kama wabongo wameshindwa kuchoma mahindi kariakoo wanaona aibu wataonekana masikini mbele za mademu zao, kwanini mchina asichome ili tununue? nyie endeleeni kuchagua kazi na kujifanya masharobaro kumbe mifukoni hamna kitu.uchumi wa nchi unayumba kila kitu kimeshafeli wachina utasikia hata wanachoma mahindi kariakoo usishangae.
Ndg zangu naombeni kuhoji kupitia jamvi hili ili na nyie mnisaidie
Mimi ni mdau wa biashara ya usafirishaji kwa njia ya barabara.
Tumevamiwa na tena tunakandamizwa hatupumui hata kidogo na hawa wawekezaji wapya WACHINA.
Nikizungumzia mabasi, leo hii kuna wachina wanapeleka mabasi route zote kutoka Dar. Na wako radhi kupakia abiria kwa bei wanayopenda wao, na kuondoa gari na abiria hata watano.
Ikumbukwe hao wachina ndio mawakala wa mabasi ya Yutong na Zhongton ambayo yako kwenye chart sasa.
Je isingekuwa vyema kwa hawa wachina kuwa restricted kwenye kutuuzia tu mabasi na sisi tufanye biashara ya usafiri?
Kumbuka mchina mmoja ana mabasi zaidi ya 150.
Wale watanzania tunaojenga uwezo na vibasi vyetu viwili, vinne hadi kumi je tuta-survive?
Kwa uelewa wa kawaida pale ubungo kwa siku yanatoka mabasi yasiyopungua 200. Katika hayo wamiliki ni zaidi ya 100. Maana yake ni kwamba uchumi umesambaa mikononi mwetu wenyewe. Je tukimwacha mchina atoe mabasi 50 peke yake akaja ma mchina mwingine tena, wamiliki watanzania tutapona? Mbaya zaidi ni kuwa mchina anaweza kuweka basi mpya kila mwezi, sisi tunaweza?
Kwa wale msiofahamu, wachina wanauza mabasi ambayo wameshatumia yenye namba B na C yote kwa bei punguzo. Na mimi nimenunua hapo kadhaa. Lengo lao ni kuhakikisha wanaendesha mapya kila wakati na sisi yetu yanaendeshwa miaka mitano. Ndiyo uwezo wetu kitanzania.
Hawa wenzetu wana access to capital huko kwao. Sisi kama yatima tunapambana tangu mavumbini hadi tulipopata cent ya kununua kamoja. Je ni halali kutufutilia mbali kwa namna hii?
Hii sera yetu ikoje? Serikali iko wapi? Mbona mnatufanya kitu mbaya hivi?
Kwenye Malori hali ndiyo mbaya zaidi. Inaogopesha mno. Kuna kampuni 4 za wachina kila moja ina zaidi ya malori 400. Wanaenda mipaka yote ya nchi kwa bei punguzo.
Halafu hao hao wachina wamenunua kampuni za clearing. Kwa hiyo wanatoa mizigo wenyewe na wanagawana wenyewe. Ukifanya sensa ya watanzania wenye gari moja hadi 20 ni wengi mno tumetapakaa nchi nzima na uchumi unasambaa. Je huyu mchina akichuma hapa anatuachia nini sisi wa matombo, ileje,masasi,na kwingineko nchini? Kodi zenyewe hawalipi wanaingiza magari kwa msamaha wa kodi. Huu usingizi wa serikali utaisha lini jamani???
Ziko bank za kitanzania nazifahamu zimekopesha wachina malori yasiyohesabika. Leo hii wewe mtanzania ukitaka moja process itachukua miezi sita na unakata tamaa hata hulipati.... ! Agha! Basi bana siendelei .... 😡
Kwa taarifa yako 95% ya mabasi yanayopiga mweleka ni scania, na matairi yanayoongoza kupasuka ni michelin na bridgestone ambayo hayatengenezwi china.
tatizo wabongo wengi hawaaminiki, hata mimi akija mchina na mbongo kwangu nitampa priority mchina kwasababu ninajua hatutasumbuana kuaiana hela ambayo ni haki yangu, mnalipana kimkataba fresh, mbongo aanze kuleta undugu hapa na kupiga kiswahili, wanini? hata wewe ukijenga uaminifu unaweza kuweka malori yako hata magogoni. uaminifu ni mtaji hasa kwenye mambo ya pesa. wabongo wengi ukiawadhamini aisee wanakuachia lubega unaanza kuhangaika nalo.ndio maana hujapeleka malori yako pale.Wachina wanajua kula na wenye Nchi. Kuna mmoja mwenye malori yadi yake ipo lugalo jeshini. Sijui kama kuna mtanzania anaweza ruhusiwa hata kilometer 1 karibu na kambi ya jeshi la china.
Na kweli hatushindwi ! Lakini hatujafikia hapo na wala hatuwaxhukii watanzania kwa kiwango hicho!
Ila najiuliza, hivi nyie mnaosupport wachina ni watanzania Kweli?
Ndgu ushindani ndio biashara yenyewe na hakuna anayeogopa, tatizo hakuna fair ground btn foreign na local investors wao wanapata some exemptions ambazo mswahili utabaki kuzisikia tu! na hiyo ya kupanda nauli december sio kosa letu wasomi mnasema high demand lead to increase in price sasa tatizo la mfanyabiashara liko wapi hapo?
Mlishawahi kufikiria kuondoa hiyo hali ? Kwa sababu hao ndo wanapandisha bei ili wapate cha kwao !! Udalali kialsehemu, eti mtu ukienda kununua matunda Buguruni unauziwa na dalali ilhali mwenye machungwa kasimama hapo hapo, ukienda Karume kumnunulia mtoto viatu vya shule ndo utakoma zaidi, mwenye kuuza viatu yupo, lakini nakuachia unapigwa bei na dalali !!!! Yaani nyie, acha tu muendelee kukaribisha udalali kwa kila kitu. Kwani ukinunu gari, ufungue ofisi na kuwaajiri watu mwnyewe na usitoe ticket zako kwa mtu mwingine huwezi kupakia ? Naomba ufafanuzi kwa kuwa fani yangu sio hiyo.
Hayo mabasi yetu mnayoyaita ngarangara Mengi( 90%) ni Scania 94. Zimetengenezewa body na na Say Dar coach. Ubora wa kutosha miaka 5 na zaidi
Zaidi ni msukumo wa chuki na wivu kwa ma bankers dhidi yaAcha kulaumu benki ....watanzania wengi wakikopeshwa mwezi wa kwanza tu wanaharibu! Hao wahindi,waarabu wanakopa wanalipa! Na benki zinawaomba wakope! Ifikie kipindi tujiangalie matatizo yetu na sio kila siku kutoa lawama zisizo na kichwa wala miguu! Benki haiangalii rangi inaangalia biashara watz wazawa wengi wakikopeshwa wanaharibu!
Hizo ngarangara zenu, siti zake ndogo na zimebanana, ziko fixed hauwezi kuadjust, ukifika mwisho wa safari duuu, ni kama ulikuwa unaendesha baiskeli ya Anita. Zile siti ziko kama EXCUTION CHAIR, na madirisha kufungua au kufunga mpaka muwe wanaume wawili! Mi nitapanda basi lenye ubora hata kama anamiliki SHETANI.
hivi wakati ule ninyi mnapopandisha nauli wakati wa xmass huwa mnafikiria wagonjwa, watu wanaosafiri kwenda kuona wagonjwa, misiba na mwingien kakopa nauli? huwa mnakuwa wazalendo kweli, nini huwa mnakuwa watz? hakuna watu wabaya kama TABOA hao wamiliki, kwanza mnawanyonya sana madereva wenu wanapata stress hadi wanadondosha magari, dereva akipata ajali akifa familia zao hamzijali, ninyi mnajali pesa tu. unafikiri ninyi ndio wazalendo? ninyi ndio mashetani wa nchi hii. bora wachina waje.
mabasi ya wachina ni new force aisee, amesambaza njia zote nchini tena mabasi mawilimawili kwa safari moja kila eneo. songea mawili kwenda mawili kurudi, tunduma mawili, mbeya mawili, kahama, mwanza, everywhere. asubuhi mchina anasimama mlangoni anasimamia ukusanyaji hela na basi likiondoka yeye ndio anarudi kulala. wako vizuri sana.Hatimaye wafanya biashara wamekuja bongo they mean "STRICTLY BUSINESS" by the way Mkuu naomba nsaidie kutaja majina ya hizo kampuni niwe ata napata usingizi safarini nimechoka kusafiri roho mkononi
Mkuu tuanze na hilo la udalali sokoni, nimewahi kuhusika na study iliyonipitisha kwenye hayo masoko.
Hakuna mkulima yeyote anayeweza kuuza bila dalali. Wameshikilia kuanzia mfumo wa uongozi mpaka upangaji wa bei.
The same na mabasi, hawa wamiliki wa basi moja hawezi kupata abiria bila dalali. Ukiweka dalali hapa Dar likienda mikoani litakutana nao, na akifanya mchezo hata huko wanaweza kumwekea kauzibe. Wana network yao. Na hapa ndipo serikali inapaswa kuingia ili kudhibiti hali.
Hata hao wachina hawatumii ofisi zao tu kukatia ticket, wanatumia pia agents.
Anachoelezea mleta thread ni kuwa pawepo na fair ground na kanuni zinazomlinda mzawa, ingawa nao wanapaswa kuboresha biashara yao.
mimi ninayo natural ya kinyatunzu chapa ya ng'ombe,sihitaji mchinakwahiyo hata makalio umenunua ya mchina yanayouzwa US na ulaya magaribi sio? hapo hujamkwepa mchina bado. yuko na wewe tu uendako.