwa ni kazi kumpata HOUSE GIRL kuliko mtu mwenye MASTERS au BACHELOR. Hii imetokana na ongezeko la idadi kubwa ya vijana wanaomaliza vyuo kila mwaka kutoka vyuo mbali mbali vya elimu ya juu.

Hii imesababisha sintofahamu kwa wazazi juu ya future za watoto wao ambao wako mashuleni na wale ambao wamemaliza vyuo tayari.

Jambo la kushangaza zaidi ni baadhi ya kada kuwa na watu wenye elimu ndogo wanaolipwa mishahara ambayo inafanya wasomi wa juu wadharauliwe, embu imagine msomi anendesha BODABODA alafu dereva wa VX la waziri ni form four tena failure, Mwanajeshi anadrive BIMA graduate anaendesha bajaji ya BOSS, na kada nyingine nyingi

Wito wangu kwa serikali ni kurekebisha mifumo ya utoaji ajira ambayo itawafavour GRADUATES

Graduates pia wanaweza kuwa Madereva, Askari, Wanajeshi, wasaidizi wa viongozi, n.k

Lakini pia ni muda sasa wa kupitisha sheria ambayo itawataka taasisi kubwa zote Tanzania kuwa na Internships angalau asilimia 10 ya waajiriwa wote katika Taasisi fulani wawe interns nadhani tutapunguza ugumu wa maisha kwa hawa Graduates wanatia huruma kwakweli.
Mkuu unachosema hapa ni kweli,
Mwaka juzi nilifanya utafiti wa miezi sita kuhusu GRADUATES EMPLOYABILITY kwanza nilihisi kuna kitu hakiko sawa kwani katika utafiti huo niligundua kwamba:
  1. 70% ya graduates wanafanya kazi ambazo hazihitaji kuwa na graduate level education
  2. 75%ya graduates wanafanya kazi nje ya fani walizosomea
  3. 55% wanalipwa mshahara wa chini ya dola 5 kwa siku
  4. 30% tu ya graduates ndo wana uwezekano wa kupata ajira mara baada ya kuhitimu
Mbaya zaidi utafiti ulionesha kwamba Graduates wengi wasipopata ajira ndani ya miaka 2-3 baada ya kuhitimu basi uwezekano wa wao kuajiriwa tena hushuka kwa zaidi ya 95%.Huu ulikuwa ni utafii binafsi wa kitaaluma ambao ulilenga zaidi majiji ya Arusha Dar es Salaam tu na hauwakilisha picha halisi ya hali ya ajira kwa wahitimu hapa nchini
 
Kwa miaka ya karibuni imekuwa ni kazi kumpata HOUSE GIRL kuliko mtu mwenye MASTERS au BACHELOR. Hii imetokana na ongezeko la idadi kubwa ya vijana wanaomaliza vyuo kila mwaka kutoka vyuo mbali mbali vya elimu ya juu.

Hii imesababisha sintofahamu kwa wazazi juu ya future za watoto wao ambao wako mashuleni na wale ambao wamemaliza vyuo tayari.

Jambo la kushangaza zaidi ni baadhi ya kada kuwa na watu wenye elimu ndogo wanaolipwa mishahara ambayo inafanya wasomi wa juu wadharauliwe, embu imagine msomi anendesha BODABODA alafu dereva wa VX la waziri ni form four tena failure, Mwanajeshi anadrive BIMA graduate anaendesha bajaji ya BOSS, na kada nyingine nyingi

Wito wangu kwa serikali ni kurekebisha mifumo ya utoaji ajira ambayo itawafavour GRADUATES

Graduates pia wanaweza kuwa Madereva, Askari, Wanajeshi, wasaidizi wa viongozi, n.k

Lakini pia ni muda sasa wa kupitisha sheria ambayo itawataka taasisi kubwa zote Tanzania kuwa na Internships angalau asilimia 10 ya waajiriwa wote katika Taasisi fulani wawe interns nadhani tutapunguza ugumu wa maisha kwa hawa Graduates wanatia huruma kwakweli.

Graduates wenyewe hawajitambui, wao wangeweza kuungana na kuleta mabadiliko katika nyanja zote za kijamii, siasa na uchumi!

Wakiendelea hivi hakuna atayewaona wala kusikia vilio vya mmoja mmoja!
 
Unaonekana una kaujinga fulani kichwani kwako lakini unakaficha kwa elimu yako ndogo

Kwani Ukimaliza Form4 Unashikiwa viboko kwenda form 5 kwann usiende udereva na ww, kwanini usiombe jeshi, Kwa nini usiende kusoma ufundi stadi Veta, kwanini usiwe mjasiliamali

Wewe uliona fursa ipo kwenda kusom Form 5 ukafika hadi chuo kikuu? Endelea na elimu maana naona kila mkipass mitihani mnaenda level ingine, Msiwe mnakwamia Degree , endeleeni hadi masters na huko mbele

Kila mtu anachagua maisha yake yaweje
Kingekuwa ni kitu cha kawaida wangefanya bila shida.

Hapo unachoshauri ni kama kuwashauri watoto walioachiwa urithi na wazazi wao kuwa wapambane na hali ngumu ya maisha bila kutumia hata chembe ya mali za wazazi wao.

Hii ni kitu mbaya sana kwa future generations. Hii inchi tunakusanya kodi, tuna madini na rasilimali mtaji za kutuwezesha kufufua taasisi na kuajiri vijana wengi na kuwalipa mishahara. Ni aibu sana kwa serikali kutoa matamko ya kuwataka vijana kujiajiri ile hali wao wenyewe hawajapitia hiyo zahma ya kujiajiri.

Ni mtu asie na akili tu ndie ataefikiria hivyo....
 
Sijui kama umenielewa

Dhana ya jamaa ni kwamba sisi tuliofeli shule tukaishia form 4 Tukaenda kusoma udereva, Jeshini na veta ndio tunakula maisha.

While yeye kasoma hadi chuo kikuu anasugua gaga

Ndio namuuliza kama naona kufeli ni fursa basi hajachelewa anaweza kwenda kusoma udereva, Veta labda Jeshini umri unaweza kuwa umemkimbia
 
sijui kama umenielewa

Dhana ya jamaa ni kwamba sisi tuliofeli shule tukaishia form 4 Tukaenda kusoma udereva, Jeshini na veta ndio tunakula maisha.

While yeye kasoma hadi chuo kikuu anasugua gaga

ndio namuuliza kama naona kufeli ni fursa basi hajachelewa anaweza kwenda kusoma udereva, Veta labda Jeshini umri unaweza kuwa umemkimbia
Mmmmmmhmn unajua ukishapiga degree akili yako inakuwa kama imefungwa unashindwa kufanya maamuzi ya kufanya kazi zingine nje ya taaluma.

Hii kiukweli msiwalaumu hawa wahitimu wa chuo. Kusoma masomo miaka mitatu ni kuwa programed kiakili kufanya hilo jambo. Hivyo mtihani wa kufanya jambo jingine ni mgumu sana kwa hawa raia.....
 
Hii mada ni muhimu sana,na inasikitisha sana,nikisikia vijana wanaambiwa wakitoka vyuoni wakajiajiri,huwa napatwa hasira sana,

Hivi mnajua kwamba,mfano watu waliopo kwenye ajira kuanzia miaka 5,wakiambiwa sasa waache hizo ajira,wengine wachukue na wao waende kitaa "wakajiajiri"asilimia kubwa watachanganyikiwa,full msongo,

Sasa Kama Hawa wanaogopa,kwenda kitaa kujiajiri,maana wanaona Giza Totoro,sembuse madogo waliotoka vyuoni na masalia ya boom kiduchu!!!!!
Hapa serikali na wadau inabidi tuje na mkakati madhubuti wakuwapatia Hawa vijana ajira wanapohitimu,tuzalishe wahitimu wazuri hata tuwauze kwenye mataifa mengine kama India,na Nigeria zinavyofanya,USA,kumejaa ma IT,madokta,wahandisi kutoka,naija na India,mi nafikiri tuige
wachina,Malaysia,Philippine,china sasa hv ipo dunia nzima inafanya miradi,
Ebu fikiri,tungekuwa na kandarasi,Rwanda,Burundi,Malawi,Congo,na zote zinaajiri vijana kutoka hapa hm,
Tutafute bidhaa moja,tuiuze dunia nzima,
Kama Samsung kwa Korea,au Tecno kwa mchina,
 
Back
Top Bottom