Wachina wanne wakamatwa kwa tuhuma za Utekaji

Wachina wanne wakamatwa kwa tuhuma za Utekaji

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,280
Reaction score
3,946
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na majukumu yake ya msingi ya kuzuia vitendo vya kihalifu na kwa ujumla hali ya Jiji ni salama. Hata hivyo tarehe 14 Mei, 2026 majira ya saa 04:30 usiku Polisi walipokea taarifa kuwa katika majengo pacha ya 'PSSSF Mtaa wa Mission Ilala Dar es Salaam watu wawili 1. Weiyi Chen miaka 64, mfanyabiashara, raia wa China na 2. Liang Xiolo miaka 44, mfanyabisahara raia wa China ilidaiwa walivamiwa na kutekwa na kundi la wahalifu waliodaiwa kuwa saba nakupelekwa kusiko julikana.

Polisi kwa kushirikiana na kamisheni zingine za uchunguzi za Jeshi hilo ilifanikiwa kupata namba za magari ambayo yalidaiwa kutumika katika tukio hilo. Gari moja wapo lililokamatwa baadae lilikutwa likiwa na namba T.305 DRP aina ya Toyota Alphard ambazo sio namba halisi za gari hilo na gari lingine lililokamatwa ni lenye namba T.188 DHT aina ya Toyota Harrier. Watuhumiwa hao kabla ya kukamatwa walitoa vitisho kwa ndugu kuwa wapewe kwa njia ambazo wangewaelekeza dolla za kimarekani milioni 20 ili wawaachie.

Upelelezi wa Jeshi la Polisi ulifanikiwa kuwaokoa wahanga hao tarehe 16 Mei, 2026 na kukutwa wakiwa wamejeruhiwa na kuumizwa kwenye maeneo ya miili yao huko maeneo ya Mbezi Kinondoni. Wahanga walipelekwa hospitali ya Agakhan lakini Weiyi Chen bado hali yake sio nzuri na amelazwa katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa wanne wamekamatwa baada ya ufuatiliaji mkali kufanyika kuhusiana na tukio hilo ambao ni; 1. Deng Anqing miaka 49, raia wa China 2. Fan Zhong miaka 49, raia wa China 3. Zhang Jianjun miaka 51, raia wa China 4. Deng Qiang miaka 40, raia wa China. Wamekutwa na simu za wahanga na vielelezo vingine.

Upelelezi wa tukio hili unakamilishwa na kila aliyehusika katika tukio hili kwa namna moja ama nyingine atashughulikiwa kwa mujibu wa hatua stahiki zilizo ndani ya mifumo ya kisheria.

Polisi Dar es Salaam haikubaliani na vitendo vyovyote vya kihalifu na inaendelea kuwashukuru wananchi ambao wamekuwa wakitoa taarifa za kweli ambazo zimesaidia kuzuia uhalifu na zingine kuwakamata wanaojihiusisha na vitendo vya kihalifu.


1779710208283.png


1779710512168.png
 
Kuna kipindi nilisikia kuwa huko Luanda Angola wachina wanatekana sana wao kwa wao. Wameanza na hapa. Jamaa hawapendani ugenini!!
 
Kuna kipindi nilisikia kuwa huko Luanda Angola wachina wanatekana sana wao kwa wao. Wameanza na hapa. Jamaa hawapendani ugenini!!
Wachina ma mafia sana. Hapa mjini wanaendesha biashara ya kuuza malaya wa kichina kama wanauza simu. Sehemu za kamari zote kubwa kubwa ni zao na supermarket zao hawatoi risiti za TRA.
 
Wachina ma mafia sana. Hapa mjini wanaendesha biashara ya kuuza malaya wa kichina kama wanauza simu. Sehemu za kamari zote kubwa kubwa ni zao na supermarket zao hawatoi risiti za TRA.
Watu wanawaangalia wanawachukulia wepesi. Mamafia wa kichina, Triad wameweka watu wao kila kwenye fursa. Huko South East Asia kama Laos ni kama wameshika nchi.
 
Hivi kumbe yale ma movie ya KIXX huwa ni maigizo tuu hakuna uhalisia hata kidogo kwamba wachina wanaweza kujihami na wapo vizuri kwa hu haaa mastaaa...!

Mchina anatekwaje na wavuta bange walioshika mapanga tu?!
Wewe jamaa 😂 😂
 
Hao wachina waliovamiwa ni wafanya biashara wa nini?
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na majukumu yake ya msingi ya kuzuia vitendo vya kihalifu na kwa ujumla hali ya Jiji ni salama. Hata hivyo tarehe 14 Mei, 2026 majira ya saa 04:30 usiku Polisi walipokea taarifa kuwa katika
well done PT,

MNAFANYA KAZI NZURI SANA WAZEE WA KAZI :BASED:
 
Mbona hamjasema kua walikutwa na kadi za chama CCM.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Kuna kipindi nilisikia kuwa huko Luanda Angola wachina wanatekana sana wao kwa wao. Wameanza na hapa. Jamaa hawapendani ugenini!!
Miaka fulani nyuma nlikuwa na rafiki wa kichina,mtu ambaye tulizoeana sana
Tunapiga stori kwa lugha ya kiswahili
Akaniambia unajuwa bongo wako wachina triads(han)
Mafia ,ngoja niishie hapa
Ila wengi ndyo wako kwenye makamali nk

Ova
 
Watekaji wajulikana😂😅😆😄😃
 

Attachments

  • 20260525_174001.jpg
    20260525_174001.jpg
    166.1 KB · Views: 14
Hao waliteka Wachina wenzao ili kupata pesa.
Policcm na wenzao wengine wakiteka hakuna anayekamatwa
 
Back
Top Bottom