Wahadhiri UDSM Waongelea tatizo la Udini

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,233
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 2/3/2013

Utangulizi

Wapendwa waandishi wa habari. Tunaomba kupitia ninyi tuweze kuongea na watanzania wenzetu kuhusu hali ya amani ilivyo nchini mwetu kufuatia kila aina ya dalili ya watanzania kukosa uvumilivu wa kidini. Tunatambua kuwa serikali yetu imefanya mambo mazuri mengi tu nchini, hilo hatuna mashaka nalo; hata hivyo kama watanzania tunadhani kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa. Hivyo basi, tunaomba kuchukua nafasi hii kuelezea wasiwasi wetu kuhusu migogoro hii ya kidini inayozidi kukua nchini.

Migogoro hii ilianza kuvuka kama moshi lakini sasa inaanza kulipuka na kusambaa zaidi. Tumeshuhudia uchomaji moto wa kanisa kule Mbagala, kumwagiwa tindikali shekhe mmoja kule Zanzibar na Shekhe mwingine kuuawawa, kuchomwa makanisa Zanzibar, kupigwa risasi viongozi wa kikristo kule Zanzibar na pia mgogoro wa kuchinja huko Geita ambako tumeshuhudia mchungaji mmoja akiuawa.

Mbali na hayo, kuna matukio kadhaa kwenye shule zetu za sekondari yakihusisha migogoro ya kidini kati ya wakristo na waislamu. Haya tumeshahudia yakitokea sekondari za Bagamoyo, Ndanda, Kibiti, Ilboru na kwingineko. Pia yapo malalamiko yasiyo rasmi kuhusu udini kwenye sehemu za kazi na kwenye taasisi mbalimbali za serikali. Wapo wanaodai kuwa baadhi ya taasisi binafsi, za kidini na hata za serikali zinazohudumia watanzania wengi zimekuwa zikiajiri wafanyakazi kwa misingi ya kupendelea dini fulani fulani. Jambo hili hata kama ni la kuzungumzwa tu, ni vema likafanyiwa kazi maana hisia hizi zikipanuka hujenga chuki na kusababisha watanzania wasielewane.

Kwanini haya yanatokea?

Sisi wanajumuiya ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunaamini, kama taifa, kuna mahali tumechepuka na kuacha misingi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa katika ujenzi wa taifa imara na lenye umoja. Kuna sababu kadhaa zilizotufikisha hapa tulipo, nazo ni:

1) Wanasiasa na watanzania wengi tunafuata dini zetu kwa hisia zaidi pasipo kufikiri kwa kina kuhusu yale tunayoyafanya. Tumesahau kabisa kuwa dini ni kwaajili ya kutuhusianisha na ulimwengu ujao tusioujua. Tunapaswa kumheshimu na kumthamini kila binadamu aliyeko hapa duniani. Kwa bahati mbaya baadhi yetu tunadhani kuwa ulimwengu huu umeumbwa kwaajili ya dini fulani na binadamu wengine hawana haki ya kufurahia maisha yao hapa duniani. Tunataka kutumia dini zetu kumiliki utawala wa dunia hii.

Dini zetu zimekuwa mtaji kwa baadhi ya wanasiasa na vyama vyao. Inasikitisha kuwa hakuna jitihada za kutosha zilizofanyika kuzuia wanasiasa kutumia dini kama sera au ajenda ya katika kupata kura. Baadhi ya wanasiasa wameingia madarakani kwa kutumia udini na ukabila na hivyo hali inapofikia watanzania kuanza kuchukiana kwa misingi ya dini wanakosa nguvu na ujasiri wa kukemea na kuzuia haya kwakuwa nao wamepitia njia hiyo.

2) Sababu ya pili ni kwamba hivi sasa umaskini nchini umekuwa wa kiwango cha juu. Kila mtu anatafuta jawabu la umaskini wake kwa kudhani kuwa umesababishwa na mfumo ulio nje ya maisha yake na ya serikali. Katika hali hii wamejitokeza watanzania wenzetu wanaotafuta majibu mepesi kwa kusingizia kuwa wamekuwa maskini kwasababu ya dini nyingine. Hali hii imesababishwa na ukosefu wa elimu kiasi kwamba watanzania wengi wanashindwa kuwa na uwezo wa kuchambua mambo kimantiki na badala yake wanaamini bila kuchuja lolote wanaloambiwa na viongozi wa dini au mwanasiasa au mwanaharakati. Ni vema watanzania wakajua kuwa ajenda ya udini si ya dini fulani bali ni ya makundi machache ndani ya taasisi zetu za dini. Tusibebeshe lawama za udini kwa dini fulani bali tuelewe kuwa udini umekuwa ni mtazamo ya watu wachache ndani ya dini zetu.

3) Tatu, watanzania tumeanza kupoteza uelewa kuhusu madui wetu wa asili ambao ni ujinga, umaskini na maradhi, na tumeongeza adui mwingine ambaye ni imani ya mwingine. Tumeacha kuelekeza nguvu zetu katika kupambana na maadui hao watatu na tunaelekeza nguvu zetu kupambana na dini nyingine ambazo kimsingi haziwezi kuwa sababu ya matatizo yetu ya kila siku.

Kwa bahati mbaya tunashindwa kuelewa kuwa dini hizi kuu mbili za kikristo na kiislamu ni dini zilizozaliwa sehemu mmoja baadaye zikasambaa sehemu tofauti na kuchukua utamaduni tofauti. Hatimaye tunachokiona sasa, ndugu wa ukoo na hata kabila moja waliotokana na historia moja, utamaduni mmoja na lugha moja wamefanywa maadui kwasababu wanafuata dini tofauti.

4) Jambo la nne, nchi yetu imeruhusu uhuru wa kuanzisha taasisi za dini pasipo kuwa na usimamizi wa karibu. Taasisi nyingi za kidini zimeibuka nchini na zimekuwa chanzo kikubwa cha kuwagawa watanzania kwa misingi ya kidini. Umoja wetu unapotea kwasababu baadhi ya taasisi za kidini zilizopo zinawagawanya watanzania kwa misingi ya dini. Taasisi nyingi za dini zinafundisha mbinu na namna ya kuwakabili waumini wa dini nyingine badala ya kuhimiza upendo na mshikamano miongoni mwa watanzania.

Baadhi ya viongozi wa taasisi hizo wamewafanya watanzania mtaji wao kwa kuwachochea wafuasi wao kuwachukia wengine kwa lengo la kutimiza haja zao binafsi. Watanzania tunapaswa kuzinduka na kuchukua tahadhari dhidi ya watu wanaotuchonganisha. Tukumbuke kuwa kiongozi wa dini anayekuambia kuwa dini fulani ni ya kishenzi na wafuasi wake ni wa kishenzi basi mtu huyo si mtumishi wa Mungu bali anatumikia maslahi yake.

Tufanyeje?

Baada ya kueleza sababu zilizotufanya tufikie hapa tulipo sasa, sisi wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunapendekeza mambo yafuatayo:

1) Serikali isimamie na kudhibiti vyombo vya habari vya kidini vinavyochochea chuki za kidini. Inasikitisha kuwa serikali iliyosheheni wataalamu wa kila aina inashindwa kutambua madhara ya uchochezi wa vyombo vya habari. Watanzania tunapaswa kujifunza kuwa hata mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda hayakuanza siku moja, yalichochewa na vyombo vya habari kwa muda mrefu na vyombo hivyo vilihamasisha pia mauaji hayo.

Hata hapa nchini kwetu, serikali isipokuwa tayari kukemea na kufungia vyombo vya habari vinavyotumia udini kuleta uchochezi, ipo siku watanzania watauana sana na nchi itapoteza heshima yake ya kuwa taifa la amani na tutakuwa wakimbizi. Tunaishangaa serikali inaweza kuyafungia magazeti yanayoikosoa lakini haiko tayari kuyafungia magazeti yanawachochea watanzania.

Tungependa ujasiri unaotumika na vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaoandika ujumbe wa vitisho kwa viongozi wa kisiasa nchini utumike pia kuwakamata wanaochochea uvunjifu wa amani. Kama tunaweza kuwalinda viongozi dhidi ya vitisho kwa maisha yao binafsi kwanini tushindwe kulilinda taifa letu kwa kutumia nguvu hizo hizo za kuwatumikia wanasiasa?

2) Pia tunatoa wito kwa wanasiasa na watanzania kwa ujumla kuwakataa wale wanaotafuta vyeo mahali popote pale, iwe kwenye vyama vya siasa au taasisi, kwa kutumia udini kama kigezo cha kutaka kuchaguliwa. Ni wakati muafaka sasa kuhuisha yale yote yatakayoleta mtangamano wa kitaifa. Kama taifa tumeacha misingi mizuri ya ujenzi wa taifa tuliloachiwa na waasisi wa taifa hili.

3) Jambo jingine ni kuhamasisha na kusimamia sera ya elimu sawa kwa wote. Elimu yetu ya sasa imejenga matabaka makubwa miongoni mwa watanzania na matokeo yake matabaka haya yanajitokeza zaidi katika sura ya udini. Kutokana na hali hii watanzania wengi waliokosa elimu wanadhani kuwa wenzao wa dini nyingine wanafanikiwa kwasababu ya upendeleo wa kidini. Kwa kusisitiza katika elimu, itakuwa rahisi kwa watanzania kuelimishwa kuwa chuki za kidini si msingi wa dini zetu tofauti na ilivyo sasa ambapo ukosefu wa elimu unawafanya wengi kuwa waathirika wa mafundisho potofu.

4) Pia tunaisihi serikali iwachunguze viongozi wa baadhi ya taasisi za kidini zinazowahamasiha wafuasi wake kufanya vitendo vya uhalifu. Ni vigumu sana kuwadhibiti wafuasi wa taasisi ya kidini ambao wameshakuwa na nguvu ya kuungana na kufanya jambo lolote baya. Tuna wasiwasi kuwa baadhi ya viongozi wa taasisi hizo wanatumika na watu wa nje kuvuruga amani yetu. Kwa bahati mbaya viongozi hawa wanajua wazi kuwa amani ikivurugika nchini wao wanazo sehemu za kukimbilia wakati ndugu zetu wakiendelea kuuana.

Wito wetu kwa watanzania wenzetu ni kwamba wajue kuwa viongozi wa kidini wanaowachochea kuwachukia wengine hawana nia njema na taifa na maisha yao. Watatuacha tukiliangamiza taifa huku wao wakiwa salama. Ni vema watanzania wakajua kuwa sababu ya umaskini na matatizo ya kimaisha hayajasababishwa na waumini wa dini nyingine bali mfumo wetu mbovu wa utawala unaoacha kukua kwa matabaka ya kijamii. Tukishirikiana sote kupambana na umaskini hakutakuwa na sababu ya kuchukiana. Pia, ni muhimu sasa, kila dini iendeshe maswala yake bila kutaka kubebwa na serikali.

Source;Nilikuwepo
 
Ukweli na tatizo letu na adui namba moja ni UMASIKINI sio dini,wala kabila au kanda yoyote ya nchi,na haya yana sababishwa na viongozi wetu,kama kweli tunapinga udini na ukabila,kuanzia leo tupinge machapicho yote katika maofisi(form za maelezo binafsi)kuwa na kipengele cha dini,na makabila kiondolewe,sijajua kina umuhimu gani katka form za ajira,maombi ya kujiunga na masomo,wakati serikali haina dini,kuna baadhi ya viongozi wamechangia kuingiza hilikatika nchi yetu,kuna baadhi ya viongozi walisema CUF ni chama cha dini fulani,pia wanasema CDM nao chama cha dini fulani,siwai kusikia wapinzani wakisema CCM ni chama cha dini fulan,leo watoke barazan na waombe radi watanzania,mwisho,UMASIKINI HAUNA DINI WALA KABILA,UJINGA HAUNA DINI WALA KABILA,NK
 
Binafsi naona tamko zuri! Kuna eneo moja tu wamekose, kwenye mapendekezo na. 3 utofauti wa kielimu kati ya dini hizi ulianza enzi za ukoloni! Hivyo baada ya uhuru uliendelea na kuendelezwa!
 
Wamesema mambo mazuri yaliyozoeleka, "they are neither new nor original" bado tunaendelea kusubiri MATAMKO mengine!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 2/3/2013

Utangulizi

Wapendwa waandishi wa habari. Tunaomba kupitia ninyi tuweze kuongea na watanzania wenzetu kuhusu hali ya amani ilivyo nchini mwetu kufuatia kila aina ya dalili ya watanzania kukosa uvumilivu wa kidini. Tunatambua kuwa serikali yetu imefanya mambo mazuri mengi tu nchini, hilo hatuna mashaka nalo; hata hivyo kama watanzania tunadhani kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa. Hivyo basi, tunaomba kuchukua nafasi hii kuelezea wasiwasi wetu kuhusu migogoro hii ya kidini inayozidi kukua nchini.

Migogoro hii ilianza kuvuka kama moshi lakini sasa inaanza kulipuka na kusambaa zaidi. Tumeshuhudia uchomaji moto wa kanisa kule Mbagala, kumwagiwa tindikali shekhe mmoja kule Zanzibar na Shekhe mwingine kuuawawa, kuchomwa makanisa Zanzibar, kupigwa risasi viongozi wa kikristo kule Zanzibar na pia mgogoro wa kuchinja huko Geita ambako tumeshuhudia mchungaji mmoja akiuawa.

Mbali na hayo, kuna matukio kadhaa kwenye shule zetu za sekondari yakihusisha migogoro ya kidini kati ya wakristo na waislamu. Haya tumeshahudia yakitokea sekondari za Bagamoyo, Ndanda, Kibiti, Ilboru na kwingineko. Pia yapo malalamiko yasiyo rasmi kuhusu udini kwenye sehemu za kazi na kwenye taasisi mbalimbali za serikali. Wapo wanaodai kuwa baadhi ya taasisi binafsi, za kidini na hata za serikali zinazohudumia watanzania wengi zimekuwa zikiajiri wafanyakazi kwa misingi ya kupendelea dini fulani fulani. Jambo hili hata kama ni la kuzungumzwa tu, ni vema likafanyiwa kazi maana hisia hizi zikipanuka hujenga chuki na kusababisha watanzania wasielewane.

Kwanini haya yanatokea?

Sisi wanajumuiya ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunaamini, kama taifa, kuna mahali tumechepuka na kuacha misingi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa katika ujenzi wa taifa imara na lenye umoja. Kuna sababu kadhaa zilizotufikisha hapa tulipo, nazo ni:

1) Wanasiasa na watanzania wengi tunafuata dini zetu kwa hisia zaidi pasipo kufikiri kwa kina kuhusu yale tunayoyafanya. Tumesahau kabisa kuwa dini ni kwaajili ya kutuhusianisha na ulimwengu ujao tusioujua. Tunapaswa kumheshimu na kumthamini kila binadamu aliyeko hapa duniani. Kwa bahati mbaya baadhi yetu tunadhani kuwa ulimwengu huu umeumbwa kwaajili ya dini fulani na binadamu wengine hawana haki ya kufurahia maisha yao hapa duniani. Tunataka kutumia dini zetu kumiliki utawala wa dunia hii.

Dini zetu zimekuwa mtaji kwa baadhi ya wanasiasa na vyama vyao. Inasikitisha kuwa hakuna jitihada za kutosha zilizofanyika kuzuia wanasiasa kutumia dini kama sera au ajenda ya katika kupata kura. Baadhi ya wanasiasa wameingia madarakani kwa kutumia udini na ukabila na hivyo hali inapofikia watanzania kuanza kuchukiana kwa misingi ya dini wanakosa nguvu na ujasiri wa kukemea na kuzuia haya kwakuwa nao wamepitia njia hiyo.

2) Sababu ya pili ni kwamba hivi sasa umaskini nchini umekuwa wa kiwango cha juu. Kila mtu anatafuta jawabu la umaskini wake kwa kudhani kuwa umesababishwa na mfumo ulio nje ya maisha yake na ya serikali. Katika hali hii wamejitokeza watanzania wenzetu wanaotafuta majibu mepesi kwa kusingizia kuwa wamekuwa maskini kwasababu ya dini nyingine. Hali hii imesababishwa na ukosefu wa elimu kiasi kwamba watanzania wengi wanashindwa kuwa na uwezo wa kuchambua mambo kimantiki na badala yake wanaamini bila kuchuja lolote wanaloambiwa na viongozi wa dini au mwanasiasa au mwanaharakati. Ni vema watanzania wakajua kuwa ajenda ya udini si ya dini fulani bali ni ya makundi machache ndani ya taasisi zetu za dini. Tusibebeshe lawama za udini kwa dini fulani bali tuelewe kuwa udini umekuwa ni mtazamo ya watu wachache ndani ya dini zetu.

3) Tatu, watanzania tumeanza kupoteza uelewa kuhusu madui wetu wa asili ambao ni ujinga, umaskini na maradhi, na tumeongeza adui mwingine ambaye ni imani ya mwingine. Tumeacha kuelekeza nguvu zetu katika kupambana na maadui hao watatu na tunaelekeza nguvu zetu kupambana na dini nyingine ambazo kimsingi haziwezi kuwa sababu ya matatizo yetu ya kila siku.

Kwa bahati mbaya tunashindwa kuelewa kuwa dini hizi kuu mbili za kikristo na kiislamu ni dini zilizozaliwa sehemu mmoja baadaye zikasambaa sehemu tofauti na kuchukua utamaduni tofauti. Hatimaye tunachokiona sasa, ndugu wa ukoo na hata kabila moja waliotokana na historia moja, utamaduni mmoja na lugha moja wamefanywa maadui kwasababu wanafuata dini tofauti.

4) Jambo la nne, nchi yetu imeruhusu uhuru wa kuanzisha taasisi za dini pasipo kuwa na usimamizi wa karibu. Taasisi nyingi za kidini zimeibuka nchini na zimekuwa chanzo kikubwa cha kuwagawa watanzania kwa misingi ya kidini. Umoja wetu unapotea kwasababu baadhi ya taasisi za kidini zilizopo zinawagawanya watanzania kwa misingi ya dini. Taasisi nyingi za dini zinafundisha mbinu na namna ya kuwakabili waumini wa dini nyingine badala ya kuhimiza upendo na mshikamano miongoni mwa watanzania.

Baadhi ya viongozi wa taasisi hizo wamewafanya watanzania mtaji wao kwa kuwachochea wafuasi wao kuwachukia wengine kwa lengo la kutimiza haja zao binafsi. Watanzania tunapaswa kuzinduka na kuchukua tahadhari dhidi ya watu wanaotuchonganisha. Tukumbuke kuwa kiongozi wa dini anayekuambia kuwa dini fulani ni ya kishenzi na wafuasi wake ni wa kishenzi basi mtu huyo si mtumishi wa Mungu bali anatumikia maslahi yake.

Tufanyeje?

Baada ya kueleza sababu zilizotufanya tufikie hapa tulipo sasa, sisi wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunapendekeza mambo yafuatayo:

1) Serikali isimamie na kudhibiti vyombo vya habari vya kidini vinavyochochea chuki za kidini. Inasikitisha kuwa serikali iliyosheheni wataalamu wa kila aina inashindwa kutambua madhara ya uchochezi wa vyombo vya habari. Watanzania tunapaswa kujifunza kuwa hata mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda hayakuanza siku moja, yalichochewa na vyombo vya habari kwa muda mrefu na vyombo hivyo vilihamasisha pia mauaji hayo.

Hata hapa nchini kwetu, serikali isipokuwa tayari kukemea na kufungia vyombo vya habari vinavyotumia udini kuleta uchochezi, ipo siku watanzania watauana sana na nchi itapoteza heshima yake ya kuwa taifa la amani na tutakuwa wakimbizi. Tunaishangaa serikali inaweza kuyafungia magazeti yanayoikosoa lakini haiko tayari kuyafungia magazeti yanawachochea watanzania.

Tungependa ujasiri unaotumika na vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaoandika ujumbe wa vitisho kwa viongozi wa kisiasa nchini utumike pia kuwakamata wanaochochea uvunjifu wa amani. Kama tunaweza kuwalinda viongozi dhidi ya vitisho kwa maisha yao binafsi kwanini tushindwe kulilinda taifa letu kwa kutumia nguvu hizo hizo za kuwatumikia wanasiasa?

2) Pia tunatoa wito kwa wanasiasa na watanzania kwa ujumla kuwakataa wale wanaotafuta vyeo mahali popote pale, iwe kwenye vyama vya siasa au taasisi, kwa kutumia udini kama kigezo cha kutaka kuchaguliwa. Ni wakati muafaka sasa kuhuisha yale yote yatakayoleta mtangamano wa kitaifa. Kama taifa tumeacha misingi mizuri ya ujenzi wa taifa tuliloachiwa na waasisi wa taifa hili.

3) Jambo jingine ni kuhamasisha na kusimamia sera ya elimu sawa kwa wote. Elimu yetu ya sasa imejenga matabaka makubwa miongoni mwa watanzania na matokeo yake matabaka haya yanajitokeza zaidi katika sura ya udini. Kutokana na hali hii watanzania wengi waliokosa elimu wanadhani kuwa wenzao wa dini nyingine wanafanikiwa kwasababu ya upendeleo wa kidini. Kwa kusisitiza katika elimu, itakuwa rahisi kwa watanzania kuelimishwa kuwa chuki za kidini si msingi wa dini zetu tofauti na ilivyo sasa ambapo ukosefu wa elimu unawafanya wengi kuwa waathirika wa mafundisho potofu.

4) Pia tunaisihi serikali iwachunguze viongozi wa baadhi ya taasisi za kidini zinazowahamasiha wafuasi wake kufanya vitendo vya uhalifu. Ni vigumu sana kuwadhibiti wafuasi wa taasisi ya kidini ambao wameshakuwa na nguvu ya kuungana na kufanya jambo lolote baya. Tuna wasiwasi kuwa baadhi ya viongozi wa taasisi hizo wanatumika na watu wa nje kuvuruga amani yetu. Kwa bahati mbaya viongozi hawa wanajua wazi kuwa amani ikivurugika nchini wao wanazo sehemu za kukimbilia wakati ndugu zetu wakiendelea kuuana.

Wito wetu kwa watanzania wenzetu ni kwamba wajue kuwa viongozi wa kidini wanaowachochea kuwachukia wengine hawana nia njema na taifa na maisha yao. Watatuacha tukiliangamiza taifa huku wao wakiwa salama. Ni vema watanzania wakajua kuwa sababu ya umaskini na matatizo ya kimaisha hayajasababishwa na waumini wa dini nyingine bali mfumo wetu mbovu wa utawala unaoacha kukua kwa matabaka ya kijamii. Tukishirikiana sote kupambana na umaskini hakutakuwa na sababu ya kuchukiana. Pia, ni muhimu sasa, kila dini iendeshe maswala yake bila kutaka kubebwa na serikali.

Source;Nilikuwepo

Tatizo ni kwamba, vikundi vyote vinavyo laani udini hapa nchini, havija kuwa tayari kumtaja/kuwataja vinara waliopandikiza UDINI hapa nchini. Tangu 2010 wapo watu wametumia karata ya UDINI ili kuingia madarakani. Na ili kujilinda na zimwi la UDINI, wameendelea kutumia AGENDA hiyo hiyo kuhubiri kwenye majukwaa ya kisiasa ili kujengea watu wengine taswira ya UDINI. Sasa wameona mbegu waliyo ipanda wakati wanatafuta uongozi inaanza kutoa mavuno, wanatufanyia tamthilia ya kwamba nao ni miongoni mwetu katika masikitiko ya ubaguzi wa KIDINI.

Hivi kweli kama UDINI ungekuwa umeanzishwa na watu ambao si viongozi, mustakabali wa watu hawa ungekuwa je?? Kila kukicha wapo watu waliopewa dhamana kuongoza nchi hii ambao wamekuwa waki u-hubiri UDINI na hasa kwenye hotuba zao ama za kisiasa au za maendeleo ya wananchi.

Na bahati mbaya sana wapo baadhi ya watu ambao pia si viongozi wa wananchi nao wameamua kuuhubiri UDINI, huku viongozi wanao jifanya kuukemea UDINI waki waangalia na kuwasilkiliza kila siku (pia naweza kusema wakiwaunga mkono). Tumeshuhudia Radio, nakala za CD, Magazeti, Vijarida, n.k. vyote hivi vikihubiri UDINI bila hatua stahiki kuchukuliwa dhidi ya vyombo hivi.

Kwenye baadhi ya nyumba za ibada, kumekuwepo na mahubiri ya ubaguzi wa kidini bila kificho na hakuna hatua zilizo chukuliwa dhidi ya wahusika.

Kama kweli tunataka kuondokana na huu mzizi wa fitina ya UDINI ifike mahali taasisi zinazo toa matamko zisiishie kuuzungumzia UDINI tu, bali pia ziwataje waasisi wa dhambi hii ya UDINI.

Inajulikana wazi kwamba, kama UDINI ungekuwa umeasisiwa na mtu/watu ambao hawana dhamana ya uongozi, watu hao wangekuwa wanaishi mahali pengine ambapo sio uraiani (gerezani).
 
Ni aibu na kujidhalilisha kwa wasomi hawa kukaa chini na kujadili chanzo cha ukosefu wa amani bila ya kuitaja DHULMA ambayo ndicho chanzo kikuu.
 
Tamko lao limesimama vizuri, kipengele no. (4) kinachohusu kuingia/kuanzishwa kwa taasisi za kidini hapa tz, hapa tumeona matokeo, rais Kikwete nimemsikia akilalamika kuna taasisi zinapewa fedha kuchafua amani ya nchi...ni hatari rais anakiri nchi kuvamiwa lakini hachukui hatua, TIS wamelala?..mkuu tis yuko ibadani?(kukumbatia kila muislam haijalishi ni nani na katoka wapi) tumefungua milango makusudi au bahati mbaya...salafi ni aina ya mafunzo ambayo hata mosad hawataki syria iangukie kwayo..sasa tunaona rabsha ndogo tu watu WAKICHINJWA koromeo hadi kutenganisha kichwa na mwili...watz tusikubali, waislam wasikubali izaliwe boko haram ktk ardhi ya tz.
 
Tatizo ni kwamba, vikundi vyote vinavyo laani udini hapa nchini, havija kuwa tayari kumtaja/kuwataja vinara waliopandikiza UDINI hapa nchini. Tangu 2010 wapo watu wametumia karata ya UDINI ili kuingia madarakani. Na ili kujilinda na zimwi la UDINI, wameendelea kutumia AGENDA hiyo hiyo kuhubiri kwenye majukwaa ya kisiasa ili kujengea watu wengine taswira ya UDINI. Sasa wameona mbegu waliyo ipanda wakati wanatafuta uongozi inaanza kutoa mavuno, wanatufanyia tamthilia ya kwamba nao ni miongoni mwetu katika masikitiko ya ubaguzi wa KIDINI.

Hivi kweli kama UDINI ungekuwa umeanzishwa na watu ambao si viongozi, mustakabali wa watu hawa ungekuwa je?? Kila kukicha wapo watu waliopewa dhamana kuongoza nchi hii ambao wamekuwa waki u-hubiri UDINI na hasa kwenye hotuba zao ama za kisiasa au za maendeleo ya wananchi.

Na bahati mbaya sana wapo baadhi ya watu ambao pia si viongozi wa wananchi nao wameamua kuuhubiri UDINI, huku viongozi wanao jifanya kuukemea UDINI waki waangalia na kuwasilkiliza kila siku (pia naweza kusema wakiwaunga mkono). Tumeshuhudia Radio, nakala za CD, Magazeti, Vijarida, n.k. vyote hivi vikihubiri UDINI bila hatua stahiki kuchukuliwa dhidi ya vyombo hivi.

Kwenye baadhi ya nyumba za ibada, kumekuwepo na mahubiri ya ubaguzi wa kidini bila kificho na hakuna hatua zilizo chukuliwa dhidi ya wahusika.

Kama kweli tunataka kuondokana na huu mzizi wa fitina ya UDINI ifike mahali taasisi zinazo toa matamko zisiishie kuuzungumzia UDINI tu, bali pia ziwataje waasisi wa dhambi hii ya UDINI.

Inajulikana wazi kwamba, kama UDINI ungekuwa umeasisiwa na mtu/watu ambao hawana dhamana ya uongozi, watu hao wangekuwa wanaishi mahali pengine ambapo sio uraiani (gerezani).

Kwa maelezo yako basi pendekezo la nini kifanyike namba 4 lirekebishwe na kuongeza Serkali iwachunguze na viongozi wa Serkali ambao wanachochea udini waziwazi au kwa kificho - na au hata kwa kutofanya chochote kuzuia gonjwa hili. tatizo ni nani katika Serkali atafanya hii kazi?
 
I said just about the same, in not so many words.

Hao wahadhiri hawana majina?
 
Ni aibu na kujidhalilisha kwa wasomi hawa kukaa chini na kujadili chanzo cha ukosefu wa amani bila ya kuitaja DHULMA ambayo ndicho chanzo kikuu.
huo ndo mtizamo wako,wao pia wametoa kulingana na mtizamo wao!si lazima mitizamo yenu iwe sawa!na hapo ndipo penye tatizo la kutoheshimu tofauti za kimsimamo!!
 
I said just about the same, in not so many words.

Hao wahadhiri hawana majina?
wamesema ni tamko la UDASA kwa hiyo ni jumuia yote ya wana taaluma and no body in particular!
 
Jambo la ajabu, hawajaitaja CCM kuwa ndo chanzo. Why?
 
Serikali ya leo sio ya keambiwa kwa matamko ni ya kuambiwa kwa vitendo. Kama wanataka tamko lao lichukuliwe serious Jumatatu waangoze maandamano kuelekea mambo ya ndani kwa waziri mwenye zamana na wakamsomee tamko hilo.
 
Kiongozi namba moja wa Taifa, Kiongozi namba mbili wa Taifa, wa tatu, ... viongozi, viongozi ... Uongozi wa Juu Wa Taifa ... KAULI ZAO DHATI ... NDIO SULIHISHO! Kutoka Mioyoni Mwao wakamate Microphone ...Mbele ya Watanzania ... Waangalie Macho ya Watanzania bila kupepesa Macho yao ... Wakemee UDINI ..WITH SUPERB FORCE ... THE TOUGH LOVE ...!! Wakemeee kwa kumaanisha sio with weak tone, wimpy and compromisingly ..wakemee objectively toka mioyoni mwao... !!
 
wamesema ni tamko la UDASA kwa hiyo ni jumuia yote ya wana taaluma and no body in particular!

Wapi wamesema ni tamko la UDASA? Na hao waliosema hivyo ni kina nani?

Tamko linawezaje kuwa la jumuiya yote bila ya kuwa la nobody in particular? Unaweza kuwa na maprofesa kumi wa UDSM halafu individually wasiwe maprofesa?

Kama tamko ni la jumuiya ni la wote, si la nobody in particular.

Nani katoa? Wapi sahihi/jina/anuani?
 
nadhani unataka ku-prolong mjadala!

Mjadala ndio lengo la JF.

Mimi nataka kujua ambacho sijajua ndio maana nauliza, kama umekosea, au huna jibu sema tu.

Kama unalo jibu toa.

Tusije kulaumu Form Four wanaopata division zero tu kumbe hata hapa JF comprehension za wengine ni zile zile tu.

Wapi imesemwa hili ni tamko la UDASA? Nani kasema hilo?

Maana isije kuwa mtu kakaa kwenye keyboard yake, katupa kitu JF, watu wanakibugia chapchap bila kuliza maswali.

Na wakiuliza maswali wanaambiwa "wanataka kuendeleza mjadala".

Kama vile JF imeanzishwa ili kuzima mijadala!
 
Mjadala ndio lengo la JF.

Tusije kulaumu Form Four wanaopata division zero tu kumbe hata hapa JF comprehension za wengine ni zile zile tu.
aiss kweli!!!!huenda na wewe ukawa kati ya hao waliopata ziro!!rudi tena hapo kwenye habari kuu,soma paragraph ya nne inayo anza na sub heading Kwanini haya yanatokea?lakini pia jamiiforums siyo box tembea na kwingine!!TAMKO LA UDASA JUU YA UCHOCHEZI WA UDINI TANZANIA - Bongo 61 ..:: Exclusive News | Sports | Celebrity News | Fashion | Jobs | Entertainment.
 
Nchi hii ya ajabu sana,eti hivi sasa kuna watu wanajiita wasomi ndio wanauona udini,wanasema tunavunja misingi tuliaachiwa na Nyerere?Nchi hii kweli inawasomi wa ajabu!!!!!!!!!

Nchi hii udini umaasisiwa na Nyerere mwenyewe,ngoja niwakumbushe hawa wanaojiita wasomi hivyo hawajua kwamba kanisa Katoliki lipo kwenye mchakato wa kumpatia Utakatifu Baba wa Kanisa Nyerere kwa kazi nzuri aliyolifanyia kanisa Katoliki?Kwa michakato kama hii watu wakisema nchi hii inaendeshwa kwa mfumo kristo mutasema ni wachochezi?

Acha tuivunje hii misingi ya mfumo kristo aliyoiasisi Baba wa Kanisa Nyerere.Kama tunataka amani ya kweli lazima tuvunje hii misingi ya mfumo kristo tulioachiwa na Baba wa kanisa Nyerere kisha tujenge taifa la watanzania wote.

Tukikataa kujenga taifa la watanzia wote hivi sasa basi tutalijenga baada ya vita vya kidini kama walivyojenga Rwanda na Burundi baada ya vita vya kikabila.Dhambi ya ubaguzi aliyoiasisi Baba wa kanisa Nyerere ndio inayotumaliza

Karibuni wakereketwa wa kanisa lije kuwatoka povu kwa kunikejeli na kunadharua,vyovyote mutakavyosema mutambue sasa hivi waislamu tupo katika phase ya kujikomboa kutoka katika mfumo kandamizi mfumo kristo,tumechoka na huu mfumo lazima uvunje na kama hamutaki tutapigana vita vya kidini hapo.
 
aiss kweli!!!!huenda na wewe ukawa kati ya hao waliopata ziro!!rudi tena hapo kwenye habari kuu,soma paragraph ya nne inayo anza na sub heading Kwanini haya yanatokea?lakini pia jamiiforums siyo box tembea na kwingine!!TAMKO LA UDASA JUU YA UCHOCHEZI WA UDINI TANZANIA - Bongo 61 ..:: Exclusive News | Sports | Celebrity News | Fashion | Jobs | Entertainment.

Sisi wanajumuiya ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunaamini, kama taifa, kuna mahali tumechepuka na kuacha misingi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa katika ujenzi wa taifa imara na lenye umoja. Kuna sababu kadhaa zilizotufikisha hapa tulipo, nazo ni:

Mie nikafikili unanipa link ya website rasmi ya UDASA, kumbe ki link cha blog ya blogspot kinachorudia habari hii hii isiyo na jina wala anuani?

Tamko la UDASA kwa vyombo vya habari lina jina la nani? Limetiwa sahihi na nani?

Tutajua vipi kwamba hili ni tamko la UDASA na si propaganda za baadhi tu ya wahadhiri au worse still, muhuni mmoja tu anafanya satire kwamba wahadhiri wanatakiwa kuandika hivi lakini hawajaandika?

Hizi habari za kutoa matamko kwenye vyombo vya habari bila kutoa hata jina la muwakilishi anayetoa habari ndio usomi wenyewe huu? Nimeangalia hata huko kwenye link uliyotoa hakuna jina wala ofisi, nitajuaje kama huko nako hawaja copy hapa JF? Au hawajawa duped the same way kama JF tulivyoletewa habari isiyo kamili?

Sasa hapo kwa kauli hizi zisizo majina wala ofisi zilikotoka, UDASA na Kiranga unayemsema wana tofauti gani?
 
Back
Top Bottom