Wahitimu wa Cuba naombeni msaada wenu tafadhali

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,793
15,693
Kwenye attachment hii ni convo ya mimi na mkewangu ambayo ilifanyika jana kupitia simu zetu. Story ni hivi, juzikati 'Jmosi' tuliandaa sherehe ya birthday ya mwaka mmoja ya mtoto wetu D, tulifanyia nyumbani huku tukialika majirani kadhaa. Maandalizi ya tukio zima roughly ilinicost kama laki2 na nusu hivi, nashukuru Mungu ilipendeza sana kama matarajio yetu yalivyokuwa (tulienjoy).

Kesho yake Jpili siku ya pasaka baada ya kutoka church nikaunganisha kwenye shughuli zangu za ujasiriamali, maana kama ni kusherehekea jana yake nilisherehekea vya kutosha kwa maana hadi saa7 usiku tulikuwa tunacheza mziki na kupigwa vyombo, hivyo sikuona sababu ya kuwa na mtoko tena siku inayofata badala yake niitumie hiyo siku kupiga kazi na kuupa unafuu mfuko baada ya kuvunja kibubu, Mama D aliniomba tutoke nikamwambia nimechoka na shughuli ya jana, acha leo nipige kazi, siku ikawa imepita.

Siku ya jana j3 nilikuwa kazini kwangu, nikawa na convo fupi ya sms na Mama D, baada ya kama nusu saa akatuma ujumbe kimakosa ambao ulikuwa unapaswa kwenda kwa mtu mwingine

'Mtandao mbaya sehem gani kutakua na usalama? Uko sipajui Nijibu kwa sms plz'.

Sikumjibu chochote baada ya kusema amekosea huo ujumbe ulikuwa unaenda kwa 'Mama Catherine ', baada ya kama lisaa limoja nikarudi home kupata lunch, sikuhoji chochote kuhusu hiyo msg yake, akasema by saa 10 jioni ataondoka kuelekea Beach. Mimi nikamwambia usiende, akahoji kwanini wakati uliniruhusu? Nikamwambia nikweli nilikuruhusu ila nimeahirisha, maongezi yakaishia hapo japo alionekana kukasirika, leo asubuhi kipindi tunapata breakfast kaniomba ruhusa kesho 'Jtano' aende kumuona Mama yake, mimi nikamjibu sawa (Mama yake anaishi pembeni mwa mji, ni kama kilometa 15 kutoka tunapoishi).

Kifupi hiyo sms ya jana aliyoituma kwangu kimakosa imenifikirisha sana, na hii safari ya katikati ya wiki kwenda kumuona Mama imenifikirisha zaidi, nahisi kuna mnyamwezi anataka kunisaidia majukumu, naombeni ushauri wasomi wenzangu, huu mtego nautegua vipi ama ni hisia zangu tu ndio zimekuwa negative? Nimruhusu hiyo kesho aende, ama nimkatalie ili niharibu formation?

NB; kwa miaka miwili tuliyoishi pamoja sijawahi mfumania Mama D, wala sijawahi hisi kama ananisaliti, ila kwa hiyo meseji nimeanza kuhisi kitu
Screenshot_20230411-172525_Messages.jpg







MREJESHO;
Soma comment no 242
 
Back
Top Bottom