Wafanyabiashara walioficha Sukari waanza kukamatwa

Wafanyabiashara walioficha Sukari waanza kukamatwa

serekali sasa inataka ku peleka lawama kwa wafanya biashara ili kuficha aibu. kwanza serekali ikubali kwamba kuzuia sukari ya nje ilikua ni kosa. pili hii iwe fundisho siku nyingine msifanye maamuzi kwa kukurupuka na kutafuta sifa.
 
kichwa cha habari kisomeke hivi.

BAADA YA KUANZA KUKATA KAMATA WAFANYABIASHARA WA SUKARI BIDHAA HIYO SASA HAIKAMATIKI KWA BEI.
 
Huyo wakala wa kiwanda cha sukari TPC - Moshi anasema kwa kawaida sukari ya mfuko wa kilo 50 wanauza TZS. 92,500

Waziri mkuu (serikali) inaelekeza kuwa sukari iuzwe kwa TZS. 1,800 kwa kilo.

Sasa mbona wafanya biashara itakula kwao iwapo watauza kwa bei hii?

Hebu cheki hapa; 1,800 × kiroba cha 50kg = TZS. 90,000!!. Hakuna faida hapa ila ni hasara!!

Nimejiuliza ni nini hasa mantiki ya agizo hili maana halitekekezeki!!?

Mimi nilikuwa nadhani labda serikali ingetangaza mpango maalumu wa kutoa ruzuku kwa wazalishaji ili kutoka hukohuko kiwandani sukari ishuke bei kwanza badala ya kulazimisha tu wafanyabiashara wa rejareja kuuza bidhaa hii muhimu nje kabisa ya bei halisi ya sokoni!!
 
Cha msingi ni kuboresha viwanda wazalishe sukari kwa wingi tu.
 
Back
Top Bottom