Wadau, mna maoni gani kuhusu vurugu inayofanyika Afrika Kusini?

Tony254

JF-Expert Member
May 11, 2017
16,017
16,427
Wadau, wiki iliyopita nimekuwa nikitazama hii kesi ya Jacob Zuma. Zuma alifungwa kifungo cha miezi 15. Alikamatwa usiku wa kuamkia Alhamisi. Wafuasi wake wakaanza kuandamana. Usiku wa kuamkia juma mosi walichoma trucks (Ukipenda trela yaani yale malorry makubwa) zaidi ya 30.

Baada ya kuchoma malorry hayo yaliyokuwa yanatokea port of Durban, wakaamua kutoa vurugu wikendi nzima kwa kuziba barabara kwa mawe na kuchoma tyres. Usiku wa kuamukia leo ndio tumeona sinema haswa. Yaani leo wameamua liwalo na liwe, sasa wameamua kuvunja malls na kuiba kabisa mali kama fridge, TV, sofa set na kadhalika.

Watu ni wengi na polisi ni wachache kwa hivyo polisi wameshindwa cha kufanya. Mimi nasema walete jeshi lao yaani SANDF pengine litaweza kutuliza hali.

Ona jinsi walibyochoma trucks zilizokuwa zimebeba mizigo

Ona watu wanavyoiba

Washenzi sana wanaiba bila hata uoga
 
Wa South nao wanaishi kiujanja ujanja vibaka wengi wanatumia mambo kama haya ya kuandamana ili wafanye uhalifu wa mali,haiwezekanai mtu mhalifu asihukumiwe kisa ana watu kama mzee Mpili,yani sheria ipindishwe kisa wafuasi wake wameandamana nchi yao ndo ulaya ndogo lkn watu wake ni UTOPOLO tu.
 
Tatizo watu wenyewe hawajasoma, hawana kazi na wanatamani mali ya wenzao. Sasa hawana namna ila kutumia kifungo hiki cha Zuma kama kisingizio ili waweze kuiba. Zuma alikata rufaa na mahakama inasikiliza kesi hio leo. Nadhani kwa sababu ya uharibifu mkubwa uliotokea, mahakama hio itamuachilia Zuma ili kupunguza hamaki ya wananchi.
 
Serikali ikomae tu, hatutaki mambo ya mungu mtu, kama una hatia ufungwe hata kama wewe nani.
Weusi tunatia huruma sana....
 
South Africa tatizo wazamiaji wengi ambao hawaajiriki kwa hiyo wanajiingizia kwenye mambo ya uhalifu...
Nchi ngumu sana ile...

Tanzania soko la kariakoo limeungua watu wanaonekana wakishangaa moto na siyo kuingia na kuiba...
 
Wadau, wiki iliyopita nimekuwa nikitazama hii kesi ya Jacob Zuma. Zuma alifungwa kifungo cha miezi 15. Alikamatwa usiku wa kuamkia Alhamisi. Wafuasi wake wakaanza kuandamana. Usiku wa kuamkia juma mosi walichoma trucks (Ukipenda trela yaani yale malorry makubwa) zaidi ya 30.

Baada ya kuchoma malorry hayo yaliyokuwa yanatokea port of Durban, wakaamua kutoa vurugu wikendi nzima kwa kuziba barabara kwa mawe na kuchoma tyres. Usiku wa kuamukia leo ndio tumeona sinema haswa. Yaani leo wameamua liwalo na liwe, sasa wameamua kuvunja malls na kuiba kabisa mali kama fridge, TV, sofa set na kadhalika.

Watu ni wengi na polisi ni wachache kwa hivyo polisi wameshindwa cha kufanya. Mimi nasema walete jeshi lao yaani SANDF pengine litaweza kutuliza hali.

Ona jinsi walibyochoma trucks zilizokuwa zimebeba mizigo

Ona watu wanavyoiba

Washenzi sana wanaiba bila hata uoga

Hao hawana hoja,ni vibaka,choka mbaya,wameona hii nafasi waitumie kuiba na kupora chini ya kivuri kwamba wanampigania mtu wa kabila lao,Zuma wanedai ameonewa, kwa kufungwa.
Hao vijana wasio na ajira,ama wanatumika,au wameona hii ni sababu nzuri ya kulianzisha na kupola kupunguza machungu ya maisha.
 
Back
Top Bottom