Wafanyabiashara walioficha Sukari waanza kukamatwa

Wafanyabiashara walioficha Sukari waanza kukamatwa

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,878
Reaction score
5,765
Kauli ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameficha sukari ili kutengeneza uhaba sokoni utakaopandisha bei ya bidhaa hiyo, imedhihirika baada ya baadhi ya wafanyabiashara hao kuanza kukamatwa wakiwa na vidhibiti.

Kutokana na hali hiyo iliyosababisha bei ya bidhaa hiyo kuanza kupanda, Waziri Mkuu Majaliwa, alitangaza uamuzi wa Serikali kuagiza sukari yake nje itakayouzwa kwa bei elekezi kwa wananchi ya Sh 1,800 kwa kilo, ili kuzuia ongezeko hilo haramu la bei.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Saidi Amanzi alitangaza polisi kuwashikilia wafanyabiashara wawili wa mjini hapa kwa tuhuma za kukutwa na zaidi ya mifuko 655 ya sukari, sawa na tani 24.3, ikiwa imekifichwa kwenye stoo zao.

Kwa mujibu wa Amanzi, wafanyabiashara hao walikamatwa kwenye msako ulioendeshwa na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa Singida pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Amanzi alisema kuwa msako huo uliendeshwa baada ya kupata taarifa za siri kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wameficha sukari, ili waje kuiuza kwa bei ya juu kwa wateja wao kwa kisingizio kuwa kuna uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo.

“Katika msako huo, tumemnasa Mohamed Alute Ally (44), mfanyabiashara wa eneo la Unyankindi aliyekutwa na mifuko 335 ya kilo 25 kila mmoja na Yusufu Suleiman (39), mfanyabiashara wa eneo la Minga katika manispaa ya Singida aliyepatikana na mifuko 320 ya kilo 50,” alisema.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa mwito kwa wafanyabiashara wote kuacha kuficha bidhaa zote muhimu, ikiwemo sukari na mchele, bali waiuze kwa bei halali kwa wateja wao.*

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Joseph Mchina, amesema msako mkali unaohusisha kikosi kazi maalumu pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama utaendelea kwa nguvu zote na kusisitiza kuwa kuhodhi bidhaa kwa sababu yoyote ile ni kosa la uhujumu uchumi.

Mmoja wa Wakala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC Moshi Mjini, Salim Nagji, amesema mfuko mmoja wa sukari huuzwa Sh 92,650 lakini tangu sukari iadimike mfuko unauzwa kati ya Sh 115,000 na Sh 120,000 huku kilo moja ikiuzwa kati ya Sh 2,400 na Sh 2,800 kwa kilo kinyume na bei elekezi ya Sh 1,800.
 
Mmmmh....tunarudi kwenye ujamaa kwa kasi ya kimbunga,muda si mrefu maduka ya ujamaa na mashamba ya nguvu kazi yatarudi,kila kitaendeshwa kwa amri.Ngoja tuone mwisho wa movie hii.

Hivi hujui kila mfanyabiashara lazima afuate masharti ya leseni?..ikiwa ni pamoja na kutoficha mali ili kumyanyasa mteja kwa kuuza bei kubwa?...ndio maana kuna Sumatra,Ewura ili kudhibiti bei kumlinda mlaji.Hii biashara ya sukari itatulia tu,baadhi ya walanguzi wanatumia wanasiasa uchwara kuneemeka.Ila udhibiti endelevu utatuliza bei...hata kwenye mabasi kabla ya Sumatra tulisota.......ninachokuambia kwa udhibiti wa serikali hii...sukari haitalipa walanguzi...!
 
Let's see where these communist policies will take us to as a nation.Let's cheer and clap our hands for now.
Hivi hujui kila mfanyabiashara lazima afuate masharti ya leseni?..ikiwa ni pamoja na kutoficha mali ili kumyanyasa mteja kwa kuuza bei kubwa?...ndio maana kuna Sumatra,Ewura ili kudhibiti bei kumlinda mlaji.Hii biashara ya sukari itatulia tu,baadhi ya walanguzi wanatumia wanasiasa uchwara kuneemeka.Ila udhibiti endelevu utatuliza bei...hata kwenye mabasi kabla ya Sumatra tulisota.......ninachokuambia kwa udhibiti wa serikali hii...sukari haitalipa walanguzi...!
 
Kwani kuweka stoke ni shida... au kuna limit??
Nasema wanakurupuka. Wampeleke mahakamani kama hatawashinda. Kuna sheria inayosema ukiwa na duka lazima uuze mali yako? Nikamua kufunga duka nitaambiwa nimehodhi bidhaa, crazy! Siwatetei waficha vitu lakini wakae wazungumze kama kweli wanapata faida au hasara na wafikie consensus sio watafute umaarufu wa kisiasa kwa wananchi
 
Hivi hujui kila mfanyabiashara lazima afuate masharti ya leseni?..ikiwa ni pamoja na kutoficha mali ili kumyanyasa mteja kwa kuuza bei kubwa?...ndio maana kuna Sumatra,Ewura ili kudhibiti bei kumlinda mlaji.Hii biashara ya sukari itatulia tu,baadhi ya walanguzi wanatumia wanasiasa uchwara kuneemeka.Ila udhibiti endelevu utatuliza bei...hata kwenye mabasi kabla ya Sumatra tulisota.......ninachokuambia kwa udhibiti wa serikali hii...sukari haitalipa walanguzi...!
Yaani mfanyabiashara kahifadhi sukari ghalani kwake nyinyi mnasema kaficha???! Hii serikali imefilisika kichwani.

Kumbe walitaka ahifadhi wapi?
 
Wanaacha kufikiria ni jinsi gani wataongeza production wao wanakimbilia kutafuta walioweka stock yao ndani.

Zalisha kwa wingi mpaka bei ishuke watatoa wenyewe hiyo sukari yao
Kwanza mifuko 655 ni kiasi kidogo sana kusema eti mtu "ameficha sukari"

Kwa sababu sukari ni very very fast moving product.

Afu unamkamata mtu kwa kuvunja sheria hipi? Kuifadhi mifuko 655 ya sukari ndo kosa?

Hawa jamaa wame lose focus, they are acting like fools.
 
Back
Top Bottom