Wafanyabiashara walioficha Sukari waanza kukamatwa

Wafanyabiashara walioficha Sukari waanza kukamatwa

Kauli ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameficha sukari ili kutengeneza uhaba sokoni utakaopandisha bei ya bidhaa hiyo, imedhihirika baada ya baadhi ya wafanyabiashara hao kuanza kukamatwa wakiwa na vidhibiti.

Kutokana na hali hiyo iliyosababisha bei ya bidhaa hiyo kuanza kupanda, Waziri Mkuu Majaliwa, alitangaza uamuzi wa Serikali kuagiza sukari yake nje itakayouzwa kwa bei elekezi kwa wananchi ya Sh 1,800 kwa kilo, ili kuzuia ongezeko hilo haramu la bei.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Saidi Amanzi alitangaza polisi kuwashikilia wafanyabiashara wawili wa mjini hapa kwa tuhuma za kukutwa na zaidi ya mifuko 655 ya sukari, sawa na tani 24.3, ikiwa imekifichwa kwenye stoo zao.

Kwa mujibu wa Amanzi, wafanyabiashara hao walikamatwa kwenye msako ulioendeshwa na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa Singida pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Amanzi alisema kuwa msako huo uliendeshwa baada ya kupata taarifa za siri kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wameficha sukari, ili waje kuiuza kwa bei ya juu kwa wateja wao kwa kisingizio kuwa kuna uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo.

“Katika msako huo, tumemnasa Mohamed Alute Ally (44), mfanyabiashara wa eneo la Unyankindi aliyekutwa na mifuko 335 ya kilo 25 kila mmoja na Yusufu Suleiman (39), mfanyabiashara wa eneo la Minga katika manispaa ya Singida aliyepatikana na mifuko 320 ya kilo 50,” alisema.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa mwito kwa wafanyabiashara wote kuacha kuficha bidhaa zote muhimu, ikiwemo sukari na mchele, bali waiuze kwa bei halali kwa wateja wao.*

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Joseph Mchina, amesema msako mkali unaohusisha kikosi kazi maalumu pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama utaendelea kwa nguvu zote na kusisitiza kuwa kuhodhi bidhaa kwa sababu yoyote ile ni kosa la uhujumu uchumi.

Mmoja wa Wakala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC Moshi Mjini, Salim Nagji, amesema mfuko mmoja wa sukari huuzwa Sh 92,650 lakini tangu sukari iadimike mfuko unauzwa kati ya Sh 115,000 na Sh 120,000 huku kilo moja ikiuzwa kati ya Sh 2,400 na Sh 2,800 kwa kilo kinyume na bei elekezi ya Sh 1,800.
inaelekea sukari haina uhaba ila wafanyabiashara wanatengeneza uhaba ili kuendesha kile enzi zile kiliitwa ulanguzi. sasa sukari ikiwa tele wananchi wanalanguliwa, ikiwa haba wanalanguliwa..ndio enzi zile za ujamaa tukasema ubepari ni unyama. wafanyabiashara ni walafi na wabinafsi, hiyo ndio dini yao. lazima kuwadhibiti kwa nguvu ili waache unyonyaji.
 
Watanzania si wazalendo kabisa mnatetea watu wanohujumu uchumi??

Mh. Rais alikua na malengo mazuri tu alivopiga marufuku uagizwaji wa sukari nje lengo lake ilikua ni viwanda vya ndani vifufuke vijana wapate ajira na viwanda vingine vijengwe ili kukidhi mahitaji ya ndani, kumbuka kama viwanda vingefufuka na vingine kujengwa ingetuwezesha sasa sisi kua na akiba nyingi bei ikapungua na kuweza kufanya nchi ikaanza ku export sukari nje ya nchi hivyo kuongeza fedha za kigeni na kuweza kuokoa thamani ya shilingi.

Lakini tusivyo wazalendo tunatetea matumbo yetu kwa kuficha sukari ili ionekane viwanda vimeshindwa kukidhi mahitaji ya ndani na serikali iruhusu uagizaji wa sukari nje. Madhara yake ni makubwa sababu viwanda vya ndani vitakufa sababu uzalishaji wake utapungua vijana watapoteza ajira na hela nyingi za kigeni zitatumika kuagiza sukari nje hivyo thamni ya shilingi ya Kitanzania itaendelea kuporomoka.

saa nyingine tuwe tunafikiria kwa kina kabla ya kukurupuka kucomments hao ni wafanya biashara wawili tu mkoa moja Je Tanzania nzima ni wafanya biashara wangapi wameficha sukari? wakiamua kuiachia je sukari itaendelea kupanda?

Fikirien kwa makini
 
Kama kuhifadhi bidhaa stoo, basi stoo zote zifungwe, ili maduka yageuke kuwa stoo. Hiyo mifuko 300, kama mfanyabiashara ni muuzaji wa jumla, mbona ni kidogo sana?
 
Watanzania si wazalendo kabisa mnatetea watu wanohujumu uchumi??

Mh. Rais alikua na malengo mazuri tu alivopiga marufuku uagizwaji wa sukari nje lengo lake ilikua ni viwanda vya ndani vifufuke vijana wapate ajira na viwanda vingine vijengwe ili kukidhi mahitaji ya ndani, kumbuka kama viwanda vingefufuka na vingine kujengwa ingetuwezesha sasa sisi kua na akiba nyingi bei ikapungua na kuweza kufanya nchi ikaanza ku export sukari nje ya nchi hivyo kuongeza fedha za kigeni na kuweza kuokoa thamani ya shilingi.

Lakini tusivyo wazalendo tunatetea matumbo yetu kwa kuficha sukari ili ionekane viwanda vimeshindwa kukidhi mahitaji ya ndani na serikali iruhusu uagizaji wa sukari nje. Madhara yake ni makubwa sababu viwanda vya ndani vitakufa sababu uzalishaji wake utapungua vijana watapoteza ajira na hela nyingi za kigeni zitatumika kuagiza sukari nje hivyo thamni ya shilingi ya Kitanzania itaendelea kuporomoka.

saa nyingine tuwe tunafikiria kwa kina kabla ya kukurupuka kucomments hao ni wafanya biashara wawili tu mkoa moja Je Tanzania nzima ni wafanya biashara wangapi wameficha sukari? wakiamua kuiachia je sukari itaendelea kupanda?

Fikirien kwa makini

Well said mkuu, tatizo hapa watu wanapofushwa na itikadi za vyama - kuna baadhi ya Watanzania ambao hawakubali kwamba mteule wao alishindwa katika uchaguzi uliyopita, ukichunguza hao ndio wanabeza beza kila kitu anacho kifanya Dk.Magufuli - wanataka ashidwe ili waseme kiko wapi?

Watanzania sisi watu wa ajabu sana - yaani tuko radhi viwanda vyetu vya sukari vifungwe watu wakose ajira, wakulima wa miwa wadogo wadogo wakose kipato na vijana wengi wakae vijuweni, hawajali hujuma zinazo fanywa na wafanya biashara kukwanisha Sugar Industry ndani ya Taifa letu, hawana habari kwamba kuficha sukari no moja ya hujuma za kiuchumi as if hawajui lengo la kuficha sukari lina maana gani, watu wenye upeo mdogo wanadhani wafanya biashara wanao ficha sukari wanataka kuiuza kwa bei ya kuruka wakati hiyo si kweli - wanacho taka ni ku create artificial shortage ili Serikali iwape vibari vya kuagiza sukari kutoka nje wa flood market ili mwisho wa siku viwanda vyetu vikose soko, sukari iwadodee - hizi ni akili gani za kutaka kunufaisha kiuchumi nchi za wenzetu!

Badala ya kumuhunga mkono Dk.Magufuli kuhusu suala la Sukari, sisi tunaleta kashfa na dhalau za kijinga - wakumbuke Watanzania wengi tunao lutakia mema Taifa letu tuna muhunga mkono Dk.Magufuli by 100%.
 
tangu walipozuia sukari ya nje kuingia kwa kisingizio cha kulinda viwanda vya ndani tuliwaambia huu mchezo wa kuficha sukari mmejipangaje kuudhibiti?
 
Na mimi mje mnikamate nimeficha gunia moja nasubiri bei iendelee kupanda niuze.
 
Hahahahaha nawaonea huruma hao ma DC wanaweweseka! Kuweka store mzigo wako ndio kuficha? Waende viwandani wakaone stock ilivyojaaa! Uchumi huria! Agizeni tani 100,000 ambazo ndio mapungufu ya nchi! Walioficha wataitoa maana bei itashuka! Wancheza game za kutumia nguvu badala ya kutumia akili ya biashara huria! Aibu!!!
 
Hao waanzilishi wa ukomunisti wameshaukimbia baa kuona hautelekezeki! Sisi sijui tunakurupukia tu mambo bila hata kuelewa! Shame! Hao DC sijui hata kama wanaelewa wanafa nini!
 
Hao waliowashika ni wajinga sana. Mifuko hiyo ni kidogo sana kwa wafanya biashara wawili.
 
Kwani wakificha tatizo liko wapi au watakuwa kila siku wananunua product yote kiwandani na kuficha?

Madhara yake wewe unanunua kilo kwa 2500 wakati ungeweza pata kwa sh 1800
 
Kumbe tunampenda kumsikiliza Mwl Nyerere akiwa anaongea tu, hatupendi enzi zake zirudi!!! Mie naombea zirudi enzi zake ili vijana wa leo waonje ladha ya Mwl ili wakiwa wanamsifia au kumponda wawe na uhakika na wanachokifanya!
yaani hapahapa ndo tutakamata wanafiki.
Ooh nyerere alikua mchapakazi,sokoine alikua kiboko.
Sasa magufuli akianza kuact kinyerere na kisokoine wanaanza kulaumu
 
Huu ni upuuzi wa hali juu kutumia rasilimali chache kukamata wafanyabiashara badala ya kuagiza sukari au kuzalisha ikidhi mahitaji. Hao walioficha wangewaacha kisha serikali ikaingiza sukari ya kutosha.
...Wangeamua kushusha bei au kuimwaga sukari yao ili kuongeza uhitaji....
 
yaani hapahapa ndo tutakamata wanafiki.
Ooh nyerere alikua mchapakazi,sokoine alikua kiboko.
Sasa Magufuli akianza kuact kinyerere na kisokoine wanaanza kulaumu
Binafsi sioni tatizo la "Unyerere na Usoko4" kwa Mheshimiwa Raisi. Tatizo nnaloliona ni UKOSEFU wa MWONGOZO, Kanuni, na MFUMO wa utendaji kazi. Hizo sera za Kisoshalisiti (walizotumia Nyerere na Sokoine) ndio zinazotekelezwa na CCM sasa? (Maana Mheshimiwa Raisi amesikika akisewaagiza Viongozi wa CCM wasimamie Vionozi wa Ki-Serikali kusimamia "sera" za CCM).....
 
Hivi kuna sheria ya kumlazimisha mtu kuuza bidhaa zake kwa wakati asiotaka?
Kwani akiweka ikioza atawadai fidia?
Hivi soko huria hufanyaje kazi yake!
 
Hivi hujui kila mfanyabiashara lazima afuate masharti ya leseni?..ikiwa ni pamoja na kutoficha mali ili kumyanyasa mteja kwa kuuza bei kubwa?...ndio maana kuna Sumatra,Ewura ili kudhibiti bei kumlinda mlaji.Hii biashara ya sukari itatulia tu,baadhi ya walanguzi wanatumia wanasiasa uchwara kuneemeka.Ila udhibiti endelevu utatuliza bei...hata kwenye mabasi kabla ya Sumatra tulisota.......ninachokuambia kwa udhibiti wa serikali hii...sukari haitalipa walanguzi...!
Kuna sumatra na ewura na ya sukari ni ipi?
Hao sumatra na ewura wenyewe ni mzigo kwetu, badala ya kutupunguzia ankara za maji, tunalipishwa pesa ya mishahara na magari yao!
 
Back
Top Bottom