Uchaguzi 2020 Wagombea Ubunge wa CHADEMA walioenguliwa wapo zaidi ya wiki moja Dodoma Ofisi za Tume ya Uchaguzi

Iwekwe hadharani na fomu ya Magufuli iliyowekewa pingamizi tujue kwa nini yake ilitupwa na za wabunge na madiwani zilipita.
Halafu hizi sheria zingine kama utawala wa mbuzi, sifa kuu ya kumzuia MTU kugombea badala ya zile za uraia, maadili, umri nk ndio kutumika zinatumika za kijinga kama picha kubandikwa vibaya, na makosa ya herufi nk?
Lissu ndio alisema ameweka pingamizi kwasababu ni haki yake kuweka pingamizi hata kama hakuna kosa au hoja ya kuweke pingamizi. Kama sio kupoteza fedha ya umma ni nini?
 
Pitia maelezo ya Polepole wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, CCM hairuhusu mgombea wake yoyote hata awe na Phd kurudisha fomu kabla haijapitiwa na wanasheria wa chama. Na hao wanasheria wako wengi sana, sasa niambie chama gani mbali na CCM kina utaratibu huo?

CCM ILIANDAA WANASHERIA ZAIDI YA 1200... - WEKA WAZI FIKRA ZAKO | Facebook

Tangu 1995 tuna chaguzi zinazo husisha vyam vingi, hakukutokea haya tuyaonayo awamu hii. Kuna udhahifu kwenye tume. Ni ktk chaguzi za za awamu hii tumeanza kushuhudia maafisa wa tume wakifunga ofisi zao ili mgombea flani ashindwe
kuchukua/kurjesha form. .......
 
Kamati za maadili ya uchaguzi wanazo hizo taarifa, siwezi kuweka hapa mimi sio msemaji wa tume lakini fomu zilizojaa makosa ziko nyingi tu. Tena saa nyingine utafikiri kama ulikuwa mkakati wa makusudi. Lakini ndio imekula kwao tena.

View attachment 1555958
Huu ni uhuni, mwenyeketi wa tume awajibike moja kwa moja kurekebisha kasoro hizo, ili vyama vyote vilivyoweka wagombea vishiriki uchaguzi mkuu, waache uhuni kama wafanyavyo miaka yote.
 
😂😂😂😂😂 Hebu tutolee UPUUZI wako! Unadhani kwanini Mkapa hakuwa na imani na hiyo tumeccm? Unadhani ni kwanini enzi za chama kimoja kwa miaka chungu nzima hakuwahi kuenguliwa mgombea yeyote yule!?

Usidhani Watanzania wote ni WAPUMBAVU hatujui uhuni unaoendelea ambao msimamizi wake ni huyo anayejiita KICHAA.

Kamati za maadili ya uchaguzi wanazo hizo taarifa, siwezi kuweka hapa mimi sio msemaji wa tume lakini fomu zilizojaa makosa ziko nyingi tu. Tena saa nyingine utafikiri kama ulikuwa mkakati wa makusudi. Lakini ndio imekula kwao tena.

View attachment 1555958
 
UPUUZI MTUPU!

1599012638950.jpeg



Pitia maelezo ya Polepole wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, CCM hairuhusu mgombea wake yoyote hata awe na Phd kurudisha fomu kabla haijapitiwa na wanasheria wa chama. Na hao wanasheria wako wengi sana, sasa niambie chama gani mbali na CCM kina utaratibu huo?

CCM ILIANDAA WANASHERIA ZAIDI YA 1200... - WEKA WAZI FIKRA ZAKO | Facebook
 
Tangu 1995 tuna chaguzi zinazo husisha vyam vingi, hakukutokea haya tuyaonayo awamu hii. Kuna udhahifu kwenye tume. Ni ktk chaguzi za za awamu hii tumeanza kushuhudia maafisa wa tume wakifunga ofisi zao ili mgombea flani ashindwe
kuchukua/kurjesha form. .......
Tena umesema jambo la maana sana, miaka hiyo ya nyuma kulikuwa na viongozi makini wa upinzani, sio wa sasa wanaopenda kutengeneza figisu zisizo na tija kwa mwananchi.

Kiongozi unasema nitaruhusu wananchi wamwage damu kama sitashinda uchaguzi. Au unaenda kupigana na askari magereza eti tu uonekane unaonewa. Sidhani kama Marehemu Mzee Bob Makani angeweza kufanya uchafu kama huo.
 
Tume ya Uchaguzi walitakiwa kujiongeza badala ya kuteua makada wa CCM Mpya waliojificha chini ya mwamvuli wa Mkurugenzi DED wa Halmashauri / Wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi huku DED-Wakurugenzi wakiwa hawapo huru na wakitumika kisiasa na CCM Mpya.

Sasa pressure kubwa imehamia Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa huku wagombea wa Urais na ubunge wa CCM Mpya na kina Polepole na Bashiru wakijifanya hawahusiki na uchafuzi huo.
Mwaka huu TUME wakileta ungese, kuna watu watapoteza vichwa vyao.
 
Hebu tutolee UPUUZI wako! Unadhani kwanini Mkapa hakuwa na imani na hiyo tumeccm? Unadhani ni kwanini enzi za chama kimoja kwa miaka chungu nzima hakuwahi kuenguliwa mgombea yeyote yule!?

Usidhani Watanzania wote ni WAPUMBAVU hatujui uhuni unaoendelea ambao msimamizi wake ni huyo anayejiita KICHAA.
Jikite kwenye hoja, kwani upinzani tu ndio uonekane unakosea taratibu na kanuni za uchaguzi? Hili ni swali ambalo upinzani wamekuwa na muda kulitafutia ufumbuzi, (tokea uchaguzi wa serikali za mitaa) lakini wameamua kulipuuzia. Na yote hii inatokana na mambo mawili, ukwasi, na kutengeneza hoja.
 
Iwekwe hadharani na fomu ya Magufuli iliyowekewa pingamizi tujue kwa nini yake ilitupwa na za wabunge na madiwani zilipita...

Tunapaswa kufikia hatua ya Tume kuchukua kumwomba mgombea kutoa taarifa na wao kuziweka katika database (ikiwa na dropdown menu) na kisha kuprint na mgombea kusaini wa kalamu na dole gumba.

Na Tume kupokea tu barua ya utambulisho kutoka chama husika. Haina maana yoyote makosa ya kiuandishi kumnyang’anya raia haki ya kikatiba!! Tume badala ya kukuza ushindani, inaondoa ushindani!!

Bado tunatumia makaratasi kudhulumiana!! Shame on Tume!!
 
Tena umesema jambo la maana sana, miaka hiyo ya nyuma kulikuwa na viongozi makini wa upinzani, sio wa sasa wanaopenda kutengeneza figisu zisizo na tija kwa mwananchi. Kiongozi unasema nitaruhusu wananchi wamwage damu kama sitashinda uchaguzi. Au unaenda kupigana na askari magereza eti tu uonekane unaonewa. Sidhani kama Marehemu Mzee Bob Makani angeweza kufanya uchafu kama huo.
Ndugu kama hizo ndo sababu, then pia tukubali kuwa tume nayo imekosa watu makini. Kipindi cha akina Makani, ilikuwa nadra sana kwa afisa wa tume kufunga ofisi ili kuenguwa wagombea fulani.
 
RAMADHAN HASSAN -DODOMA

ZAIDI ya wagombea ubunge na udiwani 1,000 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wapo jijini hapa wakisubiria hatma yao kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutokana na kukata rufaa mara baada ya majina yao kukatwa katika nafasi walizogombea.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage, alisema Dar es Salaam jana kuwa wamepokea rufaa 557 kwenye ubunge na udiwani na zilianza kufanyiwa kazi jana katika maeneo yote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wagombea hao jana, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, Susan Kiwanga ambaye aligombea Jimbo la Mlimba, alisema wanashangaa NEC kukaa kimya wakati wamepeleka rufaa zao.
“Mimi nimesimama kwa niaba ya wanawake, wanawake wengi tuliingia katika uchaguzi ili tuwawakilishe wanawake wenzetu, lakini imekuwa kinyume.

“Huu ni moto wanautengeneza, katika majimbo yetu sisi tupo tayari kwa lolote, sipo tayari kuomba haki, nipo tayari kuipigania, sisi msitujaribu, hatupo tayari kujaribiwa.

“Niwaambie Tume hali ya kule majimboni ni tete sana ni muhimu majibu yakatoka. Mimi nashangaa hawa wakurugenzi mpaka leo wanahesabika ni wasimamizi wa uchaguzi, wanatakiwa waondolewe, wanaenda kuhatarisha amani, haki itadaiwa mpaka siku ya mwisho,” alisema Kiwanga.

Naye, aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu, alisema yeye hajakatwa, lakini yupo Dodoma kuhakikisha waliokatwa hatma yao inajulikana kutoka NEC.

“Hatuifundishi tume kufanya kazi, lakini sisi ni wadau wa uchaguzi, tunayo haki ya kutoa mawazo yetu kwa sababu wao hawakuwepo kwenye majimbo huku chini, sisi kama ni dhuluma gani ilifanyika kwa wagombea wote zaidi ya 1,000 wapo Dodoma wakifuatilia.

“Baada ya kuishiwa pumzi tupo hapa tunaitaka tume ieleze majibu ya rufaa zetu, lakini tunaitaka tume ituambie tunashangazwa na maelezo kwamba majimbo 18 wamepita bila kupingwa, hii maana yake ni nini kwa sababu majimbo haya ni kati ya 57 ambayo rufaa zipo kwao.

“Kulikuwa kuna wagombea wa vyama kadhaa sio Chadema tu, kulikuwa kuna wagombea wa CUF na vyama vingine, tunashangaa kuona majimbo wamepita bila kupingwa.

“Mimi sijaenguliwa, lakini nipo hapa kwa sababu wameengua madiwani 16 kati ya 36 hii maana yake wanataka kuleta ujanja ujanja tunasema hiki kitu hakikubaliki, wagombea wetu wamekatwa kihuni.

“Kuna sehemu ya kujaza chama cha mtu, ambaye amemalizia Demokrasia na Maendeleo ameenguliwa na aliyeandika kifupi Chadema amekatwa, huu ni uhuni mkubwa,” alisema Sugu.

Chanzo: Mtanzania
 
nafikiri nj

Nafikiri njia sahihi ni kuondoka na vichwa vya wakurugenzi 10 hivi na familia zao ndo watapata akili na kujua kuwa dhulma ni kitu kibaya. mambo ya kihanithi kweli kufanywa na watu wenye mpk PhD. Ujinga uliovuka mipaka.
"Don't loose your (ones) soul to gain the world. Wisdom is better than silver and gold"
Bob Marley
 
Back
Top Bottom