SoC03 Wafanyabiashara wanakerwa usumbufu wa taasisi za umma. Kisa kodi na tozo

Stories of Change - 2023 Competition

Mzee Wa Info_tz

New Member
Aug 31, 2022
4
5
WAFANYABIASHARA WANAKERWA USUMBUFU WA TAASISI ZA UMMA. KISA KODI NA TOZO.

Wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasikiliza wafanyabiashara wa Kariakoo, Mwezi Mei 2023 Mkoani dar es salaam, Kulikuwa na Malalamiko Mengi kuhusu Utozaji, Ukusanyaji na Aina za Kodi, tozo au Ushuru.

Katika Maelezo Mengi ya wazungumzaji Kuhusu Kilichosababisha Wasifungue Maduka, Mbali na kutoridhishwa na Mtindo wa Kukusanya kodi hizo pia Kero ilikuwa ni Kukosekana kwa Taasisi chache za Umma zinazo toza wafanyabiashara hao.

Kwa kawaida Kodi za Serikali zinatozwa kwa Makundi Mawili Makuu, ambayo Kwanza ni Serikali Kuu na Pili ni Mamlaka za serikali za Mitaa Kupitia Halamshauri.

Kero Kubwa iliyopo kwa wafanyabiashara ni namna Makundi hayo Mawili yanavyokusanya kodi zake, Mfano Serikali kuu Kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Taasisi za Kisekta kwa Kila wizara, Pamoja na Halmashauri Kupiti ushuru na tozo Mbalimbali.

Kama mwana JF, SOC, Ninadhani Kuna Mahali serikali Haitaki kuwajibika au haina nia ya kuwarahisishia wafanyabiashara katika shughuli zao, ama inapenda kuona hizo kero zikiendelea kuwepo Miongoni mwa Wafanyabiashara nchini.

Kwa nini Nasema hivyo, Ikiwa Kweli Tunapenda Wafanyabaisahara wasisumbuliwe na Taasisi ambazo zimekuwa kupitia watendaji wake zinachangia kutoa Hongo ili kutosumbuliwa ni Lazima Tufanye maamuzi ya Kuunganisha Kodi,Tozo au Ushuru Ulipwe Katika Makundi Mawili ili Biashara zifanywe kwa Urahisi.

Kundi La kwanza ni Fedha Kodi na Tozo zote za Serikali Kuu, ikijumuisha Taasisi zilizo Chini ya Wizara Kama TBS, TMDA, OSHA, zimamoto (Fire) Na Nyingine Kama hizo Zilipwe TRA na taasisi hizo zibaki na Kazi ya Kuhudumia Pekee.

Kundi la Pili Kodi, Tozo au Ushuru wa Mamlaka za serikali za Mitaa zilipwe Ofisi Moja, Kwa Mjumuisho wenye Uwazi.



INAWEZEKANAJE.

Awali ya Yote ni Kufanya Mifumo ya serikali ionane au ipokezane Taarifa, Kupitia Ulimwengu wa Kidijitali, Mamlaka ya serikali Mtandao eGA ioneshe uwezo wake kikamilifu, ukizingatia Kuwa serikali Ndiyo inamiliki Mkongo wa taifa ni rahisi Kuzipatia Taasisi zake Mtandao wa Internet wa Uhakika Ili mifumo ya Taarifa ionane. Jambo hili linawezekana kama Ilivyofanywa kwenye Mfumo wa Umeme, Tozo za Mama alizoweka pamoja Kodi zote zilizowekwa Sekta ya Mafuta na Miamala ya Simu mifumo ilionana na ikakata fedha.

Kwa sasa wafanya Biashara wa mafuta Hawalalamiki kusumbuliwa kwa kuwa katika Kodi zake, hawafuatwi na EWURA wala watoza nyingine Kibao kwa sababu zikishakatwa serikali ndio huzigawanya kwenda Kwa taasisi husika.

Hivyo Ukinunua Umeme Kodi za taasisi ambazo zingemfuata Mwananchi Moja kwamoja Zinajigawia zenyewe Fedha iliyokatwa Kwa Mara Moja.

Kwa Msingi Huo kwa sasa Serikali Iweke Uwazi Kuwa (kwa Mfano) Unayeanzisha Duka Gharama za Kuilipa serikali ni kama Ifuatavyo, TBS 10,000 , Fire 5,000 ,Wakala wa Vipimo 20,000 N.k Kisha hizo fedha Zote zilipwe Kwenye Akaunti Moja, Ikishawekwa Hela mfumo wa Malipo uzigawanye, Wakate Kila Mmoja Asilimia Zinazomhusu ili Kumuepushia Usumbufu Huyo Mfanyabiashara.

Mtindo huo utaenda kwa kila Mfanyabiashara kutegemea na aina ya biashara yake anayoifanya kama ni Mifugo zitaangaliwa taasisi za Mifugo kama ni kilimo vivyohivyo.

Kundi la Pili ni Halamshauri. Kwa kuwa kila halmashauri huwa na sheria ndogo zinazowapa uwezo wa kujikusanyia Mapato ya Ndani, Kwa hapa watawekewa Mfumo ambao umeratibu kwa kila Halamshauri gharama zilizo wazi ili kila mfanyabiashara wa Halamshauri ajue shughuli yake inalipwa kiasi gani kwa akaunti Moja tu ambayo ndiyo italipa Idara Nyingine.

Kinachopaswa Kuzingatiwa na serikali au Vyombo vitakavyokuwa vinakusanya kodi, Tozo na Ushuru huo ni Kuhuisha kanzi Data Kila Wakati (Data Base Upgrading and refreshing)ili kuwa na kumbukumbu kuwa Mtu A, amelipa Fedha Kiasi Fulani na yeye Hufanya Shughuli Fulani ambayo hakulipa Kiasi Fulani hivyo ikatwe iende Kwa Taasisi Fulani kwa wakati.

Kwa Kufanya hivyo kwanza Kutaifanya Serikali iwe na ufanisi katika Ukusanyaji wa Kodi na maduhuli yote kwa kuwa kutakuwa na gharama za uendeshaji Ndogo na Makusanyo Mengi. Pili kutafanya Serikali iaminike na isiwe sehemu ya kisababishi au Kichochea Rushwa kupitia Mifumo isiyoeleweka na watendaji wasio waaminifu.

Muhimu Kujua kuwa Hatua hizi ili zifanye kazi kikamilifu lazima pia Ziende sambamba na Utatuzi wa kero Nyingine wanazolilia wafanyabaishara kama Kuwa na kodi Kubwa zisizowiana na biashara husika.

Ikumbukwe kuwa kutofungia Biashara na Kuacha kodi ziendelee kuwa Kubwa na zinazotozwa na utitiri wa taasisi Hakuwi na Msaada kwa mfanyabiashara Bali inakuwa na Msaada kwa Wategemezi wa Hiyo Biashara hasa vibarua.

Ewe Mwana JF, SOC, Kwa Andiko hilo ninaomba Kura yako.
 
Back
Top Bottom