Wahenga tukumbushane Klorokwini na mambo yake

Nimekumbuka mbali sana nilikula hizi dawa nikiwa mdogo nilikua naharisha na kutapika vibaya mno dada yangu alishinda analia akidhani ndio mwisho wangu. Hiyo ndio malaria yangu ya mwisho mwilini hakika Mungu yupo.
 
Usicheke...mimi nilikuwa nawashwa, nikijikuna tu, navimba, na nilikuwa kibonge, baada ya masaa machache tu, ninakuwa kama sanamu la Micheline....
Hahaaa ,nimecheka kwa sautii ,zile dawa hazifai yani,ukinywa hasa ikifika usiku unaona kila aina ya rangi siyo kwa miwasho hiyo duh.
 
Sijawahi kuona dawa chungu kama ile mpaka sasa, na harufu yake sasa mpaka ugonjwa unaongezeka. Ile ilikua sumu kwakweli.
Kuna watu walikuwa wakigonga ile wanapona fasta hata kabla ya kumaliza dose.
Mimi mpaka leo natumia Fansider, japo nazo wanazizengea...mimi tatu tu...maji mengi, siku ya tatu ukininunulia maji ya ilala naburudika murua kabisa.
 
Mimi unanionea bure tu....
Hahahahah....mtoto wa mwalimu wewe hukuwa na shida ya Kalamu aka Bic, Simba au lusker.
Mimi nilikuwa natumia JV kutengeneza wino...nina refeel kwenye mrija wa Bic......shida maiticha walikuwa wanoko, wakiona rangi tofauti wanauliza umetoa wapi hiyo kalamu...

.Kumbe ni fundi mchundo mimi nishafanya yangu.
 
Hahaha we kiboko dah!

We ulipaswa uwe mhandisi kabisa...
 
kuna mzee mmoja alikuwa fundi maji wa DAWASA ya Enzi hizo maeneo ya Kibaha alikuwa anakunywa vile vidonge kwa kumung'unya kama pipi. Alikuwa akija kutengeneza maji anaomba kama mna akiba ya chrolokwini anajisikia malaria ukimpa anakula kama pipi. Yeye alikuwa teja kabisa wa zile dawa akizikosa hafanyi hata kazi
 
Kuna watu walikuwa wakigonga ile wanapona fasta hata kabla ya kumaliza dose.
Mimi mpaka leo natumia Fansider, japo nazo wanazizengea...mimi tatu tu...maji mengi, siku ya tatu ukininunulia maji ya ilala naburudika murua kabisa.
Kuna watu walikua hawana shida nayo.. Wengine tulikosana nayo kabisa.. Nilikua naichukia kuanzia harufu mpaka uchungu..

Hongera mkuu, hiyo fansider simezi hata nikose dawa nyingne.. Mweh.
 
Hahahaha kweli kazi ipo. Mtoa mada umejisikiaje hadi ukaikumbuka klorokwini??
Mie niliwahi fanya ujinga mmoja badala ya 4.4.2 nikaona niokoe muda jikagonga 5.5 basi siku ya pili nilipokunywa 5 hyo baridi yake hata chumba cha mochwari haiko hivyo
 
Mi nilikuwa nikinywa hamu ya kula inatoweka tumbo love nakwangua nalegea nakuwa kama tejaa. Ila kunywa sasa mama aviringa tonge la ugali nameza ila bado uchungu unaingia kwenye ugali jamani badala ya kali tulikuwa tunasema khhali. Lakini ndo dawa zilizokuwa zinafanya vizuri malaria hairudi na nahisi inaweza kutibu ukimwi
 
Unajua kama Chloroquine ingekuwa sio chungu na haina harufu mbaya, inafaa sana kumuwekea Usiyempenda kwenye Chakula....Awashwewashwe tu bila sababu.
Ile dawa nlikuwa nikiimeza... sipendi kabisa kuona chakula. Ni kutapika tu kama mama mjamzito
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom