Waepuke wanawake masikini

😁😁 Mkuu tusifike huko, komenti yangu inahisiana na thread hii sina tatizo na wewe kama member wa Jf
Ok, nilifikiri nakupigia makelele ndio maana nikakuelekeza procedures za kuni-ignore
 
Kwasasa tafsiri ya mtu masikini sio mtu anayeshindwa ku afford chakula

Ni mtu anayeshindwa ku afford luxury life.

Hata wanaosema hawako tayari ku date na mtu masikini hawakusudii mtu asiyeweza kumudu milo mitatu kwa siku.
ooh basi mi nipo tofauti na wengine,, ukiweza kulipa kodi, uhakika wa milo mitatu, out mara 2 kwa mwezi aiii mbona kwangu ni tajeeer kabisa
 
Iko hivi uko sahihi naheshimu mtazamo wako
 
Lakini sio kwa ubaya, watu wanataka kukata mnyororo wa umasikini.

Sio kuviziana per se, Mi nimekulia uswahilini, my peers wengi wameishia form 2, form 4 wengine wamezaa, wanaruka ruka kazi hawafanyi , biashara hawana, siku moja kwenye kupiga story wanasema kupata ndoa ni ngumu blah blah, nikawachana tu fanyeni kazi, jishughulisheni, na muwe na realistic expectations kuhusu mahusiano mbona ndoa ni nje nje …….. Sio kwa ubaya mwanaume anapokuangalia ana picture familia yake miaka kumi ijayo na wewe……

Hivyo hivyo, binafsi if i want a man to leave me alone, nisijisikie guilty (maana kutongozwa pia ni heshima) nikitaka aondoke kwa heshima, inategemea tumekutana wapi, namwambia sina kazi , sijapata kazi, sina mtaji wa biashara, sina chochote nakaa kwetu tu napikia wazee, chances are 80% wanajikata shwaaa! πŸ˜…
 
Umasknini wa mwanamke,kwangu si moja ya sifa nazotumia kumchagua
 

Sio vibaya; lakini mtu akikupima kwa umasikini/poverty tayari anakuwa amekupima kwa "material things"; tafsir yake ni kwamba hata kama una mindset nzuri; mtafutaji, wife material tayari unakosa sifa kwake kwa kigezo hicho. Yeye anakuwa anakupima kwa vitu vinavyoonekana sio mindset yako ambayo ndio future yako/yenu. Kuna watu wazuri wenye "future" watashindwa kuolewa kwa kigezo hicho.
Hata hivyo sikupingi; ni sawa tuu. 😊
 
Mkuu uko sahihi kabisa. Kuchagua mwenza kwa usahihi ni njia moja wapo ya kupambana na adui masikini. Pia upo uwezekano kupunguza poverty circle kwa kizazi chako. Mwanamke awe na shughuli ya kufanya.
 
Kama wanawake kufanya kazi, hajawaanza leo wala jana. Mimi binafsi nimezaliwa na wazazi ambao wote walikuwa watumishi wa umma, lakini sikuwahi kuona haya maujinga ya haki sawa.

Ni vijana wa sasa nyoronyoro ndio wanakuja na hizi agenda uchwara za kutaka wanawake na wanaume wawe sawa.
 
Kweli kabisa, wanawake wengi wanafikiri kufanya kazi na kujenga maisha ya individually ni option sio hitaji la lazima. Ndipo hapo akiwa na kipato anaanza kujiita independent woman. Mwingine ataanza kusema badala ya kudanga nimeamua kufanya kazi hii. Ni kama wanajiona wanastahili noble prize kwa kuishi honest and decent life.

Chukulia mfano bodaboda aseme "badala ya kuwa jambazi nimeamua kuwa dereva". Hii maana yake ni kama anamajuto kutochagua hiyo njia ya ujambazi au kuna namna hilo wazo lilishawahi kumjia sema kwa sababu zake akaamua kuachana na hiyo njia.

Wanawake wemgi wanafikiri kutoka kimaisha kupitia mahusiano/kudanga ni rahisi. Ukweli ni kwamba hata mwanamke akiamua kuchagua career ya kudanga bado atahitaji connection na kujifanyia marketing, otherwise ataishia kupewa hizi elfu 20,30 ambazo amfikisha popote.

Inabidi wanawake wapanue fikra na wajue suala la kubadilisha maisha yao ni wajibu wao binafsi. No body owe you a noble prize for living a honest and decent life.
 
ooh basi mi nipo tofauti na wengine,, ukiweza kulipa kodi, uhakika wa milo mitatu, out mara 2 kwa mwezi aiii mbona kwangu ni tajeeer kabisa
Umeona sasa jinsi ulivyo piga u-turn?

Mchongo sio tena ishu ya chakula now ume switch kutoka kwenye milo mitatu hadi out mara 2 kwa mwezi

Maana yake hapa ume approach leisurely life in a smart move.

Kwasababu najua hizo out hujazipimia kuwa zifanyike kwenye mashamba ya mihogo ambapo pesa sio mchongo.

Hapana bila shaka kutakuwa kuna sehemu special ambayo huko ni Benjamin Franklin tu ndio anatamba. Dhana ambayo mwanzo haikuonekana kama kigezo ila now imejitokeza kama ishu ya dharula.
 
Sio vijana ni mifumo ya kidunia ndio inesimika huo usawa wa kijinsia. Vijana wanaji-adjust kwenye mfumo. You can't beat the system singlehandedly
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…