Wadogo zangu, kabla TV hazijaja enzi hizo mgeni alikuwa anapewa album atazame picha za zamani. Yaani umpe Mtanzania album asichomoe picha hata moja?

Hata hao wa 2003 wamezikuta wakiwa wadogo, hii technology ya picha kwa simu, tablets, to mention few!ni ya juzi tu 2010's
 
Mshua wangu alikuwa mpigapicha ukiachana na kazi yake ya kuajiriwa. Kuna siku alitishiwa kisu na tajiri ng'ombe mmoja kwa madai ya kwa nini picha ya mkewe imetoka ana makengeza wakati mkewe hana makengeza.
 
Kijana wa town niliamua kwenda na albamu yangu mkoani ili nikateke kijiji kwa sifa (nilikuwa nimeenda kuwasabahi babu na bibi).

Ile albamu ilikuwa na picha halisi za wachezaji wa Simba na Yanga. Basi wanakijiji walifurahi sana walipoona picha za wanasoka ambao walikuwa wakiwasikia tu Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) wakitangazwa na Ahmed Jongo,Juma Nkamia au Lando Mabula.

Baada ya muda picha karibu zote zilipotea mysteriously. Ilianza kupotea ya Malota Soma,ikafuata ya Dua Said, kisha ile waliyopigwa Twaha Hamidu,Thomas Kipese,Malota Soma na George Masatu wakiwa wamevaa jezi zimeandikwa Carlzeberg (ambao wala hawakuwa wadhamini wao bali wa Liverpool ya Uingereza).

Hata ile aliyopigwa Abdul Mashine wa Simba akikabana na Kenneth Mkapa wa Yanga nayo haikusalimika. NA ZILE PICHA ZINANIUMA HADI LEO.
 
Daaahh we jamaa wewe umenikumbusha mbali kinyamaaaa kitambo hicho aiseee nakumbuka mtaani kwetu kulikuwa na mpiga picha mmoja hivi dah nakumbuka tumetoka kula pilau la sikukuu basi tunamuita anakuja home alafu kipindi hicho nilikuwa navaa bwanga suruali yani ukichukua upande wa suruali wa mguu mmoja unatoa suruali nzima basi enzi hizo nilikuwa najiona nimetokelezea sana ila hawa watoto waliozaliwa 2003 wamekosa vitu vingi sana vya enzi hizoooooo
 
Nakumbuka mzee alikua na video tapes za Enrique Iglesias kulikua na videos kama bilamooooooos, sad eyes, maria maria za kina santana, kina Britney Spears, mzee alikua anamkubali sana Enrique mpaka akaniambukiza na mimi! Kipindi hicho Pierce Bosnan ndo alikua James Bond mpaka leo hii hizo ngona naskiliza! I realy miss me.
We nae unaonekana wajuz juz tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom