Uchaguzi 2020 Wagombea Ubunge wa CHADEMA walioenguliwa wapo zaidi ya wiki moja Dodoma Ofisi za Tume ya Uchaguzi

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,046
23,835
1 September 2020
Dodoma, Tanzania

Bila Uwoga SUGU ailipua TUME ya UCHAGUZI, Amtaja Katibu wa CCM, - "Amani ya nchi Ipo mikinoni Mwao"



Wabunge Wa CHADEMA Walioenguliwa na Wasimamizi wa Uchaguzi Katika Majimbo Mbalimbali Wamekutana Na Waandishi Wa habari jijini Dodoma Kuiomba Tume Ya Uchaguzi Kutoa Majibu Ya Rufaa Walizokata... kwa ujumla kuna wabunge na madiwani jumla yao zaidi ya 1, 000 wapo Dodoma wakifuatilia rufani walizokata Tume ya Uchaguzi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Joseph Mbilinyi abainisha Mbeya mjini madiwani 16 wameenguliwa, aiasa Tume ya Uchaguzi Taifa kuwa wana dhamana kubwa kuhakikisha rufani za wagombea ubunge walioenguliwa na Wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo mbalimbali zinatendewa haki kwa haraka ili wakaendelee na kampeni za kunadi sera na kuomba kuchaguliwa na wananchi.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CHADEMA anasema Hali ya kisiasa ni mbaya sana inatishia amani kutokana na Ma-DC na DED kuvuruga mchakato wa uchaguzi na ndiyo maana wapo Dodoma kuipatia Tume ya Uchaguzi ukweli wa kilichofanyika ktk kuenguliwa kihuni na Wasimamizi wa Uchaguzi walioteuliwa na Tume ya Uchaguzi kusimamia zoezi hilo muhimu ktk majimbo mbalimbali nchini.


2 September 2020

Mwanasheria wa ACT Wazalendo atowa kauli kuenguliwa wagombea

 
Tume ya Uchaguzi walitakiwa kujiongeza badala ya kuteua makada wa CCM Mpya waliojificha chini ya mwamvuli wa Mkurugenzi DED wa Halmashauri / Wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi huku DED-Wakurugenzi wakiwa hawapo huru na wakitumika kisiasa na CCM Mpya.

Sasa pressure kubwa imehamia Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa huku wagombea wa Urais na ubunge wa CCM Mpya na kina Polepole na Bashiru wakijifanya hawahusiki na uchafuzi huo.
Tunayo majina yote ya wahusika
 
bagamoyo,
Kwa ujumla ni kwamba wamekaangwa wakakaangika, pressure ikizidi kwao wanapiga simu kwa bwana mkubwa kumueleza, Bwana mkubwa anawajibu “shughulikieni mnavyoweza ninyi, mimi niko busy kutafuta kura”.

Lawama watabeba wao na majina yao yatabaki katika historia ya Tanzania yakiwa yameandikwa kwa wino mwekundu. What a pity! Unafanya dhuluma kubwa kwa nchi yako kwa mshahara wa 4M! Umasikini mbaya sana.
 
Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa elimu kwa wagombea wao kwa wakati. Mtu anajaza jina lake kwenye sehemu ya tarehe ya kuzaliwa, unategemea msimamizi wa uchaguzi atafanya nini. Kama ni job interview, unategemea utaitwa tena?
 
Unatetea dhulma ili iweje? Mbunge gani au Diwani gani alifanya hivyo?
Kamati za maadili ya uchaguzi wanazo hizo taarifa, siwezi kuweka hapa mimi sio msemaji wa tume lakini fomu zilizojaa makosa ziko nyingi tu. Tena saa nyingine utafikiri kama ulikuwa mkakati wa makusudi. Lakini ndio imekula kwao tena.

IMG_20200902_012227.jpg
 
wapuzi sana ccm wanajitapa kuwa wanakuballika ila wanataka ubunge na udiwani wa viti maalum. waende kwa wananch wawaeleze miaka mitano ya hapa kazi tu wamefanya nini ili wananchi waamuwe kuwaongeza mitano mingine au la.

Vingenevyo kama tume itakubali kuitumbukiiza nchi kwenye machafuko kwa kujaribu kubeba wezi wa haki za wananchi za kuchaguwa viongozi wanao wataka basi wananchi wana haki ya kushughulikia hao wasimamizi na wabunge na madiwani wa kuteuliwa na tume kama wezi .

Maana kupita bila kupingwa ni wizi kama wizi wowote na mwizi huwa anashughulikiwa na wenye mali kabla ya polisi kuja. haiwezekani ujiite mbunge au diwani wangu akati sijakupigia kura. Kama sijakuchaguwa halafu unajiita mbunge na diwani wewe ni tapeli kama matapeli wengine.

Mbunge au diwani ni mtu aliye tumwa na wapiga kula kuwawakilisha kwenye serikali kuu sasa lama hujapigiwa kula na wananchi hawajakutuma halafu unapoke a mshahara wa kibunge maana yake unawaibia wananchi na taifa kwa ujumla .
 
Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa elimu kwa wagombea wao kwa wakati. Mtu anajaza jina lake kwenye sehemu ya tarehe ya kuzaliwa, unategemea msimamizi wa uchaguzi atafanya nini. Kama ni job interview, unategemea utaitwa tena?
Acha kuamini vitu ambavyo vilishapangwa. Siku utakapoona formu yako mahali flani imejazwa tofauti na ulivyojaza wewe mwenyewe tena kwa lugha yako pendwa ya kiswahili ndipo utakapojua michezo michafu ipo.

Watanzania tunafanywa wajinga nasi tunakubali kwa upole wetu na kufumbiana macho, ila kama tungekuwa na hulka ya kuambiana ukweli bila kiangalia maslahi yetu binafsi, hili taifa lingekuwa limepiga hatua kubwa sana kimaendeleo na kiuwajibikaji.
 
Acha kuamini vitu ambavyo vilishapangwa. Siku utakapoona formu yako mahali flani imejazwa tofauti na ulivyojaza wewe mwenyewe tena kwa lugha yako pendwa ya kiswahili ndipo utakapojua michezo michafu ipo...
Hahahaha, watanzania mnafanywa wajinga na akina nani hao? Kwann mkubali kufanywa wajinga? Chukueni Hatua ,mmebaki nyie tu na Ccm yenu hy
 
Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa elimu kwa wagombea wao kwa wakati. Mtu anajaza jina lake kwenye sehemu ya tarehe ya kuzaliwa, unategemea msimamizi wa uchaguzi atafanya nini. Kama ni job interview, unategemea utaitwa tena?
Tatizo ni kubwa kuliko unavyo dai, haiwezekani makosa yawe ya upande mmoja. Kuanzia Pemba, Misenyi hadi Mbambabay....... kuna dalili za hujuma.
 
Kamati za maadili ya uchaguzi wanazo hizo taarifa, siwezi kuweka hapa mimi sio msemaji wa tume lakini fomu zilizojaa makosa ziko nyingi tu. Tena saa nyingine utafikiri kama ulikuwa mkakati wa makusudi. Lakini ndio imekula kwao tena.

View attachment 1555958
Iwekwe hadharani na fomu ya Magufuli iliyowekewa pingamizi tujue kwa nini yake ilitupwa na za wabunge na madiwani zilipita.

Halafu hizi sheria zingine kama utawala wa mbuzi, sifa kuu ya kumzuia MTU kugombea badala ya zile za uraia, maadili, umri nk ndio kutumika zinatumika za kijinga kama picha kubandikwa vibaya, na makosa ya herufi nk?
 
Tatizo ni kubwa kuliko unavyo dai, haiwezekani makosa yawe ya upande mmoja. Kuanzia Pemba, Misenyi hadi Mbambabay....... kuna dalili za hujuma.
Pitia maelezo ya Polepole wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, CCM hairuhusu mgombea wake yoyote hata awe na Phd kurudisha fomu kabla haijapitiwa na wanasheria wa chama. Na hao wanasheria wako wengi sana, sasa niambie chama gani mbali na CCM kina utaratibu huo?

CCM ILIANDAA WANASHERIA ZAIDI YA 1200... - WEKA WAZI FIKRA ZAKO | Facebook
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom