Wafungwa wauana kwa visu

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454










JESHI la Magereza, limeingia katika kashfa nzito baada ya nyapara mkuu wa wafungwa katika Gereza la Butimba mkoani hapa kuuawa kwa kuchomwa visu na wafungwa wenzake juzi mchana.

Nyampara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Kishiwa, aliuawa chumbani kwake wakati akila chakula cha mchana, baada ya wafungwa wenzake kumfuata na kufunga mlango, kisha kumkaba na kumchoma visu sita shingoni, ubavuni na kifuani.
Imedaiwa kuwa wafungwa wengine walishuhudia watuhumiwa hao wakiingia ndani mwake, kabla ya kusikia tafrani kubwa iliyowafanya wavamie chumba hicho na kukuta mkuu wao kauawa.
Watuhumiwa hao walishambuliwa vibaya kwa kipigo na wafungwa wenzao pamoja na baadhi ya askari magereza kiasi cha kulazimika kupelekwa hospitali kupata matibabu.
Habari za kina kutoka ndani ya gereza hilo zilizothibitishwa na Kamishna Mkuu wa Magereza nchini (CGP), Augustine Nanyaro na viongozi wengine waandamizi, zilisema chanzo cha mauaji hayo ni hali ya kutoelewana baina ya wafungwa wanaotumikia vifungo virefu.
Hata hivyo, kuna madai kwamba mauaji hayo yamechangiwa na uzembe wa uongozi wa gereza hilo wa kushindwa kuyafanyia kazi malalamiko ya siku nyingi ya wafungwa, yakiwemo ya ukatili, ingawa Mkuu wa Gereza, Kamishna Masidizi (ACP), Edson Yalimo, alikwepa kukwepa kutaja kiini halisi.
Baadhi ya askari magereza ambao waliomba kuhifadhiwa majina yao, walisema kwa muda mrefu wafungwa wamekuwa wakimtuhumu nyapara huyo kuwa ana uongozi wa kibabe ambao unakumbatiwa na viongozi wakuu wa gereza.
“Nyapara huyo alikuwa ni kama mkuu wa gereza, chochote ambacho alikuwa akisema ndicho kilichokuwa kikifuatwa na uongozi wa gereza,” alisema askari mwingine.
Kwamba hata kwa nyakati tofauti walipokuja viongozi wa Makao Makuu, Naibu Kamishana wa Magereza (DCP), John Minja, na Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Magereza (SACP) Mkoa wa Mwanza, RPO Raphael Mollel, wafungwa walitoa malalamiko yao kuhusu nyapara huyo, lakini waliishia kupigwa na kuandikishwa maelezo.
Habari zinasema wafungwa hao walimwambia Kamanda Minja kwamba kama hawamwondoi nyapara huyo, watafanya tukio kubwa lisilokuwa la kawaida, ikiwemo kuua askari au nyapara mwenyewe.
“Sisi askari tunajua ni mwiko kupuuzia taarifa yoyote ya kialifu, tunashangaa ni kwanini mkuu wa gereza na viongozi wengine walipuuzia taarifa hizi,” alisema askari mwingine.
Mkuu wa Magereza nchini, Nanyaro, alikiri kutokea kwa tukio hilo, lakini akasema kuwa alikuwa safarini mkoani Mbeya na hivyo ameagiza apatiwe taarifa kamili ndipo aweze kutoa taarifa.

 
Huyo nyampala yawezekana alikuwa anatumiwa na mafisadi,ndio maana walikuwa hawamfanyi chochote.
 
Hizi tabia za wafungwa kuchomana visu na kuuwana mara nyingi tunasikia kutoka Mexico City, Peru, Bolivia kwenye nchi za biashara ya madawa ya kulevya...sasa imefika mpaka Tanzania, ni uzembe wa Askari Magereza kuwatetea manyampala..
 
ndani ya serikali ya ccm mbona hayo madogo?
subiri yanakuja ya kustaajabisha na kushangaza.
 
Congratulations Ritz!!

Du!! Hii comment umeandikiwa na mtu bila shaka.....!!!! Really like it, inaonyesha improvement ya kifkra kwa mbaaaali.

Hizi tabia za wafungwa kuchomana visu na kuuwana mara nyingi tunasikia kutoka Mexico City, Peru, Bolivia kwenye nchi za biashara ya madawa ya kulevya...sasa imefika mpaka Tanzania, ni uzembe wa Askari Magereza kuwatetea manyampala..
 
Ni kweli kuna manyanyaso makubwa na upendeleo wa baadhi ya watu,ambao wanajipendekeza kwa wakuu wa magereza ,ili waonekane wao ni watiifu sana kuwabana wenzao!kuna tukio lingine limeripotiwa miezi kadhaa kuwa mkuu wa gereza alichomwa kisu bahati yake miguuni,hakufa ila alitakiwa nae auawe yaishe,wale wafingwa walipigwa hadi kufa.....hayo yapo ila askari wakubwa wameshafanya magereza mali yao kabisa maana kilio cha wanyonge hakifiki kokote.sasa fundisho kwa woote wanaokumbatia uhalifu!mkuu gereza hapo alie tu hana chake,hata huyo wa mkoa mwanza alie!weka benchi wote hao wamefanya magereza mali zao!!!
 
Hivi ule utaratibu wa kukaguliwa kwa wafungwa kila wanapotoka kufanya kazi nahis umeondolewa kama vp urudishwe
 
Hivi katika tukio hilo watuhumiwa watakamatwa na kushikiliwa kwa mahojiano au? Maana tayari wamo gerezani sasa sijui inakuwaje?

TUMBIRI (PhD, Hull University - UK),
tumbiri@jamiiforums.com

Watatolewa gerezani halafu wataambiwa wakimbie mbio. Polisi baadaye watawafukuza na kuwakamata na kuwafungulia mashtaka mapya. Ieleweke kuwa makosa yao ya mwanzo yatakuwa yamejifuta automatically.
 
Hizi tabia za wafungwa kuchomana visu na kuuwana mara nyingi tunasikia kutoka Mexico City, Peru, Bolivia kwenye nchi za biashara ya madawa ya kulevya...sasa imefika mpaka Tanzania, ni uzembe wa Askari Magereza kuwatetea manyampala..
Mkuu katika Magereza ya Tanzania Manyapara wanatumika kama sales agent wa bange,Unga,sigara na mengineyo wa maaskari magereza.So nyapara anakuwa na Nguvu,kibri kuliko ata baadhi ya Askari.
 
Hizi tabia za wafungwa kuchomana visu na kuuwana mara nyingi tunasikia kutoka Mexico City, Peru, Bolivia kwenye nchi za biashara ya madawa ya kulevya...sasa imefika mpaka Tanzania, ni uzembe wa Askari Magereza kuwatetea manyampala..

Ritz sometimes kumbe una utu na kusema ukweli unaoonekana...nafarijika sana kusoma hii comment yako..
 
Kesi mpya ya mauaji haihusiani na hizo wanazotumikia sasa hivi.

Mkuu zomba,
Naona hujanielewa. Nilikuwa nasema hivi, kwa vile utaratibu ni kwamba mtuhumiwa anakamatwa na kuwekwa mahabusu kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi kabla ya kesi kwenda mahakamani, sasa hawa wenzetu tayari wapo gerezani wanatumikia vifungo vyao. Je watatolewa gerezani wapelekwe mahabusu ili wahojiwe au inakuwaje? Na je wakipelekwa mahabusu si watakuwa wamekatishiwa vifungo vyao vya sasa? Au mahabusu yao itakuwa gerezani humo humo? Na kama watahojiwa wakiwa gerezani huoni kwamba watakuwa wamenyimwa haki yao ya msingi ya kushikiliwa na kuhojiwa wakiwa mahabusu badala ya gerezani? Na je kama tuhuma zao za sasa zinadhaminika na wakatimiza masharti ya dhamana wataruhusiwa kuwa nje ya mahabusu? Umenisoma Mkuu wangu?

TUMBIRI (PhD, Hull University - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
"Sisi askari tunajua ni mwiko kupuuzia taarifa yoyote ya kialifu, tunashangaa ni kwanini mkuu wa gereza na viongozi wengine walipuuzia taarifa hizi," alisema askari mwingine.

Nianavyo mimi;
Mkuu wa Gereza na viongozi wengine sio askari!.
 
Back
Top Bottom