Wadogo zangu, kabla TV hazijaja enzi hizo mgeni alikuwa anapewa album atazame picha za zamani. Yaani umpe Mtanzania album asichomoe picha hata moja?

emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
 
Yale madebe yaliandikwa Korie, palikuwa na picha ya mwanaume aliyevalia nguo na kofia nyeupe(mavazi ya wapishi)
Daaah kweli kabisa mkuu, siku hizi hayapo tena mzee baba watu wanapikia mafuta ya alizeti na michikichi
 
Kwani smartphone zimetoka mwaka gani, mbona kama dharau zinazidi ? ..
 
Dah umenikumbimusha mbali sana. Pilau linapikwa mara 2 kwa mwaka na likipikwa wanaalikwa ndugu.

Wali ulitumia masaa 7 kupikwa maji yanachemshwa, nazi inakunwa moto unawekwa juu ya sinia.

Mgeni akija wa heshima jogoo anachinjwa.

Picha inapigwa huku umejipaka mafuta na kuweka dole.

Ligi za soka za mtaa, na mpira ukiisha ni ngumi mpaka apatikane mbabe wa mtaa.

Picha inapigwa kijijini kuipata ni baada ya mwezi, mpaka mpiga picha akaoshe picha mjini/studio.

Santuri ndio zinatumika, sahani kubwa nyimbo 3
Santuri ndio LP?
 
Umenikumbusha enzi zetu tuliozaliwa kijijini .
Wakati ule hakukuwa na toilet paper wala nini.
Ukimaliza kujisaidia haja kubwa unaburuzwa kwenye mchanga tu ( gushenenha)ndo imetoka.
Ndio maana sisi wakulungwa gozi ya makalio yetu ni kama ngozi ya limao.
Kadhalika, kaptula zetu za khaki zilikuwa na ukoko fulani (ngukulu) pale kwenye maungio ya mfereji wa makalio maana wakati ule kuvaa chupi ilikuwa ni anasa na hazikuwepo.
Kwa kweli wengine tumetoka mbali aisee.
 
Hakuna kitu nachoki miss kama drive in sinema pia enzi hizo
Tulikuwa wadg lkn tulikuwa tunatoka uswaz kuchk movie kurudi saa saba usiku
Natamani drive in ingerudi aise

Ova
Drive-in cinema si ndio ubalozi wa sasa wa USA ulipo?
 
Drive-in cinema si ndio ubalozi wa sasa wa USA ulipo?
Duh ndiyo hapo tulivyokuwa wadg tulikuwa tunaenda kuangalia sinema bubu...tunakaa njee
Kuna watu hapo wakat movie inaendelea wao ni kama wakalimani wanaadisia

Kingine wale wasafiri wenzangu na mie wa zamani issue yoyote ya picha ubalozini especially hzi za us na ulaya tulikuwa tunaambiwa twende kifotoa akber photos studio zanaki basi si foleni hapo
Mhindi yule alipiga sana hela wakat ule

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Drive-in cinema si ndio ubalozi wa sasa wa USA ulipo?
Ila ndani nishazamia sanaa watu wanapaki magari wanachk movie
Ila za mwiizi arobaini kna siku nlizamiaa mule
Mlinzi akatuotea wacha tuchezeee vibaoo na polisi juu tukapelekwa polisi wakaturudisha uswaz tulikula sana makonzi sijasahau hyoo mpaka leo

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka mzee alikua na video tapes za Enrique Iglesias kulikua na videos kama bilamooooooos, sad eyes, maria maria za kina santana, kina Britney Spears, mzee alikua anamkubali sana Enrique mpaka akaniambukiza na mimi! Kipindi hicho Pierce Bosnan ndo alikua James Bond mpaka leo hii hizo ngona naskiliza! I realy miss me.
Bruce leee ndo daaa!
 
Ajabu akija kwenu kachomoa anaenda kwake anaiweka kwenye album yake.

Siku ukienda kwake anakupa album yake uangalie ghafla unakuta ile picha ambayo huionagi nyumbani

Kimoyomoyo unasema kumbe bibi / babu na wewe ni mwizi ee?

Mwisho wa siku album yenu inabaki tupu

Sijui kwanini
Wengine wanatumia kishirikina halafu unashangaa kwanini maisha hayasongii
 
Umenena vyema. Tatizo la picha za enzi zile ni pale unapoambiwa picha yako iliingua. Sasa fikiria hiyo picha ilikuwa ya kumbukumbu ya harusi yako na huwezi tena kuirudia kwani wote waliokuwepo siku Ile wamesharudi makwao!. Sina uhakika kama vijana wamenipata hapo. Kuungua kwa picha ni pale Ile negative inakuwa nyeusi kabisa na ukiisafisha kutoa positive inakuwa nyeupe pee. Halafu sijui kama hata hiyo negative na positive wanaijua? Hiyo negative ni Ile itokayo kwenye kamera ili isafishwe na kuwa positive ambayo ndiyo picha utakayoiona. Na mtiririko mzima unaweza kuchukua hata miezi miwili kwani kumaliza utepe mmoja wa filamu ilikuwa kazi kwelikweli si kila mmoja alikuwa na uwezo wa kupiga picha. Kweli tumetoka mbali.
 
Halafu nyuma ya picha ndio tulikua tuna andika kwa kalamu tarehe ya siku ambayo picha hiyo imepigwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom