Uchaguzi 2020 Wagombea Ubunge wa CHADEMA walioenguliwa wapo zaidi ya wiki moja Dodoma Ofisi za Tume ya Uchaguzi

residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,325
2,000
Post yangu namba #18 kwenye uzi huu inakupa majibu ya maswali yako.

Btw, ukatwaji umekuwepo tokea uchaguzi wa kwanza 1995, sio jambi geni. Rufaa za kabla ya uchaguzi na baada ya uchanguzi nazo zimekuwepo tokea 1995. Tatizo mitandao inaongozwa na vijana ambao aidha wavivu wa kumbukumbu, au hawakuwepo kwenye ulingo wa siasa za miaka ya zamani. Ndio maana wengi wanaona ni jambo la ajabu, lakini sio jambo la ajabu.
Nimeanza kufuatilia uchaguzi kwa kupiga kura 1990. Sijawahi ona upuuzi kama huu. Niliwahi fanya kazi na REDET na TEMCO,sijawahi shuhudia ushenzi kama huu.

Weka ushahidi wa haya kufanyika awamu zilizopita. Irregularities hazikosekani lakini ni kwa kiwango gani!?
 

Mzee Wa Republican

JF-Expert Member
Jul 20, 2013
1,276
2,000
Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa elimu kwa wagombea wao kwa wakati. Mtu anajaza jina lake kwenye sehemu ya tarehe ya kuzaliwa, unategemea msimamizi wa uchaguzi atafanya nini. Kama ni job interview, unategemea utaitwa tena?
Ebu acha ujinga. Fitna za kijinga zinafanyika afu unasema ni anomalies za kipuuzi hizo ?
 

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
6,007
2,000
Nimeanza kufuatilia uchaguzi kwa kupiga kura 1990. Sijawahi ona upuuzi kama huu. Niliwahi fanya kazi na REDET na TEMCO,sijawahi shuhudia ushenzi kama huu.
Weka ushahidi wa haya kufanyika awamu zilizopita. Irregularities hazikosekani lakini ni kwa kiwango gani!?

Kwanza uchaguzi wa 1990 ulikuwa wa chama kimoja, mfumo wa uchaguzi ulikuwa tofauti na unaotumika kwenye vyama vingi.

Hata miaka hiyo ya nyuma watu walikuwa wanatengukia na kuwekewa pingamizi pia. Tofauti ya ya miaka ya karibuni, walio teuliwa na vyama vyao lakini hawakuteuliwa na tume, asilimia kubwa ni wageni kwenye siasa na hawakupewa msaada wowote na vyama vyao kuwaonyeshwa nini cha kufanya ili wawe na sifa ya kuteuliwa na tume.

Lissu na uzoefu wake ameshidwa kuhakiki wadhamini mpaka akapeleka fomu kama ilivyo kwenye tume ndio tume ya ianze kukimbizana kuhakiki wadhami. Kama unasema hujaona uchafu kama huu, anza na Lissu kwanza.
 

Mkubwa ndevu

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,037
1,500
Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa elimu kwa wagombea wao kwa wakati. Mtu anajaza jina lake kwenye sehemu ya tarehe ya kuzaliwa, unategemea msimamizi wa uchaguzi atafanya nini. Kama ni job interview, unategemea utaitwa tena?
Kwa hiyo akikosea kujaza ndio kafeli au
 

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
6,007
2,000
Kwa hiyo akikosea kujaza ndio kafeli au
Hakuna kurekebisha au kurekebishiwa, maana ikirekebishawa vyama vingine vitaweka pingamizi na utaenguliwa. Ni sawa mwalimu akujazie mtiani wa la saba au kidato cha nne, na wenzako walalamike.
 

wagagagigi

JF-Expert Member
Dec 9, 2014
883
1,000
Huu ni utaratibu wa ndani ya CCM na sio vyama vingine, vyama vingine wao wanajiamini kama watu wateule wao wanauwezo wa kujaza fomu. Matokeo yake wale walipitisha fomu kwa mwanasheria, fomu zao hazina kosa hata moja, na wale ambao hawakupitisha kwa mwanasheria, wao wana 50% ya makosa. Je ukiwa mwenyekiti wa chama chako itatafuta mchawi wapi, tume au uliowateuwa wako?

Mtu anaambiwa banduka picha mbele kwenye fomu hii, haweki. Jaza tarehe ya kuzaliwa, anaweka tarehe ya kupeleka fomu. Unategemea nini kitatokea?
Msiwafanye watu wapumbavu, kuna siku yatakwisha haya!
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,590
2,000
27 Aug 2020
WAGOMBEA 20 WA UPINZANI WAFYEKWA || MSIMAMIZI UCHAGUZI JIMBO LA SERENGETI AFAFANUA


Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Serengeti Juma Hamsini, amesema kukatwa kwa wagombea 20 wa Udiwani kutoka vyama vya Chadema, ACT Wazalendo na CUF kunatokana na kushindwa kufuata taratibu za tume. Amesema wagombea walioteuliwa ni CCM (30)Chadema(16) ACT Wazalendo(2) na CUF (2) huku mgombea wa Nccr -Mageuzi hakurudisha fomu.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,590
2,000
5 September 2020

MGOMBEA UBUNGE AFUNGUKA KUKATIWA RUFAA, TUNAKWENDA TUME.


Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya Vijijini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Joseph Mwasote maarufu kwajina la CHINA amesema anashangazwa na kitendo kilicho fanywa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya Vijijini kwa kumuengua kwa sababu zisizo za msingi.

Akizungumza mbele ya wanachama wa chama hicho walio jitokeza kumpokea Mgombea nafasi ya Urais wa chama hicho Tundu Lisu leo Mwasote amesema kesho wanaenda Dododma katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ili kuhakikisha jina lake linarudishwa.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,590
2,000
5 Septemba 2020
Mbeya, Tanzania

TUNDU LISSU ATUMA UJUMBE KUHUSU WAGOMBEA KUENGULIWA

 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
16,725
2,000
Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa elimu kwa wagombea wao kwa wakati. Mtu anajaza jina lake kwenye sehemu ya tarehe ya kuzaliwa, unategemea msimamizi wa uchaguzi atafanya nini. Kama ni job interview, unategemea utaitwa tena?
Hakuna kitu kama hicho hizo form zilikuwa zinachezewa
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
16,725
2,000
Tena umesema jambo la maana sana, miaka hiyo ya nyuma kulikuwa na viongozi makini wa upinzani, sio wa sasa wanaopenda kutengeneza figisu zisizo na tija kwa mwananchi. Kiongozi unasema nitaruhusu wananchi wamwage damu kama sitashinda uchaguzi. Au unaenda kupigana na askari magereza eti tu uonekane unaonewa. Sidhani kama Marehemu Mzee Bob Makani angeweza kufanya uchafu kama huo.
Kwahiyo viongozi wa sasa wa vyama vya siasa huwa wanafunga ofisi za wakurugenzi ili wasiweze kupokea form?
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
16,725
2,000
Huyu Jaji anajivunjia Sana heshima
Kuna kazi zingine za lawama sana
Huyu Judge wa hovyo sana hata uchaguzi wa Ukonga wa marudio aliuvuruga mwenyewe huyu mzee.

Mtu mwenye kipara anapofanya mambo ya hovyo namna hii huonekana kituko sana.
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
16,725
2,000
Tunapaswa kufikia hatua ya Tume kuchukua kumwomba mgombea kutoa taarifa na wao kuziweka katika database (ikiwa na dropdown menu) na kisha kuprint na mgombea kusaini wa kalamu na dole gumba. Na Tume kupokea tu barua ya utambulisho kutoka chama husika. Haina maana yoyote makosa ya kiuandishi kumnyang’anya raia haki ya kikatiba!! Tume badala ya kukuza ushindani, inaondoa ushindani!!

Bado tunatumia makaratasi kudhulumiana!! Shame on Tume!!
Hata sheria ya uchaguzi hakuna sehemu yoyote inaposema mgombea anyang'anywe haki yake kwa kukosea kujaza fomu.
 

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
6,007
2,000
Hakuna kitu kama hicho hizo form zilikuwa zinachezewa
Ikiwa unapelaka fomu yako mguu kwa mguu na unakabidhi ikiwa nje ya bahasha, kila mtu anaona, na unathibitisha kama ni wewe ndio ukiejaza fomu kwa kuweka saini. Huo mchezo imechezwa wapi? Maana nakala ya fomu ipo, kwenye rufani itatolewa. Nani atacheza huo mchezo ambapo anajuwa rungu litamuangukia yeye siku ya rufani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom