Wadau wa JF Jukwaa la Siasa, changieni JF isonge mbele

Wazo lako ni zuri sana mkuu Ritz lakini ulipoharibu ni hapo kwenye Pro-Chadema.
 
Pamoja na wizi unaofanywa na ccm bado pro-ccm wengi Kama Nape hawachangii hata cent Ngoja 2015 lazima niwe Tanzanite member
 
Mkuu Ritz why only pro-CHADEMA?

SHERIA NA KANUNI ZA JAMII FORUMS
.........

3. Kuleta makala au kuendeleza mijadala yenye kuleta ugomvi, uchochezi na
yenye muelekeo wa kutengenishana badala ya kuungana miongoni mwa wajumbe wa JAMII FORUMS na Watanzania wote kwa ujumla.


.....
GREEN: Invisible je mwanzisha uzi hajalenga kweli kuleta utengano katika Jukwaa kati ya Pro- Chadema na Pro- Vyama vingine ?
 
Last edited by a moderator:
Ngoja na sie CCM makini tuchangie kidogo ili tupambane kwa hoja na hawa vijana wa Cdm.
 
GREEN: Invisible je mwanzisha uzi hajalenga kweli kuleta utengano katika Jukwaa kati ya Pro- Chadema na Pro- Vyama vingine ?

Hakuna utengano mkuu nimetoa wito kwa Pro-Chadema Jukwaa la siasa wachangie kwani muitikio wao sio mkubwa. Nenda MMU, Chit-Chat, kaone Pro-Chadema kule walivyochangia JF.

JF Daima.
 
Last edited by a moderator:
Nililiandikia hili wiki iliyopita nikiomba tupatiwe namba maalum za hii mitandao yetu ili mwenye hata sh 1,000 aweze kuchangia kati ya registered members zaidi 101,000 tulionao mbali na huu uchangiaji wa kawaida. Mods wakaitupa haraka kule mbali ile thread!
 
Back
Top Bottom