Wachina kuvamia usafirishaji ni Halali?

Wachina kuvamia usafirishaji ni Halali?

Soko huria.... Hamjazoea ushindani sio cha moto mtakiona na tabia zenu za kupandisha nauli kiholela makonda wanakauli chafu, magari mabovu, huduma ndo usiseme..... Kwanini nisimkimbilie mchina anayejua nini maana ya mteja... Mabasi yana hadi Wi-fi....
 
hivi wakati ule ninyi mnapopandisha nauli wakati wa xmass huwa mnafikiria wagonjwa, watu wanaosafiri kwenda kuona wagonjwa, misiba na mwingien kakopa nauli? huwa mnakuwa wazalendo kweli, nini huwa mnakuwa watz? hakuna watu wabaya kama TABOA hao wamiliki, kwanza mnawanyonya sana madereva wenu wanapata stress hadi wanadondosha magari, dereva akipata ajali akifa familia zao hamzijali, ninyi mnajali pesa tu. unafikiri ninyi ndio wazalendo? ninyi ndio mashetani wa nchi hii. bora wachina waje.

Mkuu chunguza kidogo tu uambiwe kitu wanafanywa hao makonda nanmadereva wa mabasi au malori ya wachina! Ulizia kesi zilizopo ubungo au urafiki polisi.

Kwa taarifa tu ni kuwa nauli kupanda December hata mmiliki hanufaiki. Wananufaika tu mawakala wa usafirishaji. Wala Taboa wala mmiliki hanufaiki! Ni uzembe wa hiihii serikali.
 
mi gari zangu za mombasa hazipatagi ajali mara kwa mara kama za huko moshi,mwanza,mbeya. mi naenjoy zangu ndani ya TAHMEED huku natafuna tambuu,parik,au manikchand hadi nafika mombasa halafu pemben yangu kuna toto chotara tunabadilishana mawazo,hizo ajali zinanichosha hata kufikiria kwenda mbeya kusalimia bibi na babu
 
bora wachina mara mia, kwasababu mabasi yao ni bora, yana kiyoyozi, bei nafuuu na hawachinji kutoa makafara kama ninyi wabongo na mibasi yenu takataka mliyotengeneza bodi kenya. mmetunyanyasa vya kutosha na kwa miaka mingi sana mkipandisha bei mpendavyo, soko huria linaendelea itafika kipindi mtapaki hayo mangarangara yenu garage.

sisi abiria tunachohitaji sio basi la mtanzania, tunachohitaji ni usafiri bora, hatujali ni wa mtz au mchina au mzungu, na hata wewe ukipata hela yako mimi hainihusu ni yako wewe na watoto wako hivyo niko radhi hata kuungana na mchina ili basi lako life kama kutakuwa na maslahi. kwendeni zenu huko chinjachinja ninyi. mlizoea biashara za mabasi kwa uchawi mchina amekuja kufanya biashara kwa kutumia akili, au naye kawazidi nguvu kwa dini yake ya Confucianism?
Hayo ni majeneza yanayotembea,tokea lini mchina akaleta kitu bora Africa?
 
Mkuu chunguza kidogo tu uambiwe kitu wanafanywa hao makonda nanmadereva wa mabasi au malori ya wachina! Ulizia kesi zilizopo ubungo au urafiki polisi.

Kwa taarifa tu ni kuwa nauli kupanda December hata mmiliki hanufaiki. Wananufaika tu mawakala wa usafirishaji. Wala Taboa wala mmiliki hanufaiki! Ni uzembe wa hiihii serikali.
mbona magari ya mchina hayapandi nauli, ni kwasababu mchina anasimamia mwenyewe hadi bus linaondoka ndio anarudi home kwa mkewe. hao wapiga debe na mawakala ambao ninyi mnawaachia ili wanyanyase abiria, wa kulaumiwa ni ninyi mnaowaachia kwasababu wameshanunua tiketi zote ninyi mshaweka hela mfukoni hamjali kinachotokea huku nyuma. dawa yake waje wachina. pale ubungo hao wachina wa new force hagusi mpiga debe pale, mtu unaenda mwenyewe ofisini, hauendi kwa wakala. kwanini mnaweka mawakala? wakati mnazo ofisi, kama bus ni la kwako kwanini uendeshwe na mawakala na wapiga debe? ina maana wewe umejali pesa yako tu, kinachotokea huku nyuma mawakala kunyanyasa abiria wewe haikuhusu na haikuumi kwasababu ushachukua chako, na kwa namna hii ninyi sio wazalendo na mnafanya biashara kishamba sana.
 
bora tu wachina kila siku migomo mkome na muache migomo isiyokuwa na maana
 
Wacha kulialia, bado usafiri ni shida sana kwetu.

Inabidi upambane nao kibiashara.

Huko kwenye biashara ya usafirishaji si mnarogana kila kukicha? haya warogeni na Wachina.
 
Waje pia wawekeze kwenye sekta ya siasa, tuwe na raisi mchina labda mambo yataenda enda.
 
mi gari zangu za mombasa hazipatagi ajali mara kwa mara kama za huko moshi,mwanza,mbeya. mi naenjoy zangu ndani ya TAHMEED huku natafuna tambuu,parik,au manikchand hadi nafika mombasa halafu pemben yangu kuna toto chotara tunabadilishana mawazo,hizo ajali zinanichosha hata kufikiria kwenda mbeya kusalimia bibi na babu

Lipia tangazo.
 
Hayo ni majeneza yanayotembea,tokea lini mchina akaleta kitu bora Africa?

Wengi mnaochangia hapa hamjui tu mchina alivyo kimaslahi na roho mbaya.

Hayo mabasi yetu mnayoyaita ngarangara Mengi( 90%) ni Scania 94. Zimetengenezewa body na na Say Dar coach. Ubora wa kutosha miaka 5 na zaidi.

Hizi take away half price nzuri tu kwa sura . Impact kidogo tu nyanganyanga! Halafu hayana stability barabarani.
 
Ba Brio akili za mwafrika ni fupi sana. Wewe unachokiona ni athari za hili jambo huko mbeleni. In 5 to 10 years to come. Mtu mweusi anafikiria nauli ndogo ya leo, asifikirie huyu foreigner ana malengo gani baadae.
Marekani ambao ni waasisi wa free market trade wana restrictions kibao kwenye foreign investors. Hasa kwenye core sectors kama agriculture,power e.t.c. Mchina hajaja kukuza uchumi wa Tanzania, kaja kuchuma. Tofauti na mtanzania ambae akipata si rahisi kwenda kujenga kwingine.
Ni lazima tujifunze kujilinda na kulinda vya kwetu jamani. Tahadhari, sisemi tuwe violent au unfriendly against foreigners HAPANA ila tulinde vyetu. Hehehehe, watakuja kuwageuka hawa mshangae na roho zenu.
 
Last edited by a moderator:
Na kweli hatushindwi ! Lakini hatujafikia hapo na wala hatuwaxhukii watanzania kwa kiwango hicho!

Ila najiuliza, hivi nyie mnaosupport wachina ni watanzania Kweli?

Mkuu, hakuna mtu anayesupport Wachina, bali huduma wanayotoa ambayo nyie mmeshindwa kuitoa, wasafiri wanahitaji huduma nzuri ya usafiri ikiwa kutolundikwa katika mabasi kama mizigo, nyie wafanyabiashara ya usafiri watanzania mnaita basi first class kwa maana ya level seat, laikini njiani linaenda linaokota kama dala dala !!! Wakati huo huo mmepiga nauli juu. Halafu kumbuka kuwa sasa hivi ni soko huria, mtu anachagua kitu kinachomfaa katika bei ya ushindani, mnatakiwa mwende na wakati, dunia hairudi nyuma bali inaenda mbele, hakuna serikali itakayokuwa tayari kulinda huduma mbovu kwa wanachi wao, wachina wamechunguza mapungufu yenu, wakaona jinsi mnavyotoa huduma mbaya, wao wamefanyia kazi mapungufu yenu. Tena nitafurahi zaidi kama wataingia hata katika ufafiri wa Daladala ili kutuondolea matusi ya makonda wenu.
 
wakati sasa umefika wafanyabiashara wa Tanzania kufanya biashara kisasa na kitaalamu, tusikalie kulalamika tu, fanyeni utafiti wa biashara zenu, kabilianeni na ushindani kwa kuboresha huduma, ajirini watendaji wastaarabu sio wa kuokotaokota, boresheni customer care, thaminini wateja/abiria, jengeni ticketing viosk bora, matajiri tembeleeni sehemu ya biashara zenu kutathmini huduma zinazotolewa, boresheni magari, usafi, fuateni ratiba husika, acheni ushamba wa kizamani wa kupandisha nauli kipindi cha sikukuu, acheni kushiriki migomo isiyo na tija, naamini hata ukiwa na basi moja kabla ya miezi 12 utaongeza mengine kama sio lingine, hiyo ndio biashara huria.
 
Ba Brio akili za mwafrika ni fupi sana. Wewe unachokiona ni athari za hili jambo huko mbeleni. In 5 to 10 years to come. Mtu mweusi anafikiria nauli ndogo ya leo, asifikirie huyu foreigner ana malengo gani baadae.
Marekani ambao ni waasisi wa free market trade wana restrictions kibao kwenye foreign investors. Hasa kwenye core sectors kama agriculture,power e.t.c. Mchina hajaja kukuza uchumi wa Tanzania, kaja kuchuma. Tofauti na mtanzania ambae akipata si rahisi kwenda kujenga kwingine.
Ni lazima tujifunze kujilinda na kulinda vya kwetu jamani. Tahadhari, sisemi tuwe violent au unfriendly against foreigners HAPANA ila tulinde vyetu. Hehehehe, watakuja kuwageuka hawa mshangae na roho zenu.

Mkuu nakushukuru sana. At least kuna wachache kama wewe wenye passion na hii nchi yetu.
Hiyo nauli yenyewe tunayowazia tu difference ni buku au buku mbili. But long term impact kwa watanzania itakuwaje?

Who among us anafikiri mchina ana uchungu sana na maisha ya mtanzania kuliko mtanzania mwenzake?

Je tukishaquit sisi wazawa wakabaki waxhina kwenye industry si watafanya watakavyo? Kama mchina mmoja anaweza kununua basi 150 at once. Baada ya 5yrs wakiwepo wachina 10 je kuna mtanzania anayebaki kwenye hii industry? Piga picha patakuwaje !
 
Last edited by a moderator:
Ndio mambo ya soko huria hayo wacha mshindane tunachotaka ni Huduma bora.
 
nakubaliana na wewe,nilienda Tunduma Mchina ndiye kakamata route,lakini tukirudi nyuma kidogo sisi watanzania bado tuna biashara za ujanja ujana,nafikiri ni boro mchina aendelee kupewa nafasi kwa sababu sisi tumeshindwa,angalia mabasi ya mbeya dar yalivyo choka na kuzeeka lakini basi linalazimishwa hivyo hivyo,acha wachina waendelee kuleta challenge kwenye hii sector ili waafrica ambao wapo tayari kwa challenge wabadilike na wale wa kujaribu jaribu watupwe nje ya game
 
Ba Brio

Bora wachina mara mia, kwasababu mabasi yao ni bora, yana kiyoyozi, bei nafuuu na hawachinji kutoa makafara kama ninyi wabongo na mibasi yenu takataka mliyotengeneza bodi kenya. mmetunyanyasa vya kutosha na kwa miaka mingi sana mkipandisha bei mpendavyo, soko huria linaendelea itafika kipindi mtapaki hayo mangarangara yenu garage.

sisi abiria tunachohitaji sio basi la mtanzania, tunachohitaji ni usafiri bora, hatujali ni wa mtz au mchina au mzungu, na hata wewe ukipata hela yako mimi hainihusu ni yako wewe na watoto wako hivyo niko radhi hata kuungana na mchina ili basi lako life kama kutakuwa na maslahi. kwendeni zenu huko chinjachinja ninyi. mlizoea biashara za mabasi kwa uchawi mchina amekuja kufanya biashara kwa kutumia akili, au naye kawazidi nguvu kwa dini yake ya Confucianism?

Well said mkuu
Mangarangara tupa kule
 
Last edited by a moderator:
Mkuu chunguza kidogo tu uambiwe kitu wanafanywa hao makonda nanmadereva wa mabasi au malori ya wachina! Ulizia kesi zilizopo ubungo au urafiki polisi.

Kwa taarifa tu ni kuwa nauli kupanda December hata mmiliki hanufaiki. Wananufaika tu mawakala wa usafirishaji. Wala Taboa wala mmiliki hanufaiki! Ni uzembe wa hiihii serikali.

Kwa nini nyie mnaweka hao mawakala, mbona msikatishe ticket wenyewe, manawauzia mawakala ticket zote halafu mnarudi kulala nyumbani na nyumba ndogo zenu !!! Mtu akija ofisi kwenu anaambiwa ticket zimeisha akienda kwa wakala anazikuta tena anauziwa kwa bei ya juu, kwa kuwa ana shida ya kusafiri ananunua hivyo hivyo !!! Ngoja mnyooshwe mpaka mtakapoenda shule kusoma soma la huduma kwa mteja, na bado msipobadilika na kusimamia biashara zenu nyie wenyewe, mtaondolewa barabarani.
 
Umenisaidia kufahamu kuwa bado kuna usafiri mzuri na salama. Nakumbuka niliwahi kupanda hilo la Mchina, Yutong, safari ilikuwa nzuri na salama, na kushuhudia mabasi kibao yana-overtake kwa kasi mlima Kitonga bila kuona mbele kuna gari au la.

Bora kuendelea kuishi, na Mchina kupata fedha yangu kuliko kupoteza maisha, kwa kumpa fedha mtanzania hasiyejali utu wa mwenzie; na ambaye hafikiri vizuri kuwa akinichinja leo, kesho atapataje hiyo pesa kutoka kwangu tena.
 
Hawaiwezi biashara ya mabasi, watakimbia wenyewe
 
Back
Top Bottom