Uchaguzi 2020 Wagombea Ubunge wa CHADEMA walioenguliwa wapo zaidi ya wiki moja Dodoma Ofisi za Tume ya Uchaguzi

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
10 September 2020
Dar es Salaam Tanzania

NEC YATOA UAMUZI wa RUFAA 67 za WAGOMBEA UBUNGE na UDIWANI, YAWAREJESHA 45 KUGOMBEA.


.. Tume ya Taifa ya Uchagzui katika kikao chake cha jana tarehe 9 Septemba, 2020 imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi jumla ya rufaa 67.

Kati ya hizo, rufaa 22 ni za Wagombea Ubunge na 45 ni za Wagombea Udiwani.

Maamuzi ya rufaa za wagombea Ubunge ni kama ifuatavyo:-
i. Imekubali rufaa 19 na kuwarejesha wagombea husika katika orodha ya wagombea.
 1. Rufaa hizo ni kutoka kwenye Majimbo ya Tunduru Kaskazini,
 2. Mbeya Vijijini,
 3. Songea Mjini,
 4. Karagwe,
 5. Ulanga,
 6. Chemba,
 7. Tanga,
 8. Kibamba,
 9. Nyasa,
 10. Same Mashariki,
 11. Buhigwe,
 12. Mufindi Kusini,
 13. Muheza,
 14. Tabora Kaskazini,
 15. Ubungo (2)
 16. na Kigamboni (3).
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
14 September 2020

CHADEMA YAITAKA TUME KUACHA KUCHEZEA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI


Katibu Mkuu wa CHADEMA John John Mnyika ataka vikao vya Tume kufanyia kazi rufani maana zipo nyingi za wabunge na madiwani lakini utendaji kazi wa kusikiliza rufani upo polepole sana na haki ikichelewa ni sawa na kupunguza haki za wagombea ikiwa rufani zao zitapitishwa waendelee kugombea.
Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya Vijijini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Joseph Mwasote maarufu kwa jina la CHINA wa CHINA.
 

Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
5,120
2,000
Huyu huyu Slowslow mzee kijana wa magazijuto
Pitia maelezo ya Polepole wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, CCM hairuhusu mgombea wake yoyote hata awe na Phd kurudisha fomu kabla haijapitiwa na wanasheria wa chama. Na hao wanasheria wako wengi sana, sasa niambie chama gani mbali na CCM kina utaratibu huo?

CCM ILIANDAA WANASHERIA ZAIDI YA 1200... - WEKA WAZI FIKRA ZAKO | Facebook
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
15 September 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Tume ya Uchaguzi yazungumzia Mbinyo toka Vyama vya Siasa kuhusu kupitia Rufani

Mkurugenzi wa Tume Dr. Wilson Charles asema wanachapa kazi sana kupitia rufani za wagombea , hata sasa unaweza kuja hapa jengo la Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, tuko kwenye kikao tunaendelea kupitia hizo rufaa•

"Waache kutusumbua, sasa wao wanapiga kelele tungetoa hizo rufaa haraka hata hao wabunge wao wasingerudi, waache uzandiki, upuuzi na uongo"

Mkurugenzi aliyasema hayo alipoongea na wenye vyombo vya habari mitandaoni.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
15 September 2020
Mbalizi, Mbeya
Tanzania

"NILITEULIWA,NIKAENGULIWA,NIKAKAMATWA" MGOMBEA UDIWANI CHADEMA KATA YA NSALALA BAADA KURUDI ULINGONI
Wananchi wakesha na kushangilia kusikia diwani wao mtarajiwa kurejeshwa ulingoni katika kampeni za 2020.
 

Pawa chilonda

JF-Expert Member
Aug 13, 2017
326
500
15 September 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Tume ya Uchaguzi yazungumzia Mbinyo toka Vyama vya Siasa kuhusu kupitia Rufani

Mkurugenzi wa Tume Dr. Wilson Charles asema wanachapa kazi sana kupitia rufani za wagombea , hata sasa unaweza kuja hapa jengo la Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, tuko kwenye kikao tunaendelea kupitia hizo rufaa•

"Waache kutusumbua, sasa wao wanapiga kelele tungetoa hizo rufaa haraka hata hao wabunge wao wasingerudi, waache uzandiki, upuuzi na uongo"

Mkurugenzi aliyasema hayo alipoongea na wenye vyombo vya habari mitandaoni.
Kwa spidi yao matokeo ya UCHAGUZI yatatolewa January huyo mkurugenzi wa NEC HATOSHI BORA KIHAMIA ANGEACHWA AU KAILIMA
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
15 September 2020
Mbeya, Tanzania

CHADEMA MKOA WA MBEYA WAFUNGUKA BAADA YA MAJIBU YA RUFAA ZA WABUNGE WAKE.

Joseph Mwasote almaaruf CHINA wa CHINA ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya atangaza kuwa Wagombea wa ubunge wa CHADEMA majimbo ya Mbarali, Mbeya Vijijini na Chunya warudishwa na Tume ya Uchaguzi kushiriki katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Joseph Mwasote asema wanasheria wa Tume ya Uchaguzi makao makuu kwa usiri wamelaani mambo yaliyofanyika na Wasimamizi wa Uchaguzi ktk majimbo.

Kuna mgongano mkubwa baina ya watendaji wa Tume ya Uchaguzi makao makuu na Wasimamizi Makada Wakurugenzi majimboni kwa watendaji majimbo kuendelea kuwazungusha madiwani kupata barua za ushindi wa rufaa zao.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
13 September 2020
Vwawa, Mbeya
Tanzania

Mgombea ashinda rufaa Tume kushiriki uchaguzi 2020

Mgombea wa CHADEMA aliyeshinda rufani Fanuel Mkisi apokekewa kwa shangwe na wananchi watakaopiga kura 2020


Fanuel Elias MKISI. Chama: CHADEMA. Mgombea ubunge tiketi ya chama cha CHADEMA, jimbo la VWAWA , Mbeya kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania 2020.
 

santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
2,172
2,000
Pitia maelezo ya Polepole wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, CCM hairuhusu mgombea wake yoyote hata awe na Phd kurudisha fomu kabla haijapitiwa na wanasheria wa chama. Na hao wanasheria wako wengi sana, sasa niambie chama gani mbali na CCM kina utaratibu huo?

CCM ILIANDAA WANASHERIA ZAIDI YA 1200... - WEKA WAZI FIKRA ZAKO | Facebook
Sema walisahau kupitia form ya Baba, kuna picha isiyo rasimi iliambatanishwa!! Nafikiri ilikua tu bahati mbaya🤩
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
15 September 2020

Wagombea wa Upinzani hawapewi mrejesho wala ushirikiano na 'uwazi' toka TUME NEC

Lumola Steven Kahumbi, Mgombea wa Ubunge jimbo la Bukene , Tabora kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)


amejitokleza hadharani baada ya kukosa majibu ya rufaa mara baada ya tume ya uchaguzi NEC kutangaza kuwa mgombea wa CCM amepita bila kupingwa. Ametoa ushauri kwa tume hiyo kuhusu mambo mbalimbali ya siasa yanayoendelea.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
16 September 2020
Mbeya Vijijini
TUNDU LISSU ATOA WITO KWA TUME YA UCHAGUZI , AJIBU TISHIO LA TUME
Aikumbusha Tume ya Uchaguzi maadili yake
 • Tume NEC imekatazwa upendeleo
 • Mambo yasiyotakiwa kufanywa na watendaji wa serikali wakati wa kampeni mfano kutumia magari na posho za serikali kukibeba chama tawala
 • Kutoa ahadi za shughuli za maendeleo wakati wa kampeni mfano kuipigia simu live TANROADS kujenga barabara wakati wa kampeni
 • N.k
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,834
2,000
15 September 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Tume ya Uchaguzi yazungumzia Mbinyo toka Vyama vya Siasa kuhusu kupitia Rufani

Mkurugenzi wa Tume Dr. Wilson Charles asema wanachapa kazi sana kupitia rufani za wagombea , hata sasa unaweza kuja hapa jengo la Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, tuko kwenye kikao tunaendelea kupitia hizo rufaa•

"Waache kutusumbua, sasa wao wanapiga kelele tungetoa hizo rufaa haraka hata hao wabunge wao wasingerudi, waache uzandiki, upuuzi na uongo"

Mkurugenzi aliyasema hayo alipoongea na wenye vyombo vya habari mitandaoni.

..Tume iko too slow.

..Tume inatakiwa ifanye kazi kwa haraka na kwa usahihi.

..Kuna rufaa zimeishaamuliwa lakini wagombea hawajapewa barua za maamuzi.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
16 September 2020
Tunduma, Songwe
Tanzania

CHADEMA yaitaka NEC kutenda haiki kwa vyama vyote

 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
22 September 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Suzana Kiwanga : Napambana na kipenzi cha John Magufuli
Suzan Kiwanga mgombea wa ubunge jimbo la Mlimba kupitia CHADEMA aliyeenguliwa na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Mlimba Morogoro, afunguka sakata zima
 • Risiti ya Halmashauri yagushiwa
 • Kuenguliwa kuwa fomu namba 8 haina risiti
 • Uteuzi ulifanyika saa moja usiku
 • Fomu namba 12 ya rufani, mkurugenzi alikimbia na kufunga ofisi tarehe 25 agosti na 26 agosti
 • Wiki 3 nimepiga kambi ofisi ya Tume Dodoma
 • Mlimba hali tete na Polisi walimtonya kuwa kuna njama ya kumkamata kutoka na hali kwa kigezo Suzan Kiwanga anasababisha vurugu
 • Mpaka leo Tume ya Uchaguzi bado inaendelea na mchakato wa kupitia rufani yake
 • Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin E. Kunambi alishiriki ktk mchakato wa ubunge akiwa bado mtumishi ngazi ya Mkurugezi wa Mji kinyume na taratibu na maadili ya wagombea kama inavyosema sheria ya uchaguzi ya Taifa na maelekezo ya Tume ya Uchaguzi
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
22 Sep 2020

ACT yafafanuwa tume za uchaguzi kujipotosha


Watumishi wa umma waenguliwa kugombea uwakilishi na ubunge kupitia ACT-WAZALENDO n.k kwa pingamizi .

Mwanasheria Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Omar Said Shaaban, ameanika hadharani jinsi Tume za Uchaguzi (ZEC na NEC) zilivyofikia maamuzi ya kuwaondowa wagombea wa chama chake kwenye nafasi za uwakilishi na ubunge bila kuzingatia kabisa hoja za kisheria wala kimantiki.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
06 October 2020
Mufindi, Tanzania

Wagombea wa CHADEMA wafika ofisi ya Mkurugenzi
Wagombea waruhusiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuatia rufaa zao lakini kuna urasimu kupewa barua waendelee na kampeni Mafinga Kaskazini na Mafinga Kusini. Tangazo la serikali la 3 Oktoba 2020 lilisema wagombea wa CHADEMA wameruhusiwa na Tume kuendelea na kampeni.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,554
2,000
06 October 2020
Mafinga mjini,
Iringa
Tanzania

WAGOMBEA UDIWANI MAFINGA WAVUTANA NA MKURUGENZI WA UCHAGUZI/WAIBUA MAZITO

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Uchaguzi jimbo la Mufindi akaidi hatua za TUME makao makuu Dodoma kurudisha majina ya wagombea wa CHADEMA kuruhusiwa kuendelea kugombea .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom