screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,916
- 15,974
- Thread starter
- #241
MREJESHO
Nimesoma comment zote nashukuru mmenipa mwangaza wa nini cha kufanya. Mimi nilichofanya niliamkia kazini kama kawaida, but kabla sijaenda nikampa pesa ya nauli na hela ya 'sukari' ya Mama, akaniomba atumie simu yangu kumpigia boda kwani muda wake wa maongezi umeisha, niliyasikia maongezi na muda aliompanga aje amchukue, nikategea huo muda ufike halafu nikaongeza nusu saa mbele. Kama unavyoona text ya kwanza niliuliza kwa kumtega kutaka kujua kama amefika nyumbani. Text hii ilichukua dakika 12 haijajibiwa nikapiga simu akapokea, nikamuuliza umeiona text yangu akajibu hapana naomba niiangalie, nikakata simu akajibu 'Ndio'. Nikamwambia nitakupigia simu nimsalimie Mama, akadelay kama dakika 7 hajajibu msg ikabidi nipige simu ambayo haikupokelewa. Nikamtext mpe simu Mama niongee nae sasahivi, akanijibu baada ya dakika5 'Mama ametoka sijamkuta', nikamwambia awashe data nimpigie whatsapp video call, akajibu baada ya dakika 8 'Mtandao unasumbua'[emoji1781], baada ya dakika1 akanitext tena nimewasha data, nikamwambia nipigie nimsalimie D, akanipigia hiyo video call; ila mazingira aliyoonekana siyajui ndio nikamuhoji hapo ndio nyumbani? Akajibu hapa ni kwa jirani nduguyao, nikamuuliza umeaga unaenda kwa Mama au kwa jirani, akasema Mama sijamkuta hivyo nikaja kusalimia majirani, nikamwambia rudi nyumbani na umpe simu Mama niongee naye, akasema sawa, nikauliza nikupe dakika ngapi? Akajibu kama 30 hivi[emoji25], nikasema usinitanie dakika 30 kutoka kwa jirani? Akajibu sijajua kama Mama nitamkuta ndio maana nimesema 30, nikakata simu. Baada ya dakika kama 7 akanipigia nikaongea na Mama......
** Ukijaribu kupiga hesabu ya Muda nilioanza kumtafuta hadi nafanikiwa kuongea na Mama ni zaidi ya dakika 40[emoji56], akili ya kufanya maamuzi magumu ya haraka ilinijia ila nikarudi nyuma kidogo kwa kuwa na mimi miezi kadhaa iliyopita alinifuma na maovu fulani tukakaa kitako tukayasuluhisha.....Meseji ya mwisho niliyomtumia ndio hiyo inayoonekana hapo kwenye attachment....