Wachina kuvamia usafirishaji ni Halali?

Wachina kuvamia usafirishaji ni Halali?

Soko huria acheni kulalamika toa huduma Bora utapata
 
Tanzania ndiyo sehemu ya kuchumia mali na kuendeleza nchi zao, inauma sana hawa watu wanapoivamia nchi na kugandamiza wazawa, ila swali je wasipofanya hizo nyie watanzania ktk sekta hiyo mtatuhakikishia tunapata huduma nzuri ya usafirishaji ktk nyanja zote? sio kesho tunaanza kusumbuka na magari mabovu, oh mara sijui nini?, ni lazima muwe vizuri sana maana hiyo sekta ni muhimu sana.

Pili ni suala la kodi, mkuu hao wachina wanalipaje kodi? je kodi yao ni sawa na mtanzania au? na kama itakua wanalipa kodi ya juu zaidi je kodi hiyo inatunufaisha wananchi? kama inatunufaisha vya kutosha wananchi, basi sio mbaya wakiendelea ila tu wasiwe huru kupita kiasi waweke sheria zitakazowapa limitation.

Je hao wachina wamewaajiri wachina wenzio au watanzania? ktk hizo ofisi zao, madereva, konda nk; ni wachina tu au? kama si wachina pekee, basi kuna namba kubwa ya watanzania wamepata ajira hapo, je ikitokea hawapo hali ya ajira na maisha ya watu itakuwaje? zingatia tatizo la ajira lilivyo!.

Hawa watu japo ndio hivyo ila pia zipo faida nyingi tunazipata toka kwao pia, Viongozi wetu waweke sheria zitakazo wapa mipaka kwa kuzingatia maslahi ya biashara ya ndani, pia maoni ya watanzania, lakini pia wasifanywe kama miungu sana eti kwasababu tu sisi tu maskini, no hata wao wapo kifaida yao zaidi ktk kuendeleza unyonyaji. wao.

Nb: sijawatetea ila pia sijataka kuwaponda moja kwa moja. mimi naona hivyo.

Madereva wako kwenye mgomo, mchina amekopa bank sasa atalipaje mkopo, inabidi yeye na mwanae na shemeji yake wakae kwenye usukani wapige kazi, Hebu tujiulize wabunge wanapewa mishahara na posho za madereva wao, lakini haohao kwanza wanaendesha wenyewe wanapeleka mikataba hewa ya madereva kwa spika. Yule mbuge pamoja na kuwa na mguu mmoja lakini alikomalia kuendesha mwenyewe hadi akatumbukia mtaroni yumo tu, nawengine wanaendeshwa na mahawara zao ili mradi shilingi isidodoke chini,

kama kweli tunataka uzalendo tuwaulize wabunge wamekosesha ajira watanzania wangapi kwa kujiendesha wenyewe ili hali wanapewa pesa za mishahara ya madereva wao.
 
Kwa nini nyie mnaweka hao mawakala, mbona msikatishe ticket wenyewe, manawauzia mawakala ticket zote halafu mnarudi kulala nyumbani na nyumba ndogo zenu !!! Mtu akija ofisi kwenu anaambiwa ticket zimeisha akienda kwa wakala anazikuta tena anauziwa kwa bei ya juu, kwa kuwa ana shida ya kusafiri ananunua hivyo hivyo !!! Ngoja mnyooshwe mpaka mtakapoenda shule kusoma soma la huduma kwa mteja, na bado msipobadilika na kusimamia biashara zenu nyie wenyewe, mtaondolewa barabarani.

Shida ninayopata na nyie ni white collars ! Hamna uelewa mpana wa huku uswazi tuliko sisi.
Kwa taarifa yako...
1. ukinunua basi leo... lazima utapakiliwa na agent. Taka usitake.
2. Ukinunua lori leo...lazima utapakiliwa mzigo na dalali.. taka usitake... labda uwe na mizigo binafsi.
3. Ukinunua mazao mkoani ukileta hapa dar... lazima uuziwe na dalali...taka usitake.
4......... na mengine mengi....
Dont ask me why!
Hata huyu mchina anakatiwa tickets na mawakala.
 
Mleta mada hii vp unaogopa ushindani na hao wavimba macho (wachina) mpambane nao tu
Acheni kulalamika kwani huu syo muda wake
 
Hayo ni majeneza yanayotembea,tokea lini mchina akaleta kitu bora Africa?

Kwa taarifa yako 95% ya mabasi yanayopiga mweleka ni scania, na matairi yanayoongoza kupasuka ni michelin na bridgestone ambayo hayatengenezwi china.
 
Mleta mada hii vp unaogopa ushindani na hao wavimba macho (wachina) mpambane nao tu
Acheni kulalamika kwani huu syo muda wake

Uuuuuiiii.... mkuu ushindani hauwezekani bila governor kutoka serikalini. Level mbili tofauti sanaaaa.... sisi wa gari 5 na wa gari 150 tushindane kivipi? Wao wana access to capital..sisi je?

Wewe mwenyewe hapo kila siku unatamani upate mkopo ujikwamue lkn huna vigezo. Ndiyo tz yetu. Imebaki kulilia serikali tu.

Stop pretending guys. Dont take it so lightly, tutamalizwa. Hali ni mbaya... twaelekea pabaya...
 
Madereva wako kwenye mgomo, mchina amekopa bank sasa atalipaje mkopo, inabidi yeye na mwanae na shemeji yake wakae kwenye usukani wapige kazi, Hebu tujiulize wabunge wanapewa mishahara na posho za madereva wao, lakini haohao kwanza wanaendesha wenyewe wanapeleka mikataba hewa ya madereva kwa spika. Yule mbuge pamoja na kuwa na mguu mmoja lakini alikomalia kuendesha mwenyewe hadi akatumbukia mtaroni yumo tu, nawengine wanaendeshwa na mahawara zao ili mradi shilingi isidodoke chini,

kama kweli tunataka uzalendo tuwaulize wabunge wamekosesha ajira watanzania wangapi kwa kujiendesha wenyewe ili hali wanapewa pesa za mishahara ya madereva wao.

Tz ina debate si mchezo!
 
ndugu unahisi ukiwa china haki yako itakuwa sawa na yule raia wa kichina? cha msingi ni serikali ingeweka regulations zitakazo saidia kukawa na wawekezaji watakaotoa usafiri bora na nafuu na muda huohuo ikilinda maslahi ya local investors, itakuwa ni uwendawazimu kufurahia mabasi mazuri na wakati huohuo watanzania wakipotezwa kwenye ramani ya biashara, hata nchi kama marekani licha ya ubepari uliokubuhu inayosera ya kulinda wawekezaji wazawa.

Asante mkuu.... please guys lets take this direction . Huu ndio uzalendo. Tujifikirie kwa mapana zaidi.
 
Asante mleta mada kwa hii thread. Basically umetuonyesha upande wa pili wa wawekezaji wetu wakibongo ambao ni uwoga wa free market na kukumbatia failures za sera ya ujamaa kutaka serikali ikukinge kila makhali.


Vitu viwili nataka kuchangia hapa:


1. Badala ya kulalamika kwamba mchina anashusha bei which is typical one of the marketing strategy market penetration…ofcoz kama hiyo bei ni hasara hawezi kuendelea kwa bei hiyo…..na kama hiyo bei ni reasonable kwenye hii biashara ili nyinyi mmbaki sokoni inabidi mumfuate kwakushusha bei au kuborehsa vitu vingne mfano - huduma nzuri.


2. Naona Xenophobia: ii mambo South Africa ilianza hivi hivi badala ya kufikiria jinsigani utashndana kwenye biashara unafikiria jinsi ya kumfukuza huyu mwekezaji nchini ili wewe with your poor business strategies uendelee kutunyanyasa sisi abiria which is very pathetic of you.


Ushauri wangu usikimbie kwenda kupaki basi nyumbani fikiria namna yakushindana kwenye hili soko. There are millions ways…


Same applies kwa wale wakarikaoo wanalalimika mchina anachukua fremu kariakoo…tubadilike tuwe kiushndani
 
Pole Ba Brio; watanzania ni wakiwa; yatima na wajane; hatuna chombo cha kutupigania; hapa tumebaki "kila mtu na lwake"; kuanzia ajira za kawaida mpaka uwekezaji; serikali haitusiidii ipasavyo sana sana ni kutoa kauli na ahadi hewa na tata tu! imagine serikali iliyofilisika kifedha; wabunge hawalipwi posho zao; shule zinafungwa kwa kukosa chakula lakini serikali inaweza kutoa kauli kwamba pesa za Escrow sio mali yake! serikali inashindwa kusimamia ajira za madreva; yakilipuka inaunda tume ili kupoteza muda; Ni upepo utapita tu! wakubwa na wenye ukwasi wananyangaya raia ardhi yao na serikali inakaa kimya; William Lukuvi halali sasa hivi anahangaika na matatizo ya ardhi utadhani nchi imepta uhuru leo hatukuwa na serikali ya wananchi! madini yanaporwa kushoto na kulia serikali iko kimya; wafanya biashara wakubwa hawatozwi kodi; mhanga ni Mama lishe na machinga; kuna msitu Mgololo unazalisha nguzo za umeme; zinauzwa nchi jirani kisha tunaziagiza kwa fedha za kigeni kuzirudisha nchini?! Ba Brio; kwa kuwa wewe umeshtuka mapema; anza kuandaa mkakati wa pili wa kutokea; inaitwa plan B au fall back position.
 
Shida ninayopata na nyie ni white collars ! Hamna uelewa mpana wa huku uswazi tuliko sisi.
Kwa taarifa yako...
1. ukinunua basi leo... lazima utapakiliwa na agent. Taka usitake.
2. Ukinunua lori leo...lazima utapakiliwa mzigo na dalali.. taka usitake... labda uwe na mizigo binafsi.
3. Ukinunua mazao mkoani ukileta hapa dar... lazima uuziwe na dalali...taka usitake.
4......... na mengine mengi....
Dont ask me why!
Hata huyu mchina anakatiwa tickets na mawakala.

Mlishawahi kufikiria kuondoa hiyo hali ? Kwa sababu hao ndo wanapandisha bei ili wapate cha kwao !! Udalali kialsehemu, eti mtu ukienda kununua matunda Buguruni unauziwa na dalali ilhali mwenye machungwa kasimama hapo hapo, ukienda Karume kumnunulia mtoto viatu vya shule ndo utakoma zaidi, mwenye kuuza viatu yupo, lakini nakuachia unapigwa bei na dalali !!!! Yaani nyie, acha tu muendelee kukaribisha udalali kwa kila kitu. Kwani ukinunu gari, ufungue ofisi na kuwaajiri watu mwnyewe na usitoe ticket zako kwa mtu mwingine huwezi kupakia ? Naomba ufafanuzi kwa kuwa fani yangu sio hiyo.
 
Uuuuuiiii.... mkuu ushindani hauwezekani bila governor kutoka serikalini. Level mbili tofauti sanaaaa.... sisi wa gari 5 na wa gari 150 tushindane kivipi? Wao wana access to capital..sisi je?

Wewe mwenyewe hapo kila siku unatamani upate mkopo ujikwamue lkn huna vigezo. Ndiyo tz yetu. Imebaki kulilia serikali tu.

Stop pretending guys. Dont take it so lightly, tutamalizwa. Hali ni mbaya... twaelekea pabaya...

Nyie Mmekuwa Ktk sector hyo kwa muda mrefu na nyie kutwa Mmekuwa mkimkandamiza abiria kwa nauli etc, sisi wote tunapenda kuona makampuni ya watanzania wazawa yakifanya vizuri Ktk biashara
Elewa tu hao wawekezaji walichoona mapungufu Ktk upande wenu wao wakaja na style tofauti ili kuboresha na wakamate soko
Kikubwa nyie acheni kulalamika komaeni tu nao
 
hawa jamaa wametunyanyasa sana, halafu huyo inaonekana sio mfanyabiashara mwenye akili ya biashara, ndio maana anaogopa ushindani. hao ndio wale wafanya biashara wa magari ambao wanategemea uchawi tu na kutoa makafara hawatumii akili ya biashara. mkipata hela muwe mnaenda hata semina za ujasiriamali walau kidogo ili muwe ana akili ya ushindani, machina akileta basi zuri wewe pia lete zuri na toa huduma bora uone.

kuna wabongo fulani wanayo mabasi yanaenda mbeya, inaitwa JM, wale waanatoza garama kubwa kuliko new force za wachina, lakini watu wanajaa lile bus. mabasi ya JM wanatoa lugha nzuri, wanajali sana abiria, wanaenda mwendo mzuri, ndani kusafi kila kitu kisafi lakini ni basi lilelile la kichina ambalo hata huyu jamaa anaweza kuwa nalo lakini ameweka vivutio vya kibiashara kuanzia customer care hadi mazingira na watu wanalipenda sana.

wewe pia weka vivutio vizuri, scandnavia zamani watu tulikuwa tunapanda tu kwasababu wanaenda mwendo safi na wanagawa soda...hahaha, kumbe ile soda imewekwa kwenye nauli mlemle. ndio maana huwa nasema bora mataifa mengine yaje tz yachangamshe watu kama huyu jamaa wanaotaka ufanya biashara kama wako pemba, kwao mteja sio mfalme na wakipata nafasi ya kupandisha nauli wanapandisha bila huruma. hawajui kuwa abiria wanaopanda asilimia 90 ni masikini kuliko wao.

Mkuu uko mle mle naona umempasha vizuri, uzalendo kwake ni kututoza nauli kubwa na kuweka magari mabovu barabarani
 
Tz ina debate si mchezo!

I tell you....tuna debate za msingi sana lakini huwezi amini kuna watu wanakula mishahara humu mitandaoni kazi yao ni kuharibu debate zote zenye maslahi ya kitaifa zisishike hatamu .

Hawataki kabisa watu wajadili maslahi mapana ya taifa ili tu kuficha madhaifu ya serikali.

Ukigusa tu wamerukia na kupotosha. Hata wale great thinkers wa ukweli wanapotezwa uelekeo na hawa waajiriwa maalum.

Hata ungeleta jambo zuri aje hata lihusu maslahi yake na familia yake tu... hawez support maana yuko kazini!

Inasikitisha sana.
 
ndg zangu naombeni kuhoji kupitia jamvi hili ili na nyie mnisaidie

mimi ni mdau wa biashara ya usafirishaji kwa njia ya barabara.

Tumevamiwa na tena tunakandamizwa hatupumui hata kidogo na hawa wawekezaji wapya wachina.

Nikizungumzia mabasi, leo hii kuna wachina wanapeleka mabasi route zote kutoka dar. Na wako radhi kupakia abiria kwa bei wanayopenda wao, na kuondoa gari na abiria hata watano.

Ikumbukwe hao wachina ndio mawakala wa mabasi ya yutong na zhongton ambayo yako kwenye chart sasa.

Je isingekuwa vyema kwa hawa wachina kuwa restricted kwenye kutuuzia tu mabasi na sisi tufanye biashara ya usafiri?

Kumbuka mchina mmoja ana mabasi zaidi ya 150.
Wale watanzania tunaojenga uwezo na vibasi vyetu viwili, vinne hadi kumi je tuta-survive?

Kwa uelewa wa kawaida pale ubungo kwa siku yanatoka mabasi yasiyopungua 200. Katika hayo wamiliki ni zaidi ya 100. Maana yake ni kwamba uchumi umesambaa mikononi mwetu wenyewe. Je tukimwacha mchina atoe mabasi 50 peke yake akaja ma mchina mwingine tena, wamiliki watanzania tutapona? Mbaya zaidi ni kuwa mchina anaweza kuweka basi mpya kila mwezi, sisi tunaweza?

Kwa wale msiofahamu, wachina wanauza mabasi ambayo wameshatumia yenye namba b na c yote kwa bei punguzo. Na mimi nimenunua hapo kadhaa. Lengo lao ni kuhakikisha wanaendesha mapya kila wakati na sisi yetu yanaendeshwa miaka mitano. Ndiyo uwezo wetu kitanzania.

Hawa wenzetu wana access to capital huko kwao. Sisi kama yatima tunapambana tangu mavumbini hadi tulipopata cent ya kununua kamoja. Je ni halali kutufutilia mbali kwa namna hii?

Hii sera yetu ikoje? Serikali iko wapi? Mbona mnatufanya kitu mbaya hivi?

Kwenye malori hali ndiyo mbaya zaidi. Inaogopesha mno. Kuna kampuni 4 za wachina kila moja ina zaidi ya malori 400. Wanaenda mipaka yote ya nchi kwa bei punguzo.
Halafu hao hao wachina wamenunua kampuni za clearing. Kwa hiyo wanatoa mizigo wenyewe na wanagawana wenyewe. Ukifanya sensa ya watanzania wenye gari moja hadi 20 ni wengi mno tumetapakaa nchi nzima na uchumi unasambaa. Je huyu mchina akichuma hapa anatuachia nini sisi wa matombo, ileje,masasi,na kwingineko nchini? Kodi zenyewe hawalipi wanaingiza magari kwa msamaha wa kodi. Huu usingizi wa serikali utaisha lini jamani???

Ziko bank za kitanzania nazifahamu zimekopesha wachina malori yasiyohesabika. Leo hii wewe mtanzania ukitaka moja process itachukua miezi sita na unakata tamaa hata hulipati.... ! Agha! Basi bana siendelei .... 😡



mh waziri husika.kamahiki uppo.embutuongezee hawa wachina wameleta heshimana adabu kwamijitanzania. Isiojali utu wabndamu nawapenda sana naukitaka kujua tofautuyaonayetu wanambebea mteja. Mpakandani. Akiwana. Mzigomkubwa namtoto wanabeba kamaumekuja. Nae hawa mahathini wakikupa tkt aunathamani tena usubiri ajali

madereva wa wachina wana adabu garizao zimefungwa kitu ata wawewapi wakisahau kufunga et mkanda tu dereva akirudi ajenamaelezo... Kwenyemalori mungu awatienguvu zaidi tukishazoeakupeleka mizigo kamkoakadogo mil 3mbaya auko pekee
 
Tatizo magari mabovu,machafu,yana mende na kunguni baadhi yao, huduma na kauli chafu hasa za makondakta wenu ndo mana mtashindwa bihashara hii.
Mfano kuna dada alikata tiketi basi ya Zuberi-mwanza,kachelewa kufika na alikuwa na mtoto,kakuta basi alilokata tiketi limeondoka,kakuta la pili ndo linatoka kalifukuzia na pikipiki mpaka mbezi,kapanda bila huruma na mtoto konda kamshusha eti subirie basi lake liko nyuma kumbe ni uhongo,dada kashuka kaachwa hapo gari hakuna,huruma ya mtoto nikampa hifadh home wala simjui,kwenda ubungo wanadai eti aongeze elfu kumi ya usumbufu.P.mb.afu zenu, ata wakibaki WACHINA barabarani poa tu nyinyi huruma hamna.
 
wengi mnaopingana na mleta mada ni wale mnaotegemea monthly salary hakuna anayejua reality ya mazingira ya biashara ya tanzania, mengi mnayoyasikia kwenye media na matangazo ya serikali sio yanayofanyika, huku ni akili kichwani na magumashi nyingine nyingi, na anapotokea foreign investor serikali humchukulia ndio first priority na favour zote wanapewa wao, ndio maana locals wanaonekana ni matapeli tu!
sasa kama reality ya biashara watu hawaijui, mbona mchina ameweza na ninyi mnashindwa? au kwasababu ana vimacho vidogo na ni mweupe?

kama mna akili kwanini msijikusanye kikundi mnunue mabasi mengi kuliko mchina mfanye ushindani mzuri? au kwasababu ninyi ni maajenti wa mashetani kumwaga damu za watu? mna pesa kama wakinga lakini analala chini kwasababu akilala kwenye kitanda mganga kamkataza? akili zenu hazijakaa kijasiriamali ndio maana mnaogopa ushindani. mtanyooka mwaka huu.

au basi unganeni na mchina, if you cannot defeat them why can't you join them? au unakuja hapa kulialia ukitaka tukuonee huruma wakati najua mwezi wa kumi na mbili xmass nikitaka kwenda kuhesabiwa lazima nilipe nauli kwenu mara mbili.....
 
Hayo ni majeneza yanayotembea,tokea lini mchina akaleta kitu bora Africa?
hata wewe mwenyewe ni jeneza linalotembea kwasababu mwili wako umejaa vitu vya kichina vitupu kuanzia nywele, heleni, makalio, nguo, viatu kila kitu hadi vyakula vipo vingine unakula vya kichina. mbona bado unaishi sasa
 
wengi mnaopingana na mleta mada ni wale mnaotegemea monthly salary hakuna anayejua reality ya mazingira ya biashara ya tanzania, mengi mnayoyasikia kwenye media na matangazo ya serikali sio yanayofanyika, huku ni akili kichwani na magumashi nyingine nyingi, na anapotokea foreign investor serikali humchukulia ndio first priority na favour zote wanapewa wao, ndio maana locals wanaonekana ni matapeli tu!

Kayaman asante .....
Watu wanasahau huyu mchina yeye ana msamaha wa kodi... kwa hilo tu ..the moment anaweka gari barabarani tayari ana unafuu mkubwa sana.... sisi wavuja jasho tutashindanaje nao?

Shida yetu ni mazingira yaliyojengwa na serikali kuwajali wawekezaji bila mipaka na kutusahau sisi wazawa tuliohangaika na hili taifa tangu uhuru hadi leo.
Tumewavusha wakati wote barabara zikiwa vumbi hadi leo kuna unafuu.

Je hizo youtong zingewapeleka mwanza enzi zile tunapiga shimo mwanzo mwisho siku tatu? Tulivumilia tukawafikisha watanzania wenzetu. Tulindwe basi twende na moderate speed kukua kufikia huko waliko wenzetu.

Mtaji wa ghafla hivyo kwa Tz hii tutapata wapi?
 
Back
Top Bottom