WISDOM SEEDS
JF-Expert Member
- Jun 1, 2011
- 841
- 282
HUU NI MTAZAMO WANGU TU:
Kwa siku tatu mfululizo tangu Rais Jakaya Kikwete ahutubie wazee pale Diamond Jubilee nimekuwa nikijitahidi kusoma kila post inayowekwa kwenye Jukwaa la Siasa ili nisipitwe na habari zinazoendelea katika nchi yetu, hasa ikizingatiwa kuwa mimi niko mbali kidogo na nchi. Kuna wakati nilikuwa natamani kuchangia lakini nikawa nasita kutokana na ama kupandwa na hasira au kukerekwa na habari zinazowekwa humu.
Hakika kuna jambo moja kubwa nimeligundua: wasomaji na wachangiaji wa Jukwaa la Siasa wana nafasi kubwa ya kufariki vifo vya ghafla kutokana na stress zinazosababishwa na namna nchi inavyopelekwa! Huwa najiapiza kuwa nisiwe naingia Jukwaa la Siasa na badala yake niingie kwenye majukwaa mengine lakini kuna wakati nashikwa na "mshawasha" wa kutaka kujua nini kinaendelea nchini mwangu kwenye masuala ya kisiasa na kiuchumi, lakini kila nikiingia, baada ya dakika ishirini hivi huwa najikuta nimechanganyikiwa!