Kati ya Watanzania Milioni 64, Maprofesa ni 226 tu. Baba wa Taifa ndiyo wa kubeba hii aibu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,107
49,808
Tukiambiwa Tanzania ni Nchi ya wajinga hatutakiwi kubisha.

Yaani Taifa lenye watu takribani Milioni 65 linakuwa na Maprofesa 226 huku Full Professors Wakiwa 63 na Associate Professors Wakiwa 163 tuu,na hizi ni takwimu za 2023.

Tukilinganisha na Wenzetu Kenya wao wana maprofesa 1,619 Kwa takwimu za 2019.Kati Yao Full Professors Wakiwa 710 na Associate Professors Wakiwa 979.

Screenshot_20230905-145728.jpg
prof2.JPG
Kiufupi Tanzania ni ya Mwisho level Moja na Burundi Kwa kuwa na jamii yenye Elimu Duni(Mbumbumbu) Kwa Kanda ya hapa Africa Mashariki..

Anaetakiwa kubeba aibu hii kwa sehemu kubwa ni Hayati Mwalimu Nyerere maana huyo bwana yeye hakutaka kabisa ku priotise Elimu Kwa sababu anazozijua yeye na in short ni sababu za Kisiasa kuogopa challenges kutoka Kwa Wasomi ndio sababu aliwatia kizuizini na wengine wakakimbilia uhamishoni.

Hakuna shule Mpya alijenga ukiacha za wakoloni Wala kuhangaika kuwaendeleza watu kielimu.Kitu pekee alichofanya ni kuwapa watu Elimu ya UPE waweze kusoma na kuandika Kwa level ya basic education tuu.

Wanyime watu Elimu Ili uweze kuwatawala.Hii tabia imekuwa inafanywa sana na Viongozi wa lile Dhehebu.Bila JK na Sasa Samia kupanuka Elimu ,Tanzania itaendelea kuwa na watu wajinga ambao wanalishwa propaganda na Watawala.

Mathalani JK ndio alianzisha na kukuza sana shule za Sekondari Kila kata,akaalika private sector kuwekeza kwenye Elimu na awamu yake ndio kulianzoshwa vyuo vikuu vingi sana.

Baada ya hapo Rais Samia nae Kwa Sasa anajenga maelfu ya miundombinu ya Elimu,amewaondoa Watoto wa kike kunyimwa Elimu Kwa visingizio vya mimba na anajenga Veta Kila Wilaya na vyuo vikuu Kwa Kila Mkoa ambao hauna Chuo Kikuu walau tuweze kushindana na Dunia badala ya kuogopa Wageni.

My Take
Dunia ya Sasa bila Elimu na maarifa ni kunidanganya,tupeleke Watoto kupata Elimu badala ya kuogopa Wageni Kwa visingizio visivyo na msingi.
---

Mbunge ataka juhudi za kuongeza maprofesa​

Dodoma. Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Dk Oscar Ishengoma amehoji idadi ya maprofesa wanaozalishwa nchini na wale wanaostaafu, huku Serikali ikisema hadi kufikia mwaka 2022, Tanzania ilikuwa na maprofesa 226.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga, amesema:Profesa ni ngazi ya kitaaluma, ambayo mhadhiri au mtumishi wa taasisi za elimu ya juu huifikia baada ya matokeo ya kazi za kitaaluma ikiwemo kufanya machapisho na ufundishaji,” amesema na kuongeza;

“Hivyo kupanda cheo kwa mwanataaluma kunatokana na jitihada za mhusika katika ufundishaji, kufanya tafiti na kuchapisha maandiko yake katika majarida yanayokubalika kitaifa na kimataifa.”

Kipanga amesema kuongezeka kwa idadi yao kunategemea zaidi jitihadi za mtu binafsi katika utekelezaji wa majukumu yake na kukubalika kwa jitihada hizo kwa wanataaluma wenziwe kwa kuzingatia miongozo waliyojiwekea.

Amesema hadi kufikia mwaka 2022 tulikuwa na jumla ya maprofesa 226, kati yao 163 wakiwa ni maprofesa washiriki (Associate Professors) na 63 ni maprofesa kamili (Full Professors).

Amesema suala la kustaafu linahusu zaidi vyuo vikuu vya umma ambapo umri wa kustaafu ni miaka 65.

Amesema kwa takwimu za mwaka 2022 idadi ya maprofesa kamili waliostaafu ni wanne na wanaotarajia kustaafu kwa mwaka 2023 ni watano, mwaka 2024 ni wawili na mwaka 2025 ni sita.

Kipanga amesema maprofesa washiriki waliostaafu kwa mwaka 2022 ni mmoja na wanaotarajiwa kustaafu kwa mwaka 2023 ni 18, mwaka 2024 ni wanne na mwaka 2025 ni sita.

Katika swali la nyongeza Ishengoma ametaka umri wakustaafu kwa maprofesa kuongezeka kutoka miaka 65 hadi 70, huku pia akihoji kama kuna mpango wa kuongeza maslahi kwa maprofesa ili kuvutia vijana wengi kusoma kufikia ngazi hiyo ambako kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wanahitajika 161 lakini wapo tisa tu.

Akijibu swali hilo nyongeza, Kipanga amesema kuwa suala la kuongeza umri limechukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi na suala la maslahi wamekuwa wakiendelea kuongeza.

Mwananchi
 
Hao Plof wanatusaidia nini? Umewahi kufanya uchunguzi watu wanao jikomboa kiuchumi ni watu gani? Umewahi kuangalia sehemu yoyote inayoongozwa na hao Plof kuna nini cha ziada? Hii elimu iliyo jaa misingi ya kigeni haitusaidii ndugu, tena hao Plof walitakiwa hata wasiwepo
 
Maprofesa wenyewe wa michongo

Wanaacha areas zao za specialization katika field zao wanaenda kuwa Machawa wa Wanasiasa

Sasa kama Mtu aliyekuwa Professor Mbobezi wa Sheria na Lecturer wa chuo kikuu (UDSM) anaingizwa katika siasa na kumshukuru Mwanasiasa kwa kusema

" Mimi uliyenitoa jalalani sijui nikulipe nini"

Mtazame Hon. Ndalichako hivi sasa

Aibu tupu
 
Hao Plof wanatusaidia nini? Umewahi kufanya uchunguzi watu wanao jikomboa kiuchumi ni watu gani? Umewahi kuangalia sehemu yoyote inayoongozwa na hao Plof kuna nini cha ziada? Hii elimu iliyo jaa misingi ya kigeni haitusaidii ndugu, tena hao Plof walitakiwa hata wasiwepo
Na hii comment ni kigezo kingine kwamba Tz tuna wajinga wengi sana.
 
Hao Plof wanatusaidia nini? Umewahi kufanya uchunguzi watu wanao jikomboa kiuchumi ni watu gani? Umewahi kuangalia sehemu yoyote inayoongozwa na hao Plof kuna nini cha ziada? Hii elimu iliyo jaa misingi ya kigeni haitusaidii ndugu, tena hao Plof walitakiwa hata wasiwepo
Haya ndioadhala ya Taifa kuwa na watu wajinga wengi Sasa,eti hizi ndio hoja 🤣🤣
 
Wewe kwanini sio Professor? Baba wa taifa ndo kakutaza kuwa prof?

Mimi sio Prof kwa uamuzi wangu binafsi baba wa taifa has nothing do to with it wala baba yangu mzazi.

Kuendelea kumpa lawama JKN mtu aliyeondika madarakani karibu miaka 40 iliyopita ni kutafuta cheap excuses na kuonyesha uvivu wa kufikiri. Mlitaka JKN asolve matatizo yenu ya miaka yote nyie mfanye nini sasa? Ni sawa na mtu kumlaumu babu yake for his shorcomings huku baba yake hajafanya kitu na yeye kawa mtu mzima hafanyi kitu kujikomboa.
 
Back
Top Bottom