Wahadhiri kuomba kuongezewa muda wa kustaafu kutoka miaka 60 hadi 70

georgeallen

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
4,118
1,870
Nimemsoma mkuu wa chuo kikuu huria cha Tanzania, OUT akimuomba makamu wa Rais, Mh Mpango awaongezee wahadhiri wa vyuo vikuu muda wa kustaafu Kutoka miaka 60 ya sasa hadi miaka 70.

Kwa kuwa umri wa kuishi kwa mtanzania ni miaka 65, kuna faida yoyote kuwaongezea umri wa kustaafu wahadhiri hao?

Ni yapi madhara ya kuwaongezea umri wa kustaafu na upatikanaji wa ajira za kada hiyo katika vyuo vya Serikali?

Je, mhadhiri wa chuo ufanisi wake kikazi hauna kikomo?

Kuna madhara gani ya kuwaongezea muda wa kustaafu na kuwaacha kada nyingine wakistaafu at 60?
 
Kikawaida ujuzi huwa hauzeeki ila kinacho pungua ni efficiency, hivyo kama ulikuwa unatumie Dakika 50 kusahihisha mitihani ya wanafunzi 50 kuba wakati utafika utayumia Dakika 100 na zaidi kusahihisha hio mitihani.

Ujue Unapo ajiliwa huwa Mwajili ana nunua muda wako, na si vinginevyo, wala sio ujuzi wako hapana bali ni muda, Sasa kuna wakati unafika Muda wako unakiwa ni hasara kwa mwajili wako, ila still bado una ujuzi make ujuzi hauzeeki. Kinacho zeeka ni muda.
 
Waongezewe mpaka 65 tu.

Walifelisha sana wanafunzi wa kuziba nafasi zao, wamejikuta Wana upungufu wa wahadhiri.

65 na kuendelea waanzishe research institutions, wapige consultants. Mwisho, wawe wanajiandaa kimaisha, unakaaje ofisini mpaka unatembela fimbo.
Magu aliwaongezea hadi 65, lakini bado wanaona hiyo haitoshi.

Kuongezewa muda hadi 70 wengi watakufa kabla ya kufikia umri huo. Na hii itakuwa na madhara kwa familia zao, na hasa kuhusu mafao yao
 
Mtaani kugumu wanaogopa kuja kunywa sungura?

hahaha kuna mmoja alistaafu pale UDOM hata nyumba hana akaishia kukaa hotelini huku anajenga mpunga ukakata akahamia guest za 50, 30, 20, 10, mpaka akashindwa kulipa akapewa kauchochoro alale hapo
ALIJIFIA NI KINGEREZA CHAKE
 
Mtaani kugumu wanaogopa kuja kunywa sungura?
hahaha kuna mmoja alistaafu pale UDOM hata nyumba hana akaishia kukaa hotelini huku anajenga mpunga ukakata akahamia guest za 50, 30, 20, 10,,,, mpaka akashindwa kulipa akapewa kauchochoro alale hapo
ALIJIFIA NI KINGEREZA CHAKE
Hao wa aina hiyo ndiyo wako wengi na ndiyo wanaoshinikiza waongezewe muda.
 
Njaa tu, wahadhiri wachache wanashindwa kujipanga kimaisha hivyo wanaishia kufukuzia part time baada ya kustaaf.
Kwa hiyo serikali iwaongeze muda wa kustaafu ili kuwanusuru? Kama ni haki kwa nini iwe kwa wahadhiri tu?
 
Back
Top Bottom