Wahadhiri UDSM Waongelea tatizo la Udini

Wahadhiri UDSM Waongelea tatizo la Udini

Mpaka sasa hakuna uhakika kwamba hili tamko ni la wahadhiri wa UDSM au kuna ki blog kinataka kuanzisha satires za "The Onion" type kujifurahisha.

Tamko la wahadhiri wanaojua ku submit mpaka papers kwenye academic journals kwa formats na fotnotes halina anuani wala jina?

Kama wahadhiri wa Chuo Kikuu chetu kikongwe kabisa ndo wanaandika hivi, je tunaweza kushangaa hao form four wanavyofanya vibaya?

hili tamko la udasa mkandara ameliona?dr.bana naye alikuwepo?wote hao wameafiki?hiyo sababu ya kwanza read btn the line jk and ccm is inn ndiyo maana wanashindwa kupambana nao coz ndiyo sera iliyowaingiza madarakani.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 2/3/2013




Utangulizi


Wapendwa waandishi wa habari. Tunaomba kupitia ninyi tuweze kuongea na watanzania wenzetu kuhusu hali ya amani ilivyo nchini mwetu kufuatia kila aina ya dalili ya watanzania kukosa uvumilivu wa kidini. Tunatambua kuwa serikali yetu imefanya mambo mazuri mengi tu nchini, hilo hatuna mashaka nalo; hata hivyo kama watanzania tunadhani kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa. Hivyo basi, tunaomba kuchukua nafasi hii kuelezea wasiwasi wetu kuhusu migogoro hii ya kidini inayozidi kukua nchini.


Migogoro hii ilianza kuvuka kama moshi lakini sasa inaanza kulipuka na kusambaa zaidi. Tumeshuhudia uchomaji moto wa kanisa kule Mbagala, kumwagiwa tindikali shekhe mmoja kule Zanzibar na Shekhe mwingine kuuawawa, kuchomwa makanisa Zanzibar, kupigwa risasi viongozi wa kikristo kule Zanzibar na pia mgogoro wa kuchinja huko Geita ambako tumeshuhudia mchungaji mmoja akiuawa.


Mbali na hayo, kuna matukio kadhaa kwenye shule zetu za sekondari yakihusisha migogoro ya kidini kati ya wakristo na waislamu. Haya tumeshahudia yakitokea sekondari za Bagamoyo, Ndanda, Kibiti, Ilboru na kwingineko. Pia yapo malalamiko yasiyo rasmi kuhusu udini kwenye sehemu za kazi na kwenye taasisi mbalimbali za serikali. Wapo wanaodai kuwa baadhi ya taasisi binafsi, za kidini na hata za serikali zinazohudumia watanzania wengi zimekuwa zikiajiri wafanyakazi kwa misingi ya kupendelea dini fulani fulani. Jambo hili hata kama ni la kuzungumzwa tu, ni vema likafanyiwa kazi maana hisia hizi zikipanuka hujenga chuki na kusababisha watanzania wasielewane.


Kwanini haya yanatokea?


Sisi wanajumuiya ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunaamini, kama taifa, kuna mahali tumechepuka na kuacha misingi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa katika ujenzi wa taifa imara na lenye umoja. Kuna sababu kadhaa zilizotufikisha hapa tulipo, nazo ni:


1) Wanasiasa na watanzania wengi tunafuata dini zetu kwa hisia zaidi pasipo kufikiri kwa kina kuhusu yale tunayoyafanya. Tumesahau kabisa kuwa dini ni kwaajili ya kutuhusianisha na ulimwengu ujao tusioujua. Tunapaswa kumheshimu na kumthamini kila binadamu aliyeko hapa duniani. Kwa bahati mbaya baadhi yetu tunadhani kuwa ulimwengu huu umeumbwa kwaajili ya dini fulani na binadamu wengine hawana haki ya kufurahia maisha yao hapa duniani. Tunataka kutumia dini zetu kumiliki utawala wa dunia hii.


Dini zetu zimekuwa mtaji kwa baadhi ya wanasiasa na vyama vyao. Inasikitisha kuwa hakuna jitihada za kutosha zilizofanyika kuzuia wanasiasa kutumia dini kama sera au ajenda ya katika kupata kura. Baadhi ya wanasiasa wameingia madarakani kwa kutumia udini na ukabila na hivyo hali inapofikia watanzania kuanza kuchukiana kwa misingi ya dini wanakosa nguvu na ujasiri wa kukemea na kuzuia haya kwakuwa nao wamepitia njia hiyo.


2) Sababu ya pili ni kwamba hivi sasa umaskini nchini umekuwa wa kiwango cha juu. Kila mtu anatafuta jawabu la umaskini wake kwa kudhani kuwa umesababishwa na mfumo ulio nje ya maisha yake na ya serikali. Katika hali hii wamejitokeza watanzania wenzetu wanaotafuta majibu mepesi kwa kusingizia kuwa wamekuwa maskini kwasababu ya dini nyingine. Hali hii imesababishwa na ukosefu wa elimu kiasi kwamba watanzania wengi wanashindwa kuwa na uwezo wa kuchambua mambo kimantiki na badala yake wanaamini bila kuchuja lolote wanaloambiwa na viongozi wa dini au mwanasiasa au mwanaharakati. Ni vema watanzania wakajua kuwa ajenda ya udini si ya dini fulani bali ni ya makundi machache ndani ya taasisi zetu za dini. Tusibebeshe lawama za udini kwa dini fulani bali tuelewe kuwa udini umekuwa ni mtazamo ya watu wachache ndani ya dini zetu.


3) Tatu, watanzania tumeanza kupoteza uelewa kuhusu madui wetu wa asili ambao ni ujinga, umaskini na maradhi, na tumeongeza adui mwingine ambaye ni imani ya mwingine. Tumeacha kuelekeza nguvu zetu katika kupambana na maadui hao watatu na tunaelekeza nguvu zetu kupambana na dini nyingine ambazo kimsingi haziwezi kuwa sababu ya matatizo yetu ya kila siku.


Kwa bahati mbaya tunashindwa kuelewa kuwa dini hizi kuu mbili za kikristo na kiislamu ni dini zilizozaliwa sehemu mmoja baadaye zikasambaa sehemu tofauti na kuchukua utamaduni tofauti. Hatimaye tunachokiona sasa, ndugu wa ukoo na hata kabila moja waliotokana na historia moja, utamaduni mmoja na lugha moja wamefanywa maadui kwasababu wanafuata dini tofauti.


4) Jambo la nne, nchi yetu imeruhusu uhuru wa kuanzisha taasisi za dini pasipo kuwa na usimamizi wa karibu. Taasisi nyingi za kidini zimeibuka nchini na zimekuwa chanzo kikubwa cha kuwagawa watanzania kwa misingi ya kidini. Umoja wetu unapotea kwasababu baadhi ya taasisi za kidini zilizopo zinawagawanya watanzania kwa misingi ya dini. Taasisi nyingi za dini zinafundisha mbinu na namna ya kuwakabili waumini wa dini nyingine badala ya kuhimiza upendo na mshikamano miongoni mwa watanzania.


Baadhi ya viongozi wa taasisi hizo wamewafanya watanzania mtaji wao kwa kuwachochea wafuasi wao kuwachukia wengine kwa lengo la kutimiza haja zao binafsi. Watanzania tunapaswa kuzinduka na kuchukua tahadhari dhidi ya watu wanaotuchonganisha. Tukumbuke kuwa kiongozi wa dini anayekuambia kuwa dini fulani ni ya kishenzi na wafuasi wake ni wa kishenzi basi mtu huyo si mtumishi wa Mungu bali anatumikia maslahi yake.


Tufanyeje?


Baada ya kueleza sababu zilizotufanya tufikie hapa tulipo sasa, sisi wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunapendekeza mambo yafuatayo:


1) Serikali isimamie na kudhibiti vyombo vya habari vya kidini vinavyochochea chuki za kidini. Inasikitisha kuwa serikali iliyosheheni wataalamu wa kila aina inashindwa kutambua madhara ya uchochezi wa vyombo vya habari. Watanzania tunapaswa kujifunza kuwa hata mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda hayakuanza siku moja, yalichochewa na vyombo vya habari kwa muda mrefu na vyombo hivyo vilihamasisha pia mauaji hayo.


Hata hapa nchini kwetu, serikali isipokuwa tayari kukemea na kufungia vyombo vya habari vinavyotumia udini kuleta uchochezi, ipo siku watanzania watauana sana na nchi itapoteza heshima yake ya kuwa taifa la amani na tutakuwa wakimbizi. Tunaishangaa serikali inaweza kuyafungia magazeti yanayoikosoa lakini haiko tayari kuyafungia magazeti yanawachochea watanzania.


Tungependa ujasiri unaotumika na vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaoandika ujumbe wa vitisho kwa viongozi wa kisiasa nchini utumike pia kuwakamata wanaochochea uvunjifu wa amani. Kama tunaweza kuwalinda viongozi dhidi ya vitisho kwa maisha yao binafsi kwanini tushindwe kulilinda taifa letu kwa kutumia nguvu hizo hizo za kuwatumikia wanasiasa?


2) Pia tunatoa wito kwa wanasiasa na watanzania kwa ujumla kuwakataa wale wanaotafuta vyeo mahali popote pale, iwe kwenye vyama vya siasa au taasisi, kwa kutumia udini kama kigezo cha kutaka kuchaguliwa. Ni wakati muafaka sasa kuhuisha yale yote yatakayoleta mtangamano wa kitaifa. Kama taifa tumeacha misingi mizuri ya ujenzi wa taifa tuliloachiwa na waasisi wa taifa hili.


3) Jambo jingine ni kuhamasisha na kusimamia sera ya elimu sawa kwa wote. Elimu yetu ya sasa imejenga matabaka makubwa miongoni mwa watanzania na matokeo yake matabaka haya yanajitokeza zaidi katika sura ya udini. Kutokana na hali hii watanzania wengi waliokosa elimu wanadhani kuwa wenzao wa dini nyingine wanafanikiwa kwasababu ya upendeleo wa kidini. Kwa kusisitiza katika elimu, itakuwa rahisi kwa watanzania kuelimishwa kuwa chuki za kidini si msingi wa dini zetu tofauti na ilivyo sasa ambapo ukosefu wa elimu unawafanya wengi kuwa waathirika wa mafundisho potofu.


4) Pia tunaisihi serikali iwachunguze viongozi wa baadhi ya taasisi za kidini zinazowahamasiha wafuasi wake kufanya vitendo vya uhalifu. Ni vigumu sana kuwadhibiti wafuasi wa taasisi ya kidini ambao wameshakuwa na nguvu ya kuungana na kufanya jambo lolote baya. Tuna wasiwasi kuwa baadhi ya viongozi wa taasisi hizo wanatumika na watu wa nje kuvuruga amani yetu. Kwa bahati mbaya viongozi hawa wanajua wazi kuwa amani ikivurugika nchini wao wanazo sehemu za kukimbilia wakati ndugu zetu wakiendelea kuuana.




Wito wetu kwa watanzania wenzetu ni kwamba wajue kuwa viongozi wa kidini wanaowachochea kuwachukia wengine hawana nia njema na taifa na maisha yao. Watatuacha tukiliangamiza taifa huku wao wakiwa salama. Ni vema watanzania wakajua kuwa sababu ya umaskini na matatizo ya kimaisha hayajasababishwa na waumini wa dini nyingine bali mfumo wetu mbovu wa utawala unaoacha kukua kwa matabaka ya kijamii. Tukishirikiana sote kupambana na umaskini hakutakuwa na sababu ya kuchukiana. Pia, ni muhimu sasa, kila dini iendeshe maswala yake bila kutaka kubebwa na serikali.

Source;Nilikuwepo
Freeland
Wasomi hawa wa UDSM wameeleza mambo ya msingi sana kwa ustawi wa taifa hili. Lkn ninataka kusema jambo moja muhimu ambalo kama hatutakuwa tayari kulitekeleza kwa vitendo usomi wetu utakuwa ni bure. Watz wengi hasa wasomi tumekosa kuwa wakweli kwa kila jambo tunalolisema au kulijadili. Watz tulitegemea wasomi wangesimamia kitu kinaitwa "kusema ukweli kwa kila jambo" lkn wameshindwa! Wasomi hawa pamoja na mawazo yao mazuri wameshindwa kusema ukweli uliowazi huu udini, ukabila au ukanda umepaliliwa na nani? Chama cha CCM kwa upofu wake kimekuwa kikieneza sumu ya udini, ukabils na ukanda pale ambapo kinaona kinazidiwa ushawishi na vyama vya upinzani. Kila mtu anajua CCM ilivoeneza swala udini kuhusu chama cha CUF mwaka 2005 kwenye uchaguzi mkuu baada ya CUF kuonekana kimepata nguvu na ushawishi kwa watz wengi. CCM ilirudie mbinu ile ile ya udini na ukanda kwa CDM kwa 2010. Narudia tena watz tunawategemea sana wasomi wetu lkn kama wanakuwa waoga kusema yalikweli kuhusu chanzo au kiini cha tatizo basi ni bora wangekaa kimya kwa sababu haya mawazo waliyoyasema yamesemwa na watu wengi tena wa kawaida. Taifa hili limeangushwa na wasomi kwa kiasi kikubwa kuogopa kusema ukweli pale watawala wanakwenda kinyume na matakwa ya watz wengi. Wasomi wengi wamekuwa wakipigana kila siku kuwa upande wa watawala badala ya kuwa upande wa raia wengi masikini!
 
Last edited by a moderator:
Nyie Chadema si kila siku mnawatukana Waislamu humu ndani Leo CCM ndo mnaona wadini kweli nyani hajioni kundule
Jambo la ajabu, hawajaitaja CCM kuwa ndo chanzo. Why?
 
Ni ajabu leo wahadhiri kumsanifu mwalimu nyerere leo wakati kupitia makongamno mengi wahadhiri hawahawa wanasema mwalimu nyerere si baba wa taifa na kuwa hakuleta huru bali uliletwa na waislamu wenzetu. Sasa leo mnapata wapi ujasiri wakuficha unafiki wenu kuwa nyerere baba wa taifa na wakati mnadai yeye ndo alisababisha muwe nyuma hadi kielimu?

Wahadhiri hawahawa mkikutana na wanafunzi wa kiislamu mnawaeleza kuwa uhuru uliletwa na waislamu na baadhi yenu mlidai mnaandika kitabu cha jinsi waislamu walivyouleta uhuru na kuzika uongo wa mwalimu nyerere na mbinu za wakristo kuudanganya umma kuwa nyerere ndie alieleta uhuru. Kitabu chenu kimefikia wapi kwanza?
 
Tatizo watu wengi wanashindwa kusema ukweli. Hakuna tatizo la udini bali kuna tatizo la waislam kuwachukia wakristo na kuamua kuwadhuru. Wanawaua wakristo na kuwachomea makanisa yao. Sasa udini uko wapi hapa? Wakristo wanasema na kufundishwa kuwa mtu akikuzaba kofi shavu la kushoto wewe mgeuzie shavu la kulia na kumsamehe. Waislamu eanasemaje? Ni dini ya kigomvi ya kiuaji na nfio maana salman rushdie aliita kurani ina aya za kishetani. Matendo ya waislamu kwa ujumla wao ni ya kishetani na hatuwezi kuondoa jili kwa sababu limeandikwa kwenye vitabu vyao vitakatifu na wanafundishwa hivuo toka utotoni.
Sasa kama tunataka kuleta amani ni bora tukawafindisha na kuwaelimisha watu kama kina Ilunga na Ponda watu ambao hawana elimu yoyote iliwaelimike kidogo na kuwaongoza wafuasi wao kwa weledi kidogo. Wewe utaongozwaje na mtu kama Ilunga mtu mbu mbu mbu kabisa au Ponda who can hardly read and write?
 
Nyie wahadhiri mmesahau mchango wenu kwenye huu udini unaoendelea leo?
1. mlio viongozi mnaajiri kidini yaani waislamu kwanza, mlio madarasani mnajua mnachokifanya kwa wanafunzi wa kiislamu
2. wahadhiri makonganmano mlianzisha wenyewe na mmekuwa wahubiri wazuri kuwa uhuru uliletwa na waislamu na si nyerere na kuwa mlikuwa mnaandika kitabu cha jinsi waislamu walivyoleta uhuru na si nyerere na wakatoliki wenzie
3. Tuna kumbuka kwa walioona dvd ya kongamano la pasaka mliyoyasema huko leo mnaibuka na tamko la udin? Elimu zenu hazijakomboa
 
Unafiki wa matamko yasiyo taja wachochezi hautusaidii
Kwanini haya yanatokea?[/B]


Sisi wanajumuiya ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunaamini,
kama taifa, kuna mahali tumechepuka na kuacha misingi tuliyoachiwa na
Baba wa Taifa katika ujenzi wa taifa imara na lenye umoja. Kuna sababu
kadhaa zilizotufikisha hapa tulipo, nazo ni:


1) Wanasiasa na watanzania wengi tunafuata dini zetu kwa hisia
zaidi pasipo kufikiri kwa kina kuhusu yale tunayoyafanya. Tumesahau
kabisa kuwa dini ni kwaajili ya kutuhusianisha na ulimwengu ujao
tusioujua. Tunapaswa kumheshimu na kumthamini kila binadamu aliyeko hapa
duniani. Kwa bahati mbaya baadhi yetu tunadhani kuwa ulimwengu huu
umeumbwa kwaajili ya dini fulani na binadamu wengine hawana haki ya
kufurahia maisha yao hapa duniani. Tunataka kutumia dini zetu kumiliki
utawala wa dunia hii.


Dini zetu zimekuwa mtaji kwa baadhi ya wanasiasa na vyama vyao.
Inasikitisha kuwa hakuna jitihada za kutosha zilizofanyika kuzuia
wanasiasa kutumia dini kama sera au ajenda ya katika kupata kura. Baadhi
ya wanasiasa wameingia madarakani kwa kutumia udini na ukabila na hivyo
hali inapofikia watanzania kuanza kuchukiana kwa misingi ya dini
wanakosa nguvu na ujasiri wa kukemea na kuzuia haya kwakuwa nao
wamepitia njia hiyo.


2) Sababu ya pili ni kwamba hivi sasa umaskini nchini umekuwa wa
kiwango cha juu. Kila mtu anatafuta jawabu la umaskini wake kwa kudhani
kuwa umesababishwa na mfumo ulio nje ya maisha yake na ya serikali.
Katika hali hii wamejitokeza watanzania wenzetu wanaotafuta majibu
mepesi kwa kusingizia kuwa wamekuwa maskini kwasababu ya dini nyingine.
Hali hii imesababishwa na ukosefu wa elimu kiasi kwamba watanzania wengi
wanashindwa kuwa na uwezo wa kuchambua mambo kimantiki na badala yake
wanaamini bila kuchuja lolote wanaloambiwa na viongozi wa dini au
mwanasiasa au mwanaharakati. Ni vema watanzania wakajua kuwa ajenda ya
udini si ya dini fulani bali ni ya makundi machache ndani ya taasisi
zetu za dini. Tusibebeshe lawama za udini kwa dini fulani bali tuelewe
kuwa udini umekuwa ni mtazamo ya watu wachache ndani ya dini zetu.


3) Tatu, watanzania tumeanza kupoteza uelewa kuhusu madui wetu wa
asili ambao ni ujinga, umaskini na maradhi, na tumeongeza adui mwingine
ambaye ni imani ya mwingine. Tumeacha kuelekeza nguvu zetu katika
kupambana na maadui hao watatu na tunaelekeza nguvu zetu kupambana na
dini nyingine ambazo kimsingi haziwezi kuwa sababu ya matatizo yetu ya
kila siku.


Kwa bahati mbaya tunashindwa kuelewa kuwa dini hizi kuu mbili za
kikristo na kiislamu ni dini zilizozaliwa sehemu mmoja baadaye
zikasambaa sehemu tofauti na kuchukua utamaduni tofauti. Hatimaye
tunachokiona sasa, ndugu wa ukoo na hata kabila moja waliotokana na
historia moja, utamaduni mmoja na lugha moja wamefanywa maadui kwasababu
wanafuata dini tofauti.


4) Jambo la nne, nchi yetu imeruhusu uhuru wa kuanzisha taasisi za
dini pasipo kuwa na usimamizi wa karibu. Taasisi nyingi za kidini
zimeibuka nchini na zimekuwa chanzo kikubwa cha kuwagawa watanzania kwa
misingi ya kidini. Umoja wetu unapotea kwasababu baadhi ya taasisi za
kidini zilizopo zinawagawanya watanzania kwa misingi ya dini. Taasisi
nyingi za dini zinafundisha mbinu na namna ya kuwakabili waumini wa dini
nyingine badala ya kuhimiza upendo na mshikamano miongoni mwa
watanzania.
 
Acheni unafiki kuna kitu mnatafuta kwenye hili tamko lakini dhamira zenu zi wazi kuwa nyie ndio miongoni mwa waanzilishi wa huo udini. kuna wakti watu fulani toka chuo fulani walifika hapa tabora kwenye baadhi ya sekondari kuhubiri baadhi ya wanafunzi wakiiislamu na mliyoyasema mnayafahamu. Pimeni dhamira zenu na muwe wakweli nchi hii hamjaitendea haki. mmesoma shule za wakristo mmefika hapo vyuo vikuu mnarudi kusema wakristo wabaya sana
 
mimi nimeikubali sana hii ila serikali ingekua sikivu ingeyachukua yote haya na kuyafanyia kazi kwakweli udini makazini unaitafuna nchi yaani sasa hv elimu imekuwa si kigezo bali watu wanaangaliana kwa dini na ukabila ndipo wapeane vyeo makazini system nzima ya nchi imeharibika tunahitaji kiongozi asiye mwoga na mwenye msimamo na uwezo wa kukemea na kufanya maamuzi magumu mahala popote pale
 
Haina haja ya kupiga polojo za udini. chazaidi ni hii post ya wason kuwa na mapungfu coz imekaa kiumbea haina rejea na tafiti, ila ina hear says tu. "NO RESEARCH NO RIGHT TO SAY". hawa walitaka kusika kwny vyombo vya habar na hako ka umoja kao.
 
safi sana wana zuoni, mchango wenu umeonekana katika kuhimiza amani bila umwagaji wa damu, ni mjinga tena mburula wa kutupa ndio anaweza kupinga tamko lenu, kuna mijitu humu haijui msahafu wala biblia inavyoagiza kuishi kazi yao ni kupiga kelele na ushabiki usiokuwa na maana, hivi tuchukulie mfano vita ikaanza na ukaona jinsi mama, baba, wadogo zako, mkeo, na jamaa wa karibu wanapoteza maisha mbele yako utafanya nini!? Itakuwa ni uchungu usioweza kusahaulika hata kidogo, leo hii kuna watu wengi sana ambao ndugu na jamaa wapo dini nyingine mfano utakuta majina kama haya Michael Selemani, Abdallah John, Christina Zuberi, Khadija Steven, n.k hawa wote wamelelewa na wazazi wa dini nyingine hivyo sio vyema uanze kusema dini ya baba yako ni ya kifedhuri wakati kupitia dini hiyo amelelewa vyema mpaka imefika hali ya wewe kumpenda, kumuoa na kubadilisha dini yake. NI MPUMBAVU PEKEE NDIO ANAEWEZA KUWABEZA NDUGU ZAKE WATANZANIA NA KUSHABIKIA UDINI.
 
Freeland
Wasomi hawa wa UDSM wameeleza mambo ya msingi sana kwa ustawi wa taifa hili. Lkn ninataka kusema jambo moja muhimu ambalo kama hatutakuwa tayari kulitekeleza kwa vitendo usomi wetu utakuwa ni bure. Watz wengi hasa wasomi tumekosa kuwa wakweli kwa kila jambo tunalolisema au kulijadili. Watz tulitegemea wasomi wangesimamia kitu kinaitwa "kusema ukweli kwa kila jambo" lkn wameshindwa! Wasomi hawa pamoja na mawazo yao mazuri wameshindwa kusema ukweli uliowazi huu udini, ukabila au ukanda umepaliliwa na nani? Chama cha CCM kwa upofu wake kimekuwa kikieneza sumu ya udini, ukabils na ukanda pale ambapo kinaona kinazidiwa ushawishi na vyama vya upinzani. Kila mtu anajua CCM ilivoeneza swala udini kuhusu chama cha CUF mwaka 2005 kwenye uchaguzi mkuu baada ya CUF kuonekana kimepata nguvu na ushawishi kwa watz wengi. CCM ilirudie mbinu ile ile ya udini na ukanda kwa CDM kwa 2010. Narudia tena watz tunawategemea sana wasomi wetu lkn kama wanakuwa waoga kusema yalikweli kuhusu chanzo au kiini cha tatizo basi ni bora wangekaa kimya kwa sababu haya mawazo waliyoyasema yamesemwa na watu wengi tena wa kawaida. Taifa hili limeangushwa na wasomi kwa kiasi kikubwa kuogopa kusema ukweli pale watawala wanakwenda kinyume na matakwa ya watz wengi. Wasomi wengi wamekuwa wakipigana kila siku kuwa upande wa watawala badala ya kuwa upande wa raia wengi masikini!

Mkuu;Nadhani wameongelea hilo katika point ya kwanza kwa ya kwa nini haya yanatokea
 
Muasisi wa udini ni huyo baba yenu Nyerere that all..hakuna haja ya kumtafuta mchawi ni nani... Katika kuandika historia ya harakat za kupigania uhuru wa tz ye2 ndo hapo Huyo nyerere wenu alipoanza ku2bagua waislamu,alafu leo mnamtafuta mchawi ni nani? Shame on u?!!
 
Jumuiya ya wanataaluma wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (Udasa), imesema hakuna haja ya wanasiasa kufanya maandamano ya kupinga matokeo mabaya ya kidato cha nne na badala yake wanatakiwa kushirikiana na Watanzania kudai mfumo mpya wa elimu.


Mbali na hilo, wamesema kwa sasa wanatakiwa kusubiri majibu ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufuatilia chanzo cha wanafunzi wengi kufanya vibaya kwenye mitihani yao ili wajue tatizo.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dk Francis Michael wakati akitoa taarifa ya kukemea vitendo mbalimbali vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na baadhi ya watu.
 
Nimesoma mara kadhaa hii post,na nyingine ambazo umechangia ktk hii sredi,niseme wazi kwamba hata hao Waislamu wa Tanzania unaozungumzia haufahamu hata mazingira wanayoishi! Usipende kuchukulia matatizo yako binafsi,familia yako na eneo unalotokea kwamba yanawakilisha Waislamu wote ktk Tanzania. Kuna maeneo ktk Tanzania Waislamu walitambua elimu dunia mapema,na kamwe huwezi wasikia wanalalamika kama wewe! Kuna maeneo hapa Tanzania kama mikoa ya Pwani,Lindi na Mtwara wenyeji wake wanathamini kucheza ngoma,kuoa na kuolewa,issue ya shule siyo kipaumbele. Sasa kama hawa utasema mfumo umewabagua? Kuna sehemu ktk nchi yetu wao bila kujali dini zao,wao ni kufuga tu,elimu hawana habari. Hata mtoto akipelekwa shule kwa nguvu anatoroka. Mwisho niseme,changamoto kubwa mtu kupata/kukosa elimu wakati wa Mwl. Nyerere haikua dini ya mtu,bali ilikua tamaduni za jamii husika na uelewa juu ya umuhimu wa elimu kuanzia mtu binafsi na jamii husika.

Mwaka 1996 wakati namaliza shule ya msingi,wilaya ya kilwa mkoani Lindi ilikuwa na shule ya sekondari ya serikali moja yenye walimu wawili wakati wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ilikuwa na shule za sekondari za serikali zenye walimu wa kutosha 17(kumi na saba).Wakati huo wanafunzi tuliokuwa tunatoka mikioa ya kusini kwenda kusoma shule za bweni katika mikao mingine ilikuwa inatuchukua mwezi na zaidi ili tufike Dar wakati wa masika.


Baba wa kanisa Nyerere aling'oa reli Mtwara na akapiga marufuku kilimo cha pamba kanda ya kusini.Mataa ya uwanjwa wa ndege Mtwara yalihamishiwa Arusha,jenereta ya umeme ya kisasa ya mtwara ilihamishiwa Bukoba


Viwanda na mashamba ya mmonge Tanga Nyerer aliyaua kupitia vibaraka wake wa mfumo kristo.


Tabora ilikuwa kitivu cha harakati za uhuru,baada ya uhuru Nyerere akaiua Tabora kupitia vibaraka wake wa mfumi kristo


Shule zilizopo mkoa wa Pwani zimejazwa Wakristo kutoka mikoa ya Bara.


Serikali ya mfumo kristo tokea uhuru imefanya juhudi gani kuondoa upogo huu wa mgawanyo wa maendeleo katkia nchi hii,ndio kwanza maendeleo yanaelekezwa mikoa ya wikristo wengi na mikoa ya waislamu wengi inaachwa na kuambiwa ni wavivu wakati hawana miundombinu yoyote katika mikoa yao.


Naomba nipe mfano mmoja tu wa mkoa wenye waislamu wengi ulioendelea?Ni juhudu za mfumo kristo ulioasisiwa na Baba wa Kanisa Nyerere.


Tupigie Jicho upande wa Pili,mtoto aliyezaliwa katika familia ambayo ilisomeshwa na mfumo kristo kabla na baada ya uhuru,katika familia yao kuna watu wenye Phd zaidi ya watatu,madaktari,walimu,wahasibu,na watu wa fani mbali mbali,na mtoto aliyezaliwa katika familia iliyopigwa teke na mfumo kristo,familia ambayo,mama aliuza vitumbua,baba anetembeza njegere,mjomba anauza dagaa,je ni mtoto gani ambaye serikali inapasa ifanye juhudi kuhakikisha anasoma.


Niliongoza kimasomo kuanzia darasa la kwanza mpaka form two mama yangu akakosa shilingi 40000 ya ada ya shule,mama akalia sana,nikaenda wilayani kwetu na ripoti zangu,na kabla ya hapo wanajua nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa naongoza mitihani yote ya wilaya,huko nikakutana na mawakala wa mfumo kristo walinitukana na kunikejeli kwa sababu ya dini yangu.Nilishindwa kurudi shule mpaka form four mwezi wa sita ndio nikarudi shule,yaani nilikaa mwaka mmoja na nusa nyumbani bila ya kusoma,nikafanya mtihani wa form four nikapata division one point 17.


Jamani tuache porojo tuondoe mfumo kristo kwa ustawi wa taifa letu,namkumbuka second master wangu aliyekuwa wakala wa mfumo kristo alivyotutukana mimi na mama yangu kipindi kile aliponipeka shuleni form four tena tukiwa na barua ya wizara inayoelezea matatizo yangu.
 
Taarifa inajitosheleza kwakuwa lengo letu kama Watanzania tunaomba tuendelee kuishi kwa amani.Tumezoea kushirikiana pasipo kuangalia dini,rangi au kabila. Ila kwa mtazamo wangu,taarifa hii kuanzia kipengele cha Tufanyeje sehemu ya 3 juu ya kutoa elimu kwa usawa,hii naiona inachochea kilekile wanachokipinga:tuendelee kupewa elimu kwa kuulizwa wewe wa dini gani bila kujali uwezo au sifa za mhusika?
 
Chanzo cha udini hapa nchini ni wanasiasa,aliwahi sema siku moja jaji warioba kwamba udini unaanzishwa na wanasiasa,lakini watu wa kawaida wanashirikiana vizuri tu,wanapanda daladala pamoja wanakula pamoja,na mimi nakubaliana naye kabisa.SIASA na hasa CCM kuigeuza BAKWATA kama jumuiya yake ya nne ya kisiasa,ukiachilia mbali jumuiya zake kama wanawake,vijana na wazazi.
CCM.imekuwa ikiwadhalilisha waislam kwa kutumia BAKWATA kama wasemaji wa chama,mfano mzuri ni kule IGUNGA-BAKWATA wilaya walipojitokeza hadharani kuwashawishi wananchi waipigie kura CCM,na wasiipigie CHADEMA kwa kuwa ni maadui wa Uislam.
 
Ni wakati muafaka sasa kwa CCM kujitokeza hadharani kuwaomba radhi waislaam na watanzania kwa ujumla,kwa haya yanayotokea ya mauwaji ya kidini na hasa kwa kuigeuza BAKWATA kama JUMUIYA yake ya NNE ya kisisa.
 
Nchi hii ya ajabu sana,eti hivi sasa kuna watu wanajiita wasomi ndio wanauona udini,wanasema tunavunja misingi tuliaachiwa na Nyerere?Nchi hii kweli inawasomi wa ajabu!!!!!!!!!

Nchi hii udini umaasisiwa na Nyerere mwenyewe,ngoja niwakumbushe hawa wanaojiita wasomi hivyo hawajua kwamba kanisa Katoliki lipo kwenye mchakato wa kumpatia Utakatifu Baba wa Kanisa Nyerere kwa kazi nzuri aliyolifanyia kanisa Katoliki?Kwa michakato kama hii watu wakisema nchi hii inaendeshwa kwa mfumo kristo mutasema ni wachochezi?

Acha tuivunje hii misingi ya mfumo kristo aliyoiasisi Baba wa Kanisa Nyerere.Kama tunataka amani ya kweli lazima tuvunje hii misingi ya mfumo kristo tulioachiwa na Baba wa kanisa Nyerere kisha tujenge taifa la watanzania wote.

Tukikataa kujenga taifa la watanzia wote hivi sasa basi tutalijenga baada ya vita vya kidini kama walivyojenga Rwanda na Burundi baada ya vita vya kikabila.Dhambi ya ubaguzi aliyoiasisi Baba wa kanisa Nyerere ndio inayotumaliza

Karibuni wakereketwa wa kanisa lije kuwatoka povu kwa kunikejeli na kunadharua,vyovyote mutakavyosema mutambue sasa hivi waislamu tupo katika phase ya kujikomboa kutoka katika mfumo kandamizi mfumo kristo,tumechoka na huu mfumo lazima uvunje na kama hamutaki tutapigana vita vya kidini hapo.

wewe ni mchochezi mmojawapo na kwa taarifa yako wote mliotuma msg na post zenye sura ya kidini kama yako mtakuwa mahali salama zaidi mtoe maelezo yakutosha ! Punde 'take my word'
 
Hili tamko wala halijakaa kichuo kikuu kabisa. Kama mpaka UDSM nao wanatoa tamko light na empty kiasi hiki kwenye jambo zito na nyeti kama udini basi tuko pabaya mno...

Even fools critisize. What are your suggestions/opinions?
 
Back
Top Bottom