wewe mwenyewe sio mzalendo, mngekuwa wazalendo msingewanyanyasa abiria kwa bei mtakavyo. kumbuka mnachofanya siku za mwisho wa mwaka na sikukuuu. sisi wasafiri ndio tunaojua uchungu, wewe mwenye gari unayetaka tuwe wazalendo kwako tumefaidika nini toka kwako? kama usafiri hata mchina atatupatia, usijefikiri kuleta magari yenu mnatusaidia msaada. mbona maduka ya wachina bidhaa zao ni bei nafuu, hata tukijumua sisi wengine kwenye maduka ya jumla tunaona faida. kwenye biashara, wako
Kayaman asante .....
Watu wanasahau huyu mchina yeye ana msamaha wa kodi... kwa hilo tu ..the moment anaweka gari barabarani tayari ana unafuu mkubwa sana.... sisi wavuja jasho tutashindanaje nao?
Shida yetu ni mazingira yaliyojengwa na serikali kuwajali wawekezaji bila mipaka na kutusahau sisi wazawa tuliohangaika na hili taifa tangu uhuru hadi leo.
Tumewavusha wakati wote barabara zikiwa vumbi hadi leo kuna unafuu.
Je hizo youtong zingewapeleka mwanza enzi zile tunapiga shimo mwanzo mwisho siku tatu? Tulivumilia tukawafikisha watanzania wenzetu. Tulindwe basi twende na moderate speed kukua kufikia huko waliko wenzetu.
Mtaji wa ghafla hivyo kwa Tz hii tutapata wapi?
Uzalendo tunaouangalia ni serikali kupata kodi yake . Kama kodi inalipwa na Sheria hazivunjwi amna uzalendo zaidi ya huo mengine ni blablaaa
usilalamike hii ndo maana ya biashara huria.ushindani ni muhimu.ukiwa na huduma nzuri utapata abiria.hawa wachina wana huduma nzuri sana ktk mabasi yao nilishasafiri nao kutoka kahama hadi dar.boreshen huduma na sio kulalamika.Ndg zangu naombeni kuhoji kupitia jamvi hili ili na nyie mnisaidie
Mimi ni mdau wa biashara ya usafirishaji kwa njia ya barabara.
Tumevamiwa na tena tunakandamizwa hatupumui hata kidogo na hawa wawekezaji wapya WACHINA.
Nikizungumzia mabasi, leo hii kuna wachina wanapeleka mabasi route zote kutoka Dar. Na wako radhi kupakia abiria kwa bei wanayopenda wao, na kuondoa gari na abiria hata watano.
Ikumbukwe hao wachina ndio mawakala wa mabasi ya Yutong na Zhongton ambayo yako kwenye chart sasa.
Je isingekuwa vyema kwa hawa wachina kuwa restricted kwenye kutuuzia tu mabasi na sisi tufanye biashara ya usafiri?
Kumbuka mchina mmoja ana mabasi zaidi ya 150.
Wale watanzania tunaojenga uwezo na vibasi vyetu viwili, vinne hadi kumi je tuta-survive?
Kwa uelewa wa kawaida pale ubungo kwa siku yanatoka mabasi yasiyopungua 200. Katika hayo wamiliki ni zaidi ya 100. Maana yake ni kwamba uchumi umesambaa mikononi mwetu wenyewe. Je tukimwacha mchina atoe mabasi 50 peke yake akaja ma mchina mwingine tena, wamiliki watanzania tutapona? Mbaya zaidi ni kuwa mchina anaweza kuweka basi mpya kila mwezi, sisi tunaweza?
Kwa wale msiofahamu, wachina wanauza mabasi ambayo wameshatumia yenye namba B na C yote kwa bei punguzo. Na mimi nimenunua hapo kadhaa. Lengo lao ni kuhakikisha wanaendesha mapya kila wakati na sisi yetu yanaendeshwa miaka mitano. Ndiyo uwezo wetu kitanzania.
Hawa wenzetu wana access to capital huko kwao. Sisi kama yatima tunapambana tangu mavumbini hadi tulipopata cent ya kununua kamoja. Je ni halali kutufutilia mbali kwa namna hii?
Hii sera yetu ikoje? Serikali iko wapi? Mbona mnatufanya kitu mbaya hivi?
Kwenye Malori hali ndiyo mbaya zaidi. Inaogopesha mno. Kuna kampuni 4 za wachina kila moja ina zaidi ya malori 400. Wanaenda mipaka yote ya nchi kwa bei punguzo.
Halafu hao hao wachina wamenunua kampuni za clearing. Kwa hiyo wanatoa mizigo wenyewe na wanagawana wenyewe. Ukifanya sensa ya watanzania wenye gari moja hadi 20 ni wengi mno tumetapakaa nchi nzima na uchumi unasambaa. Je huyu mchina akichuma hapa anatuachia nini sisi wa matombo, ileje,masasi,na kwingineko nchini? Kodi zenyewe hawalipi wanaingiza magari kwa msamaha wa kodi. Huu usingizi wa serikali utaisha lini jamani???
Ziko bank za kitanzania nazifahamu zimekopesha wachina malori yasiyohesabika. Leo hii wewe mtanzania ukitaka moja process itachukua miezi sita na unakata tamaa hata hulipati.... ! Agha! Basi bana siendelei .... 😡
Na kweli hatushindwi ! Lakini hatujafikia hapo na wala hatuwaxhukii watanzania kwa kiwango hicho!
Ila najiuliza, hivi nyie mnaosupport wachina ni watanzania Kweli?
umebuuuuuugi,pole mimi sinunuagi mchina kilichopo Africa,nanunua mchina aliyepo USA NA ULAYA MAGHARIBIhata wewe mwenyewe ni jeneza linalotembea kwasababu mwili wako umejaa vitu vya kichina vitupu kuanzia nywele, heleni, makalio, nguo, viatu kila kitu hadi vyakula vipo vingine unakula vya kichina. mbona bado unaishi sasa
Ba Brio
Bora wachina mara mia, kwasababu mabasi yao ni bora, yana kiyoyozi, bei nafuuu na hawachinji kutoa makafara kama ninyi wabongo na mibasi yenu takataka mliyotengeneza bodi kenya. mmetunyanyasa vya kutosha na kwa miaka mingi sana mkipandisha bei mpendavyo, soko huria linaendelea itafika kipindi mtapaki hayo mangarangara yenu garage.
sisi abiria tunachohitaji sio basi la mtanzania, tunachohitaji ni usafiri bora, hatujali ni wa mtz au mchina au mzungu, na hata wewe ukipata hela yako mimi hainihusu ni yako wewe na watoto wako hivyo niko radhi hata kuungana na mchina ili basi lako life kama kutakuwa na maslahi. kwendeni zenu huko chinjachinja ninyi. mlizoea biashara za mabasi kwa uchawi mchina amekuja kufanya biashara kwa kutumia akili, au naye kawazidi nguvu kwa dini yake ya Confucianism?
Pambafuuuhawa namgome tena kumbemgomowenu sababu yawachina. Mtajibebaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Biashara siomabasii njoomuuze. condom nazo zinalipaaaa wapiidinaaaaa werraaaaweraaaa mzeematolaaaaa kijanaaaa wa panda ya.....
Uuuuuiiii.... mkuu ushindani hauwezekani bila governor kutoka serikalini. Level mbili tofauti sanaaaa.... sisi wa gari 5 na wa gari 150 tushindane kivipi? Wao wana access to capital..sisi je?
Wewe mwenyewe hapo kila siku unatamani upate mkopo ujikwamue lkn huna vigezo. Ndiyo tz yetu. Imebaki kulilia serikali tu.
Stop pretending guys. Dont take it so lightly, tutamalizwa. Hali ni mbaya... twaelekea pabaya...