Uchaguzi 2020 Wagombea Ubunge wa CHADEMA walioenguliwa wapo zaidi ya wiki moja Dodoma Ofisi za Tume ya Uchaguzi

Nimeanza kufuatilia uchaguzi kwa kupiga kura 1990. Sijawahi ona upuuzi kama huu. Niliwahi fanya kazi na REDET na TEMCO,sijawahi shuhudia ushenzi kama huu.

Weka ushahidi wa haya kufanyika awamu zilizopita. Irregularities hazikosekani lakini ni kwa kiwango gani!?
 
Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa elimu kwa wagombea wao kwa wakati. Mtu anajaza jina lake kwenye sehemu ya tarehe ya kuzaliwa, unategemea msimamizi wa uchaguzi atafanya nini. Kama ni job interview, unategemea utaitwa tena?
Ebu acha ujinga. Fitna za kijinga zinafanyika afu unasema ni anomalies za kipuuzi hizo ?
 

Kwanza uchaguzi wa 1990 ulikuwa wa chama kimoja, mfumo wa uchaguzi ulikuwa tofauti na unaotumika kwenye vyama vingi.

Hata miaka hiyo ya nyuma watu walikuwa wanatengukia na kuwekewa pingamizi pia. Tofauti ya ya miaka ya karibuni, walio teuliwa na vyama vyao lakini hawakuteuliwa na tume, asilimia kubwa ni wageni kwenye siasa na hawakupewa msaada wowote na vyama vyao kuwaonyeshwa nini cha kufanya ili wawe na sifa ya kuteuliwa na tume.

Lissu na uzoefu wake ameshidwa kuhakiki wadhamini mpaka akapeleka fomu kama ilivyo kwenye tume ndio tume ya ianze kukimbizana kuhakiki wadhami. Kama unasema hujaona uchafu kama huu, anza na Lissu kwanza.
 
Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa elimu kwa wagombea wao kwa wakati. Mtu anajaza jina lake kwenye sehemu ya tarehe ya kuzaliwa, unategemea msimamizi wa uchaguzi atafanya nini. Kama ni job interview, unategemea utaitwa tena?
Kwa hiyo akikosea kujaza ndio kafeli au
 
Kwa hiyo akikosea kujaza ndio kafeli au
Hakuna kurekebisha au kurekebishiwa, maana ikirekebishawa vyama vingine vitaweka pingamizi na utaenguliwa. Ni sawa mwalimu akujazie mtiani wa la saba au kidato cha nne, na wenzako walalamike.
 
Msiwafanye watu wapumbavu, kuna siku yatakwisha haya!
 
27 Aug 2020
WAGOMBEA 20 WA UPINZANI WAFYEKWA || MSIMAMIZI UCHAGUZI JIMBO LA SERENGETI AFAFANUA


Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Serengeti Juma Hamsini, amesema kukatwa kwa wagombea 20 wa Udiwani kutoka vyama vya Chadema, ACT Wazalendo na CUF kunatokana na kushindwa kufuata taratibu za tume. Amesema wagombea walioteuliwa ni CCM (30)Chadema(16) ACT Wazalendo(2) na CUF (2) huku mgombea wa Nccr -Mageuzi hakurudisha fomu.
 
5 September 2020

MGOMBEA UBUNGE AFUNGUKA KUKATIWA RUFAA, TUNAKWENDA TUME.


Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya Vijijini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Joseph Mwasote maarufu kwajina la CHINA amesema anashangazwa na kitendo kilicho fanywa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya Vijijini kwa kumuengua kwa sababu zisizo za msingi.

Akizungumza mbele ya wanachama wa chama hicho walio jitokeza kumpokea Mgombea nafasi ya Urais wa chama hicho Tundu Lisu leo Mwasote amesema kesho wanaenda Dododma katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ili kuhakikisha jina lake linarudishwa.
 
5 Septemba 2020
Mbeya, Tanzania

TUNDU LISSU ATUMA UJUMBE KUHUSU WAGOMBEA KUENGULIWA

 
Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa elimu kwa wagombea wao kwa wakati. Mtu anajaza jina lake kwenye sehemu ya tarehe ya kuzaliwa, unategemea msimamizi wa uchaguzi atafanya nini. Kama ni job interview, unategemea utaitwa tena?
Hakuna kitu kama hicho hizo form zilikuwa zinachezewa
 
Kwahiyo viongozi wa sasa wa vyama vya siasa huwa wanafunga ofisi za wakurugenzi ili wasiweze kupokea form?
 
Huyu Jaji anajivunjia Sana heshima
Kuna kazi zingine za lawama sana
Huyu Judge wa hovyo sana hata uchaguzi wa Ukonga wa marudio aliuvuruga mwenyewe huyu mzee.

Mtu mwenye kipara anapofanya mambo ya hovyo namna hii huonekana kituko sana.
 
Hata sheria ya uchaguzi hakuna sehemu yoyote inaposema mgombea anyang'anywe haki yake kwa kukosea kujaza fomu.
 
Hakuna kitu kama hicho hizo form zilikuwa zinachezewa
Ikiwa unapelaka fomu yako mguu kwa mguu na unakabidhi ikiwa nje ya bahasha, kila mtu anaona, na unathibitisha kama ni wewe ndio ukiejaza fomu kwa kuweka saini. Huo mchezo imechezwa wapi? Maana nakala ya fomu ipo, kwenye rufani itatolewa. Nani atacheza huo mchezo ambapo anajuwa rungu litamuangukia yeye siku ya rufani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…