Wafanyakazi wa hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma wapewe maua yao

TheCrocodile

JF-Expert Member
May 31, 2021
1,077
2,814
Nilikwenda hapo hospitali ya Benjamin Mkapa siku ya Alhamis wiki iliyopita, nikiwa na tatizo ambalo lilihitaji wabobezi. Mimi ninaishi Dodoma, baada ya kutafakari sana, nikakata shauri kuwa niende tu. Mwanzoni niliwaza labda niombe ruhusa kazini, nifunge safari Dar niende hospitali kubwa kubwa hizi za private, lakini nikasema ngoja tu niwajaribu hawa Benjamin Mkapa.

Niseme kuwa, tangu nimefika pale huduma zimekuwa ni nzuri sana kama ifuatavyo:
1. Watoa huduma wana upendo mkubwa kwa wagonjwa, na hawana hasira wala frustrations,wanakuelekeza kwa upendo mkubwa nini cha kufanya. Hata ikitokea mgonjwa ukaghafilika na kuanza kufoka/kutoa lugha chafu, hawakurudishii kwa kukufokea, bali wanakusikiliza shida ni nini na wanakutuliza na kukuelekeza utaratibu na kukusikiliza shida nini.

2. Utaratibu wao umenyooka, ukifika cha kwanza unachukua namba kutoka kwenye vimashine, na unahudumiwa kulingana na muda uliokuja (first in, first out), isipokua kwa wale ambao wanaumwa sana

3. Ile hospitali ina vifaa na vipimo vya kisasa, na watoa huduma wanavitendea haki kwa kuvitumia kwa usahihi kwa ajili ya tiba ya wagonjwa wao-Nimepata huduma ya kibingwa kwa bei rahisi sana, mimi nimewahi tibiwa Aga Khan hospitali Dar es salaam huduma za kibingwa, yaani gharama zake kama ningeenda hapo ingekua ni zaidi ya mara 20. Sijasikia malalamiko ya mara leo kifaa hiki kimeharibika, kesho CT Scan haifanyi kazi sijui.
Kwa kweli watoa huduma pale wanajitahidi mno mno, kuanzia mfagiaji hadi daktari bingwa unaona wote wana motisha ya hali ya juu ya kuhudumia wagonjwa wao.

Of course, changamoto hazikosekani, kwa mfano wanazidiwa sana na wagonjwa, kunakua na foleni kubwa mno, ila hili liko nje ya uwezo wao, kwa kweli wanatimiza ahadi ya viapo vyao kuwahudumia wagonjwa kwa upendo. Nimekua impressed sana na huduma zao, na pia kikubwa zaidi motisha na upendo wao kwa wagonjwa, kwani wana sura zenye bashasha na hawana makasiriko, na wanajua namna ya kudeal na wagonjwa, hata yule ambae ana hasira, hawamfokei wanamtuliza na kumshusha chini, kisha kutatua changamoto yake kwa upendo.

Niseme wazi, nimeenda hospitali nyingi za serikali kupata huduma, sijawahi kukutana na nilichokiona Benjamin Mkapa...!! Sijui serikali imefanya nini pale hadi hali hii kumea kwa wafanyakazi, ila chochote walichofanya inabidi wakifanye kwa hospitali zao zote ziwe namna hii, its super super impressive!!
Wizara ya Afya Tanzania naomba sana, hii hospitali muiangalie kwa jicho zuri na muwape sana kongole watumishi wake, na muendelee kuwajali sana, hawa watu wanafanya kazi yao kwa upendo na kwa moyo mkubwa sana.

Hospitali zingine za serikali, please nendeni Benjamin Mkapa mkajifunze wenzenu wanachofanya muige, hakuna ubaya kuiga mambo mazuri!!

Watanzania wengi tumekua wapesi kukandia pale ambapo jambo fulani linatuudhi, ila si wepesi kusifia tunapokua impressed. Nimeamua kuandika post hii ili kuonyesha appreciation yangu, in the spirit ya kuwatia moyo wafanyakazi wa hii hospitali kwa kazi kubwa wanayofanya.

Wafanyakazi wote wa Benjamin Mkapa, Mwenyezi Mungu awabariki mno mno, nimeona niwape maua yenu wakati bado mna uwezo wa kusikia harufu yake!

Hongereni sana
 
Bora iyo kuliko amana.

Amana unaenda na mgonjwa mahututi usiku unaangaika kumbeba mwenyewe Wala hawajishughurishi..ila hongera kwa nurse mmoja mweupe anavaa ushungi anajitaidi sana yupo upande wa emergency.

Wengine wajitaidi kujirekebisha...na Yule mama wa chumba Cha maiti ajitaidi kuwa na kauli nzuri..Hongera kwa hospitali ya Benjamin.W.Mkapa
 
Lipa vizuri , usilimbikize madeni, wape nafasi ya kujiendeleza kitaaluma kila mfanyakazi atakuwa poa sana, mgonjwa utabebwa mgongoni kabisa....
 
Kumbe ulienda hapo Kuwajaribu tu kama ulivyosema katika Maelezo yako hapa hivyo na Wao pia waliamua kukupa Huduma yao kwa Kukujaribu.

Nakuomba sasa Safari ijayo ukienda hapo tena usiende na Lengo la Kuwajaribu bali nenda kwa Kudhamiria kisha kwa Utakachokipata hapo / huko tutakuomba uje hapa hapa JamiiForums utuambie na ikiwezekana uanzishe na Thread yake kabisa sawa?
 
Nilikwenda hapo hospitali ya Benjamin Mkapa siku ya Alhamis wiki iliyopita, nikiwa na tatizo ambalo lilihitaji wabobezi. Mimi ninaishi Dodoma, baada ya kutafakari sana, nikakata shauri kuwa niende tu. Mwanzoni niliwaza labda niombe ruhusa kazini, nifunge safari Dar niende hospitali kubwa kubwa hizi za private, lakini nikasema ngoja tu niwajaribu hawa Benjamin Mkapa.

Niseme kuwa, tangu nimefika pale huduma zimekuwa ni nzuri sana kama ifuatavyo:
1. Watoa huduma wana upendo mkubwa kwa wagonjwa, na hawana hasira wala frustrations,wanakuelekeza kwa upendo mkubwa nini cha kufanya. Hata ikitokea mgonjwa ukaghafilika na kuanza kufoka/kutoa lugha chafu, hawakurudishii kwa kukufokea, bali wanakusikiliza shida ni nini na wanakutuliza na kukuelekeza utaratibu na kukusikiliza shida nini.

2. Utaratibu wao umenyooka, ukifika cha kwanza unachukua namba kutoka kwenye vimashine, na unahudumiwa kulingana na muda uliokuja (first in, first out), isipokua kwa wale ambao wanaumwa sana

3. Ile hospitali ina vifaa na vipimo vya kisasa, na watoa huduma wanavitendea haki kwa kuvitumia kwa usahihi kwa ajili ya tiba ya wagonjwa wao-Nimepata huduma ya kibingwa kwa bei rahisi sana, mimi nimewahi tibiwa Aga Khan hospitali Dar es salaam huduma za kibingwa, yaani gharama zake kama ningeenda hapo ingekua ni zaidi ya mara 20. Sijasikia malalamiko ya mara leo kifaa hiki kimeharibika, kesho CT Scan haifanyi kazi sijui.
Kwa kweli watoa huduma pale wanajitahidi mno mno, kuanzia mfagiaji hadi daktari bingwa unaona wote wana motisha ya hali ya juu ya kuhudumia wagonjwa wao.

Of course, changamoto hazikosekani, kwa mfano wanazidiwa sana na wagonjwa, kunakua na foleni kubwa mno, ila hili liko nje ya uwezo wao, kwa kweli wanatimiza ahadi ya viapo vyao kuwahudumia wagonjwa kwa upendo. Nimekua impressed sana na huduma zao, na pia kikubwa zaidi motisha na upendo wao kwa wagonjwa, kwani wana sura zenye bashasha na hawana makasiriko, na wanajua namna ya kudeal na wagonjwa, hata yule ambae ana hasira, hawamfokei wanamtuliza na kumshusha chini, kisha kutatua changamoto yake kwa upendo.

Niseme wazi, nimeenda hospitali nyingi za serikali kupata huduma, sijawahi kukutana na nilichokiona Benjamin Mkapa...!! Sijui serikali imefanya nini pale hadi hali hii kumea kwa wafanyakazi, ila chochote walichofanya inabidi wakifanye kwa hospitali zao zote ziwe namna hii, its super super impressive!!
Wizara ya Afya Tanzania naomba sana, hii hospitali muiangalie kwa jicho zuri na muwape sana kongole watumishi wake, na muendelee kuwajali sana, hawa watu wanafanya kazi yao kwa upendo na kwa moyo mkubwa sana.

Hospitali zingine za serikali, please nendeni Benjamin Mkapa mkajifunze wenzenu wanachofanya muige, hakuna ubaya kuiga mambo mazuri!!

Watanzania wengi tumekua wapesi kukandia pale ambapo jambo fulani linatuudhi, ila si wepesi kusifia tunapokua impressed. Nimeamua kuandika post hii ili kuonyesha appreciation yangu, in the spirit ya kuwatia moyo wafanyakazi wa hii hospitali kwa kazi kubwa wanayofanya.

Wafanyakazi wote wa Benjamin Mkapa, Mwenyezi Mungu awabariki mno mno, nimeona niwape maua yenu wakati bado mna uwezo wa kusikia harufu yake!

Hongereni sana
Hongera kwa hosp kuficha kifo cha nusura
 
Mabosi wote wapi hapo, walete za kuleta si watatumbuliwa.
 
Niseme wazi, nimeenda hospitali nyingi za serikali kupata huduma, sijawahi kukutana na nilichokiona Benjamin Mkapa...!! Sijui serikali imefanya nini pale hadi hali hii kumea kwa wafanyakazi, ila chochote walichofanya inabidi wakifanye kwa hospitali zao zote ziwe namna hii, its super super impressive!!
Ni kweli kabisa hali ya BWM Hospital ni tofauti kabisa utadhani siyo hospital ya serikali, japo kuna vimelea vya rushwa kwenye vipimo.
 
Hilo ni sahihi, mama yangu amepata hapo matibabu bora kabisa baada ya kuhangaika hospital za private bila kugundua shida.

Alikuwa na shida ya miguu kuwaka moto na mikono pia, lakini Tulipata kujua shida baada ya kumpeleka hapo Benjamini Mkapa, alikutwa ana tatizo la pingili za mgongo zilipishana zikawa zinasagana kwa sasa amepewa dawa na mazoezi yupo vizuri kabisa.
 
Tunatofautiana. Nilivyoenda pale kupata huduma, sikuona kama wataalamu wako vizuri, kuna vitu wanapungukiwa. Majengo na miundombinu mengine ni mazuri lakini wataalamu wake hawapo makini ikiwemo specialists ambao nilitegemea wawe makini zaidi.
 
Nilikwenda hapo hospitali ya Benjamin Mkapa siku ya Alhamis wiki iliyopita, nikiwa na tatizo ambalo lilihitaji wabobezi. Mimi ninaishi Dodoma, baada ya kutafakari sana, nikakata shauri kuwa niende tu. Mwanzoni niliwaza labda niombe ruhusa kazini, nifunge safari Dar niende hospitali kubwa kubwa hizi za private, lakini nikasema ngoja tu niwajaribu hawa Benjamin Mkapa.

Niseme kuwa, tangu nimefika pale huduma zimekuwa ni nzuri sana kama ifuatavyo:
1. Watoa huduma wana upendo mkubwa kwa wagonjwa, na hawana hasira wala frustrations,wanakuelekeza kwa upendo mkubwa nini cha kufanya. Hata ikitokea mgonjwa ukaghafilika na kuanza kufoka/kutoa lugha chafu, hawakurudishii kwa kukufokea, bali wanakusikiliza shida ni nini na wanakutuliza na kukuelekeza utaratibu na kukusikiliza shida nini.

2. Utaratibu wao umenyooka, ukifika cha kwanza unachukua namba kutoka kwenye vimashine, na unahudumiwa kulingana na muda uliokuja (first in, first out), isipokua kwa wale ambao wanaumwa sana

3. Ile hospitali ina vifaa na vipimo vya kisasa, na watoa huduma wanavitendea haki kwa kuvitumia kwa usahihi kwa ajili ya tiba ya wagonjwa wao-Nimepata huduma ya kibingwa kwa bei rahisi sana, mimi nimewahi tibiwa Aga Khan hospitali Dar es salaam huduma za kibingwa, yaani gharama zake kama ningeenda hapo ingekua ni zaidi ya mara 20. Sijasikia malalamiko ya mara leo kifaa hiki kimeharibika, kesho CT Scan haifanyi kazi sijui.
Kwa kweli watoa huduma pale wanajitahidi mno mno, kuanzia mfagiaji hadi daktari bingwa unaona wote wana motisha ya hali ya juu ya kuhudumia wagonjwa wao.

Of course, changamoto hazikosekani, kwa mfano wanazidiwa sana na wagonjwa, kunakua na foleni kubwa mno, ila hili liko nje ya uwezo wao, kwa kweli wanatimiza ahadi ya viapo vyao kuwahudumia wagonjwa kwa upendo. Nimekua impressed sana na huduma zao, na pia kikubwa zaidi motisha na upendo wao kwa wagonjwa, kwani wana sura zenye bashasha na hawana makasiriko, na wanajua namna ya kudeal na wagonjwa, hata yule ambae ana hasira, hawamfokei wanamtuliza na kumshusha chini, kisha kutatua changamoto yake kwa upendo.

Niseme wazi, nimeenda hospitali nyingi za serikali kupata huduma, sijawahi kukutana na nilichokiona Benjamin Mkapa...!! Sijui serikali imefanya nini pale hadi hali hii kumea kwa wafanyakazi, ila chochote walichofanya inabidi wakifanye kwa hospitali zao zote ziwe namna hii, its super super impressive!!
Wizara ya Afya Tanzania naomba sana, hii hospitali muiangalie kwa jicho zuri na muwape sana kongole watumishi wake, na muendelee kuwajali sana, hawa watu wanafanya kazi yao kwa upendo na kwa moyo mkubwa sana.

Hospitali zingine za serikali, please nendeni Benjamin Mkapa mkajifunze wenzenu wanachofanya muige, hakuna ubaya kuiga mambo mazuri!!

Watanzania wengi tumekua wapesi kukandia pale ambapo jambo fulani linatuudhi, ila si wepesi kusifia tunapokua impressed. Nimeamua kuandika post hii ili kuonyesha appreciation yangu, in the spirit ya kuwatia moyo wafanyakazi wa hii hospitali kwa kazi kubwa wanayofanya.

Wafanyakazi wote wa Benjamin Mkapa, Mwenyezi Mungu awabariki mno mno, nimeona niwape maua yenu wakati bado mna uwezo wa kusikia harufu yake!

Hongereni sana
Umenena vyema.nawjua hawa watu nami pia NI shuhuda.wamenitibu pia na Mzee wangu walintibu baada ya wengine kufeli.ila Dodoma general hospital NI kichefuchefu. Hawajielewi
 
Kwa Mkoa wa Dodoma, nadhani Benjamin Mkapa Hospital kama haishiki namba 1 kwa ubora wa huduma, basi itakuwepo kwenye 3 bora. Nilishawahi kufanyiwa upasuaji fulani pale, kwa mafanikio makubwa.

Hivyo naunga mkono hoja! wanastahili kupewa maua yao. Kiukweli wako well organized.
 
Kuna Magunga hospital ya mji wa KOROGWE ni hatari Sana kwanza vipimo hamna huduma ni mbovu wahudumu wapo busy na Mambo Yao..hata kipimo Cha wingi wa damu hakuna ...mkuu wa wilaya joketi tunaomba upite hapo
 
Back
Top Bottom