Wahenga tukumbushane Klorokwini na mambo yake

Enzi hizo nikitaka kumeza hio dawa mama lazima aniwekee sukari ya kulamba..
Maana sio kwa huo uchungu.

NOTE:vijana wa miaka ya 2000s hamuwezi kuelewa kulamba sukari ni nini...
Enzi hizo kuramba sukari ilikua ni kosa la kuchezea kichapo cha haja..
Lkn ukipewa chroloquine mzazi anakupa sukari yeye mwenyewe urambe (hiki kitendo katika hali ya kawaida kilikua hakiwezekani)
 
Niliiacha mwaka 2008 baada ya kuwashwa siku tatu mfululizo, ikanianzishia ugonjwa mwingine nikioga ninawashwa.
 
Mimi kuinywa ile dawa lazima niwe na sukari pembeni, lakini cha ajabu ile dawa ikigusa tu ulimi lazima nitapike. Nikagundua kuifinyanga kwenye tonge la ugali nameza zimazima. Kingine wazee walikuwa watu wa afya so the first option nilikuea naomba nichomwe sindano badala ya kunywa ile dawa. Naamini ile ni sumu mbaya sana waafrica tulinyweshwa
Na mpaka leo hii dawa haswa ya malaria bado haijapatikana.ni wanatubadilishia tu.sisi ndo wamajaribio.maana tangu kwinini zimekuja aina nyingi tu za dawa ya malaria, huku zilizoko tunaambiwa hazifai.mm siku hizi napiga miti shamba tu.
 
duh umenikumbusha mbali sana.....yaani kwanza nilikuwa nakunywa na sukari....halafu...muwasho ule siyo wa nchi hii....nilikuwa najikuna kwa kujitupa kwenye magunia ya mahindi stoo usiku kucha....yaani ilikuwa hekaheka....unawashwa mpaka kwenye kinyeo au korodani...dah si mchezo......
 
Kuna dawa ya malaria ya sindano, iliyofuatia Chloroquine, ikiitwa "Christapen". Hii ilikuwa mbaya zaidi manake ukidungwa hiyo sindano lazima mguu ufe ganzi!
 
Duh mbona mimi nilitumia bila changamoto yoyote,?? au nina damu ya kunguni?
 
Back
Top Bottom