Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,890
- 14,601
Kusema mtu anayekuuliza kama umeelewa anajivuna ndiyo kujivuna kwenyewe.Kwa jinsi unavyojivuna kwenye haya maandishi yako huna tofauti na wanawake anaowasema mleta mada..una maringo ya kishamba sana eti "Do you even understand what that means? Kwahiyo unamuona mwenzio gharasa sana?
Kwa sababu ni sawa na kusema kuwa wewe huna uwezo wa kutoelewa, unaelewa kila kitu.
Na mtu akikuuliza kama umeelewa, kakutukana kwa ujivuni.
Ukiwa mwanafunzi wa aina hii, kila mwalimu atakapokuuliza "umeelewa?" kwa nia nzuri tu ya kuhakikisha mko pamoja, utaona kakutukana.
Hutaweza kujifunza vizuri, kwa sababu kujifunza vizuri kunahitaji ukubali kwamba kuna uwezekano wewe ukawa huelewi vitu fulani.
Swali la "umeelewa?" halina ujivuni, labda kama ujivuni unaonekana kutokana na "inferiority complex" ya anayeona ujivuni.
Kwa sababu walimu wazoefu wanajua hata mwalimu huwa anafundishwa na wanafunzi wake. Swali la "umeelewa?" linaweza kuzua uchambuzi utakaoonesha anayeuliza "umeelewa?" hajaelewa anachofikiri anaelewa, na anayeulizwa "umeelewa?" akawja kuonekana ameelewa vizuri kinachozungumzwa kuliko anayeuliza "umeelewa?".
Ni swali la kuhakiki kwamba wote tuko sawa kuliko kingine chochote. Ukifikiri kingine utakuwa na unyonge wa kujitakia mwenyewe.
Na kama umeangalia filamu ya "The King And I" utakuwa umeona mpaka wimbo wenye mashairi yanayosema hili.
Panua upeo wako, usiangalie mambo kwa ufinyu wa "inferiority complex".
Ukiwa na "inferiority complex" mtu anaweza kukusalimu tu "Hello" ukaweka swali, kwa nii kakusalimia, lazima atakuwa anakudharau.