Wahitimu wa vyuo waokolewe

Wahitimu wa vyuo waokolewe

Kwa miaka ya karibuni imekuwa ni kazi kumpata HOUSE GIRL kuliko mtu mwenye MASTERS au BACHELOR. Hii imetokana na ongezeko la idadi kubwa ya vijana wanaomaliza vyuo kila mwaka kutoka vyuo mbali mbali vya elimu ya juu.

Hii imesababisha sintofahamu kwa wazazi juu ya future za watoto wao ambao wako mashuleni na wale ambao wamemaliza vyuo tayari.

Jambo la kushangaza zaidi ni baadhi ya kada kuwa na watu wenye elimu ndogo wanaolipwa mishahara ambayo inafanya wasomi wa juu wadharauliwe, embu imagine msomi anendesha BODABODA alafu dereva wa VX la waziri ni form four tena failure, Mwanajeshi anadrive BIMA graduate anaendesha bajaji ya BOSS, na kada nyingine nyingi

Wito wangu kwa serikali ni kurekebisha mifumo ya utoaji ajira ambayo itawafavour GRADUATES

Graduates pia wanaweza kuwa Madereva, Askari, Wanajeshi, wasaidizi wa viongozi, n.k

Lakini pia ni muda sasa wa kupitisha sheria ambayo itawataka taasisi kubwa zote Tanzania kuwa na Internships angalau asilimia 10 ya waajiriwa wote katika Taasisi fulani wawe interns nadhani tutapunguza ugumu wa maisha kwa hawa Graduates wanatia huruma kwakweli.
Kumbe unajua kabisa hao kidato cha nne wanakua madereva na wanalipwa vizuri sasa kwanini usitumie cheti chako cha kidato cha nne na ww ukapate io ajira ndugu maisha ni kuchagua wenzako walichagua izo kazi na zimewafikisha hapo na wewe pia ulichagua kusoma kwaio subili mda wako utafika.
 
Ili mbegu iote lazima ioze kwanza. Hivo hivo Ili upate maisha mazuri lazima upitie magumu. Nchi ambazo kwa sasa tunasema zimeendelea zilipitia hali tunayopitia hivi sasa. Katika kutafuta kipi cha kufanya watu waliamua kutumia elimu yao vizuri kwa kuangalia fursa zinazowazunguka. Mwanzo so mwepesi lakini penye nia kuna njia
 
Hoja yako ni nzuri na makini sana ila huko ndani hizo content umevurunda mkuu anyway uhalisia ndivyo ulivyo na maisha lazima yaendelee , tujifunze kuyakabili na tukubali ukwel.
 
Suluhisho la hili tatizo ni ajira za kudumu ziondolewe, mtu aajiriwe kwa miaka 5 tu, baada ya hapo wakajiajiri....nadhani ikiwa hivyo itatatua hii changamoto ya ukosefu wa ajira, pia uchumi utakwenda kwa kasi kwa sababu sekta binafsi zitakuwa nyingi zikiongozwa na wasomi.
Wazo flani safi sanaaa
 
Tulikuwa na mradi wa kusaidia vijana waliohitimu kozi fulanifulani kupata ajira. Tulituma tangazo, na vijana kadhaa wakajitokeza. Baada ya mchujo, tukapata vijana kadhaa kwenda kujitolea.

Katika wale waliochaguliwa, ilibidi kurudi kwenye taasisi tulizoomba nafasi kwa wahitimu, kwani baadhi walikuwa wakikataa nafasi hizo, walizoziomba wenyewe!

Sehemu ya kazi ilikuwa ni mjini kwenye viyoyozi na porini pa hapa kazi tu. Wazoefu wa sekta waliwashauri vijana wajitose kwenda maporini.

Tunashukuru wale vijana walioenda kujitolea, hawakutuangusha. Walichapa kazi. Wengi miongoni mwao waliishia kupata ajira walipokuwa wakifanyia kazi, na wengine taasisi jirani. Wengine walikataa ajira kwa sababu zao binafsi. Na wengine waliutumia uzoefu walioupata huko kufanya shughuli nyingine. Kwa ujumla zoezi lilikuwa na mafaniko makubwa.

Pengine ipo haja kuendeleza zoezi hilo kwa sekta ile, na hata kwa sekta nyinginezo.
ingependeza kama huu mradi ungekuwa endelevu ungetusaidia sana graduates

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom