Wafungwa wauana kwa visu

Mkuu zomba,
Naona hujanielewa. Nilikuwa nasema hivi, kwa vile utaratibu ni kwamba mtuhumiwa anakamatwa na kuwekwa mahabusu kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi kabla ya kesi kwenda mahakamani, sasa hawa wenzetu tayari wapo gerezani wanatumikia vifungo vyao. Je watatolewa gerezani wapelekwe mahabusu ili wahojiwe au inakuwaje? Na je wakipelekwa mahabusu si watakuwa wamekatishiwa vifungo vyao vya sasa? Au mahabusu yao itakuwa gerezani humo humo? Na je kama tuhuma zao za sasa zinadhaminika na wakatimiza masharti ya dhamana wataruhusiwa kuwa nje ya mahabusu? Umenisoma Mkuu wangu?

TUMBIRI (PhD, Hull University - UK),
tumbiri@jamiiforums.com

Nimekusoma. Watakuja waatalamu zaidi kujibu hoja zako. Nijuavyo, ukiwa mfungwa na una kesi zingine za kujibu, unakwenda mahakamani na inahesabika kuwa ni mfungwa.
 
Watu wanashangaa ya Butimba, Hebu waende Gereza la Isupilo pale Mafinga-Mufindi-Iringa washuhudie mauaji yanayotokea kila kukicha! Isupilo ndio Gwandanamo ya Afrika, askari kuua mfungwa ni suala la kawaida sana tena anaua huku akisema "nitatoa maelezo",

Nimefika pale kwakweli serikali inatakiwa kuwajibishwa kwa yanayoendelea kutokea!

Mfungwa yeyote Tanzania akihamishiwa gereza lingine na akisema aliwahi/anatokea Gereza la Isupilo anaheshimika na kupewa saluti popote pale!
 
Mkuu katika Magereza ya Tanzania Manyapara wanatumika kama sales agent wa bange,Unga,sigara na mengineyo wa maaskari magereza.So nyapara anakuwa na Nguvu,kibri kuliko ata baadhi ya Askari.

Chipukizi na Kimbunga.

Kuna movie moja tafuteni inaitwa Midnight Express kuna kijana mmoja alifungwa Uturuki mkiona movie hiyo ndio mtajua jera sio mchezo ubabe na mateso...
 
Last edited by a moderator:
Huyo Mkuu wa gereza
Anapaswa kuwajibishwa haraka sana. Inakuwaje wafungwa wanakuwa na visu gerezani? Maanaake uongozi wa gereza hauko makini.
 
Wana kila kitu kuna wale wapishi wanakuwa hata na mashoka kabisa na kama utulivi muda mrefu askari wanazoea(kazi kwa mazoea) wanaanza kuwamini hao,kumbika pia wengine wanashinda kulima kwenye nyumba za wakubwa wanaiba zana ndogo ndogo,wanaingia nazo...wana mbinu nyingi sana hao ona hvy hvy....
 
Chipukizi na Kimbunga.

Kuna movie moja tafuteni inaitwa Midnight Express kuna kijana mmoja alifungwa Uturuki mkiona movie hiyo ndio mtajua jera sio mchezo ubabe na mateso...
ritz hiyo move hiyo inapatikana wapi? Hivi mkuu Magereza ya Uturuki ni sawa na ya Tanzania?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom