Wafanyabiashara walioficha Sukari waanza kukamatwa

Wafanyabiashara walioficha Sukari waanza kukamatwa

Yaani mfanyabiashara kahifadhi sukari ghalani kwake nyinyi mnasema kaficha???! Hii serikali imefilisika kichwani.

Kumbe walitaka ahifadhi wapi?
Yaani mfanyabiashara kahifadhi sukari ghalani kwake nyinyi mnasema kaficha???! Hii serikali imefilisika kichwani.

Kumbe walitaka ahifadhi wapi?

Hivi dogo hujui kuwa...kutokufungua duka ni kukukiuka masharti ya leseni.Sasa wewe una mali halafu hutaki kuuza utashitakiwa.Hivi PM Majaliwa alivyoagiza maafisa biashara wakague maghala,hukujua kuwa ni kwa mujibu wa sheria?
 
Huu ni upuuzi wa hali juu kutumia rasilimali chache kukamata wafanyabiashara badala ya kuagiza sukari au kuzalisha ikidhi mahitaji. Hao walioficha wangewaacha kisha serikali ikaingiza sukari ya kutosha.
Kwa hiyo na mafuta ya petroli tuache tu wayafiche, serikali itaagiza mengine kutoka nje kwa kutumia foreign currency researve yake!! Sasa wewe huoni kwamba huu ni uhujumu uchumi. Wilaya zingine zitekeleze agizo la PM haraka kama ambavyo Singida wamefanya.
 
wkamatwe tu kwani wanazolotesha uchumi kwa sababu ya kutaka vijisent.
 
Hii ndio faida ya maamuzi ya kukurupuka. Yaani mtu ukiwa na sukari umeiweka ghalani tayari wewe ni muhalifu. Tatizo ni kwamba mahitaji na sukari tunayozalisha hapa nchini ni tofauti, vinginevyo hao wenye kuficha wasingefanya hivyo. mbona bidhaa nyingine watu wamehifadhi matani kwa matani lakini hakuna upuuzi kama huu!
 
Hivi dogo hujui kuwa...kutokufungua duka ni kukukiuka masharti ya leseni.Sasa wewe una mali halafu hutaki kuuza utashitakiwa.Hivi PM Majaliwa alivyoagiza maafisa biashara wakague maghala,hukujua kuwa ni kwa mujibu wa sheria?
Mkuu nimefungua duka ila stoo yangu nimefunga. Au na stoo zetu ziwe wazi.
 
Kila mwaka mimi huwa nanunua mpunga naweka stock nasubiri bei ikipanda nauza kwaiyo mwaka huu mtanikamata?
 
Hivi dogo hujui kuwa...kutokufungua duka ni kukukiuka masharti ya leseni.Sasa wewe una mali halafu hutaki kuuza utashitakiwa.Hivi PM Majaliwa alivyoagiza maafisa biashara wakague maghala,hukujua kuwa ni kwa mujibu wa sheria?
Mkuu acha kudanganya watu.

Kama hakuna mgogoro wowote, hakuna sheria inayokulazimisha kufungua duka lako.

Lakini kufunga duka kwa mgomo hilo kweli ni kosa. Sasa je hao wafanyabiashara wamefanya kosa lipi? Kuifadhi hizo sukari ndio kosa?

Je kuna wengine walikuwa hawaendelee kuuza?

Kama hao wawili wameifadhi hizo sukari lakini wengine wanauza, hapo hamna kosa.

Bottom line, kufunga duka lako sio kosa. Kosa ni kulifunga kwa mgomo na kutolipa kodi.
 
Huu ni upuuzi wa hali juu kutumia rasilimali chache kukamata wafanyabiashara badala ya kuagiza sukari au kuzalisha ikidhi mahitaji. Hao walioficha wangewaacha kisha serikali ikaingiza sukari ya kutosha.

Ndugu Nchi yeyote hufanya jitihada mbalimbali kulinda Viwanda au soko la ndani, kuzuia uingizaji au kupandisha kodi ni moja ya njia hizo.
Usijijar wewe tu, kuna maelfu ya wenzetu wanategemea Kuliko cha miwa kuishi, so Viwanda vikifa tegemea wao kuishi maisha magumu zaidi (Watakosa soko), wengine watakosa ajira, kuwa nchi tegemezi na upotefu mkubwa wa Mapato ya serikali.
Kwa Hapo Watanzania tunatakiwa kushirikiana kuzuia hawa walanguzi wenye Bia ovu, kuficha mzigo, Mzigo uadimike na Wao waongeze bei.
Mbona kwenye mafuta tuliungana kupinga hizi inshu za ulanguzi?
 
Kwa hiyo na mafuta ya petroli tuache tu wayafiche, serikali itaagiza mengine kutoka nje kwa kutumia foreign currency researve yake!! Sasa wewe huoni kwamba huu ni uhujumu uchumi. Wilaya zingine zitekeleze agizo la PM haraka kama ambavyo Singida wamefanya.
Kwenye biashara kuna kitu kinaitwa immaterialism.

Mifuko 655 ni kiwango kidogo sana, labda ungeniambia tani 1000 hapo ningekuelewa.
 
watu walitoa ahadi nying sana ila taratibu naona wameanza kuonja ugumu wa kuongoza nchi,tutashuhudia mengi sana awamu hii
 
Kwanza mifuko 655 ni kiasi kidogo sana kusema eti mtu "ameficha sukari"

Kwa sababu sukari ni very very fast moving product.

Afu unamkamata mtu kwa kuvunja sheria hipi? Kuifadhi mifuko 655 ya sukari ndo kosa?

Hawa jamaa wame lose focus, they are acting like fools.
Huu ni upuuzi, yaani mtu anunue bidhaa halali aihifadhi ghalani kwake aje aonekane ana makosa! Mtu kama kaamua kutouza bidhaa kwani yeye ndio anayezalisha? Viwanda vizalishe sukari kwa wingi huyo aliyeamua kuficha atanywea chai na watoto wake
 
Ukomunisti na ujamaa ulioshindikana kwingine umerudi,nchi imerudi miaka 40 nyuma,au kwa vile alifananishwa na sokoine???!!!!! Mpaka October namba zitasomeka sawasawa
 
Back
Top Bottom