IHOLOMELA
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,807
- 1,672
Kwa uongozi wa hospitali,
Nachukua fursa hii kutoa malalamiko yangu kuhusu suala la mende katika wodi za kulazwa wagonjwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa hapa Dodoma. Ingawa hospitali hii inatoa huduma nzuri kwa ujumla, suala la mende katika Wodi mbalimbali hospitalini hapo ni kero kubwa inayotia doa hospitali hii kubwa na yenye ubora hapa nchini.
Mende wamekuwa wakitambaa juu ya vitanda vya wagonjwa, vifaa vya tiba, na hata kwenye kuta za vyumba vya wodi. Hali hii ni hatari sana kwa afya na ustawi wa wagonjwa, na kwa kweli linakwenda kinyume na azma ya hospitali hii kutoa huduma bora na mazingira salama na safi.
Naomba uongozi wa hospitali hii kuweka mkazo kuhusu katika usafi na furmigation mara kwa mara na pia kuwa na utaratibu mzuri wa kusafisha na kutunza wodi. Pia ni muhimu kwa hospitali kuwa na ukaguzi wa mara kwa mara wa mazingira ili kubaini chanzo cha tatizo hili na kuweka mikakati sahihi ya kudhibiti mende kwa njia inayofaa.
Kwa sababu hiyo, tungependa kuona uongozi wa hospitali ukiangalia suala hili kwa umakini na kuchukua hatua za haraka kulimaliza tatizo hili la mende.
Tunatarajia kuona hatua za haraka zikichukuliwa kukabiliana na tatizo la mende katika wodi za kulazwa wagonjwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa. Tutafuatilia kwa karibu utekelezaji wa hatua hizo na tunatarajia kusikia kutoka kwa uongozi wa hospitali katika kipindi kifupi.