Wachina kuvamia usafirishaji ni Halali?

Wachina kuvamia usafirishaji ni Halali?

Ba Brio

Member
Joined
Mar 19, 2012
Posts
78
Reaction score
37
Ndg zangu naombeni kuhoji kupitia jamvi hili ili na nyie mnisaidie

Mimi ni mdau wa biashara ya usafirishaji kwa njia ya barabara.

Tumevamiwa na tena tunakandamizwa hatupumui hata kidogo na hawa wawekezaji wapya WACHINA.

Nikizungumzia mabasi, leo hii kuna wachina wanapeleka mabasi route zote kutoka Dar. Na wako radhi kupakia abiria kwa bei wanayopenda wao, na kuondoa gari na abiria hata watano.

Ikumbukwe hao wachina ndio mawakala wa mabasi ya Yutong na Zhongton ambayo yako kwenye chart sasa.

Je isingekuwa vyema kwa hawa wachina kuwa restricted kwenye kutuuzia tu mabasi na sisi tufanye biashara ya usafiri?

Kumbuka mchina mmoja ana mabasi zaidi ya 150.
Wale watanzania tunaojenga uwezo na vibasi vyetu viwili, vinne hadi kumi je tuta-survive?

Kwa uelewa wa kawaida pale ubungo kwa siku yanatoka mabasi yasiyopungua 200. Katika hayo wamiliki ni zaidi ya 100. Maana yake ni kwamba uchumi umesambaa mikononi mwetu wenyewe. Je tukimwacha mchina atoe mabasi 50 peke yake akaja ma mchina mwingine tena, wamiliki watanzania tutapona? Mbaya zaidi ni kuwa mchina anaweza kuweka basi mpya kila mwezi, sisi tunaweza?

Kwa wale msiofahamu, wachina wanauza mabasi ambayo wameshatumia yenye namba B na C yote kwa bei punguzo. Na mimi nimenunua hapo kadhaa. Lengo lao ni kuhakikisha wanaendesha mapya kila wakati na sisi yetu yanaendeshwa miaka mitano. Ndiyo uwezo wetu kitanzania.

Hawa wenzetu wana access to capital huko kwao. Sisi kama yatima tunapambana tangu mavumbini hadi tulipopata cent ya kununua kamoja. Je ni halali kutufutilia mbali kwa namna hii?

Hii sera yetu ikoje? Serikali iko wapi? Mbona mnatufanya kitu mbaya hivi?

Kwenye Malori hali ndiyo mbaya zaidi. Inaogopesha mno. Kuna kampuni 4 za wachina kila moja ina zaidi ya malori 400. Wanaenda mipaka yote ya nchi kwa bei punguzo.
Halafu hao hao wachina wamenunua kampuni za clearing. Kwa hiyo wanatoa mizigo wenyewe na wanagawana wenyewe. Ukifanya sensa ya watanzania wenye gari moja hadi 20 ni wengi mno tumetapakaa nchi nzima na uchumi unasambaa. Je huyu mchina akichuma hapa anatuachia nini sisi wa matombo, ileje,masasi,na kwingineko nchini? Kodi zenyewe hawalipi wanaingiza magari kwa msamaha wa kodi. Huu usingizi wa serikali utaisha lini jamani???

Ziko bank za kitanzania nazifahamu zimekopesha wachina malori yasiyohesabika. Leo hii wewe mtanzania ukitaka moja process itachukua miezi sita na unakata tamaa hata hulipati.... ! Agha! Basi bana siendelei .... 😡
 
Ba Brio

Bora wachina mara mia, kwasababu mabasi yao ni bora, yana kiyoyozi, bei nafuuu na hawachinji kutoa makafara kama ninyi wabongo na mibasi yenu takataka mliyotengeneza bodi kenya. mmetunyanyasa vya kutosha na kwa miaka mingi sana mkipandisha bei mpendavyo, soko huria linaendelea itafika kipindi mtapaki hayo mangarangara yenu garage.

sisi abiria tunachohitaji sio basi la mtanzania, tunachohitaji ni usafiri bora, hatujali ni wa mtz au mchina au mzungu, na hata wewe ukipata hela yako mimi hainihusu ni yako wewe na watoto wako hivyo niko radhi hata kuungana na mchina ili basi lako life kama kutakuwa na maslahi. kwendeni zenu huko chinjachinja ninyi. mlizoea biashara za mabasi kwa uchawi mchina amekuja kufanya biashara kwa kutumia akili, au naye kawazidi nguvu kwa dini yake ya Confucianism?
 
Last edited by a moderator:
Hute#
Uzalendo umekutoka kabisa. Hizo ajali zinasababishwa na vichochoro vya nchi hii. Hiyo imani ya kafara unayo wewe! Hujui tu ni kwa kiasi gani unanufaika na uchumi kurudi mikononi mwetu wenyewe.
Nikukumbushe tu kabla ya wachagga kushika hatamu kwenye maduka walikuwepo wahindi tu kwenye biashara zote. Kariakoo kiatu kilikuwa hakishikiki, nguo balaa. Mhindi alikuwa hana lugha mbili.
Na magofu yalijaa miji yote.
Leo hii maduka yanamilikiwa na watanzania kwa kiasi kikubwa.... unaona miji inavyopendeza? Magofu yameisha kariakoo. Hata kule mkoani kwako bobobo kuna ghorofa zimejengwa na wafanyabiashara wazawa.

Tahadhari, wachona nao wamevamia tena biashara ya maduka! Endelea kuwasifia. Utawaona hapo ofisini kwako wanafanya kazi ya cashier.
TRA tayari wameingia... ndiyo systems administrators (Tancis)

Guys tuache ushabiki, back to our senses, tuzungumze hawa mchwa wawekewe ukomo. Watatumalizaaaa
 
Last edited by a moderator:
chonde chonde msiwafanyie hujuma ya ajari huko barabarani ili kuwaharibia soko...
 
Tatizo sio mchina kaka, tatizo lipo kwenu wabongo. Wewe umechanganya Maelezo. Lalamiko lako kuu ni wachina. Ila si kweli una mtaji mdogo kaka, jipange. Tena wachina wameongeza ajira kwa Ndugu zetu, pili wameraishisha usafiri. Tatu bei imepungua kwani mabasi yapo mengi. Mlitaka muendelee kutunyanyasa. Kaka si lazima ufanye biashara hiyo zipo nyingine pia. Asanteni wachina
 
bora wachina mara mia, kwasababu mabasi yao ni bora, yana kiyoyozi, bei nafuuu na hawachinji kutoa makafara kama ninyi wabongo na mibasi yenu takataka mliyotengeneza bodi kenya. mmetunyanyasa vya kutosha na kwa miaka mingi sana mkipandisha bei mpendavyo, soko huria linaendelea itafika kipindi mtapaki hayo mangarangara yenu garage.

sisi abiria tunachohitaji sio basi la mtanzania, tunachohitaji ni usafiri bora, hatujali ni wa mtz au mchina au mzungu, na hata wewe ukipata hela yako mimi hainihusu ni yako wewe na watoto wako hivyo niko radhi hata kuungana na mchina ili basi lako life kama kutakuwa na maslahi. kwendeni zenu huko chinjachinja ninyi. mlizoea biashara za mabasi kwa uchawi mchina amekuja kufanya biashara kwa kutumia akili, au naye kawazidi nguvu kwa dini yake ya Confucianism?
Wewe jamaa ni taahirra. Umejitoa akil
 
Asante saint ivugha.
Sijui watu wanafikiriaje !
 
Last edited by a moderator:
Hute#
Uzalendo umekutoka kabisa. Hizo ajali zinasababishwa na vichochoro vya nchi hii. Hiyo imani ya kafara unayo wewe! Hujui tu ni kwa kiasi gani unanufaika na uchumi kurudi mikononi mwetu wenyewe.
Nikukumbushe tu kabla ya wachagga kushika hatamu kwenye maduka walikuwepo wahindi tu kwenye biashara zote. Kariakoo kiatu kilikuwa hakishikiki, nguo balaa. Mhindi alikuwa hana lugha mbili.
Na magofu yalijaa miji yote.
Leo hii maduka yanamilikiwa na watanzania kwa kiasi kikubwa.... unaona miji inavyopendeza? Magofu yameisha kariakoo. Hata kule mkoani kwako bobobo kuna ghorofa zimejengwa na wafanyabiashara wazawa.

Tahadhari, wachona nao wamevamia tena biashara ya maduka! Endelea kuwasifia. Utawaona hapo ofisini kwako wanafanya kazi ya cashier.
TRA tayari wameingia... ndiyo systems administrators (Tancis)

Guys tuache ushabiki, back to our senses, tuzungumze hawa mchwa wawekewe ukomo. Watatumalizaaaa
wewe mwenyewe sio mzalendo, mngekuwa wazalendo msingewanyanyasa abiria kwa bei mtakavyo. kumbuka mnachofanya siku za mwisho wa mwaka na sikukuuu. sisi wasafiri ndio tunaojua uchungu, wewe mwenye gari unayetaka tuwe wazalendo kwako tumefaidika nini toka kwako? kama usafiri hata mchina atatupatia, usijefikiri kuleta magari yenu mnatusaidia msaada. mbona maduka ya wachina bidhaa zao ni bei nafuu, hata tukijumua sisi wengine kwenye maduka ya jumla tunaona faida. kwenye biashara, wako
 
Mleta mada unanishangaza sana! Tena umesema wewe ni mdau wa usafirishaji. Unalalamika mchina kutoza nauli ndogo,ni soko huria mlivyokuwa mnachaji nauli kubwa mbona hukusikia kilio cha abiria?!

Pili unalalamika mchina anauza gari za zamani ili anunue mpya na bado wewe no mnunuzi! Sasa si uache kununua ukanunue mpya?! Hivyo wanavyofanya ndio inatakiwa sio mnakaa na mabasi mpaka yaue watu kwa ubovu.

Na kuhusu kuondoa basi na abiria watano tu hivyo ndivyo inavyotakiwa,kama unaendesha kampuni inavyotakiwa muda ukifika basi linatakiwa kuondoka hata likiwa na abiria mmoja au muombe umlipe apande basi lingine.

Naona hao wachina watawanyoosha sasa na msipoungana na kuwa professionals watawatoa barabarani.
 
Tanzania ndiyo sehemu ya kuchumia mali na kuendeleza nchi zao, inauma sana hawa watu wanapoivamia nchi na kugandamiza wazawa, ila swali je wasipofanya hizo nyie watanzania ktk sekta hiyo mtatuhakikishia tunapata huduma nzuri ya usafirishaji ktk nyanja zote? sio kesho tunaanza kusumbuka na magari mabovu, oh mara sijui nini?, ni lazima muwe vizuri sana maana hiyo sekta ni muhimu sana.

Pili ni suala la kodi, mkuu hao wachina wanalipaje kodi? je kodi yao ni sawa na mtanzania au? na kama itakua wanalipa kodi ya juu zaidi je kodi hiyo inatunufaisha wananchi? kama inatunufaisha vya kutosha wananchi, basi sio mbaya wakiendelea ila tu wasiwe huru kupita kiasi waweke sheria zitakazowapa limitation.

Je hao wachina wamewaajiri wachina wenzio au watanzania? ktk hizo ofisi zao, madereva, konda nk; ni wachina tu au? kama si wachina pekee, basi kuna namba kubwa ya watanzania wamepata ajira hapo, je ikitokea hawapo hali ya ajira na maisha ya watu itakuwaje? zingatia tatizo la ajira lilivyo!.

Hawa watu japo ndio hivyo ila pia zipo faida nyingi tunazipata toka kwao pia, Viongozi wetu waweke sheria zitakazo wapa mipaka kwa kuzingatia maslahi ya biashara ya ndani, pia maoni ya watanzania, lakini pia wasifanywe kama miungu sana eti kwasababu tu sisi tu maskini, no hata wao wapo kifaida yao zaidi ktk kuendeleza unyonyaji. wao.

Nb: sijawatetea ila pia sijataka kuwaponda moja kwa moja. mimi naona hivyo.
 
Hawashindwi hawa....

Na kweli hatushindwi ! Lakini hatujafikia hapo na wala hatuwaxhukii watanzania kwa kiwango hicho!

Ila najiuliza, hivi nyie mnaosupport wachina ni watanzania Kweli?
 
Mleta mada unanishangaza sana! Tena umesema wewe ni mdau wa usafirishaji. Unalalamika mchina kutoza nauli ndogo,ni soko huria mlivyokuwa mnachaji nauli kubwa mbona hukusikia kilio cha abiria?!

Pili unalalamika mchina anauza gari za zamani ili anunue mpya na bado wewe no mnunuzi! Sasa si uache kununua ukanunue mpya?! Hivyo wanavyofanya ndio inatakiwa sio mnakaa na mabasi mpaka yaue watu kwa ubovu.

Na kuhusu kuondoa basi na abiria watano tu hivyo ndivyo inavyotakiwa,kama unaendesha kampuni inavyotakiwa muda ukifika basi linatakiwa kuondoka hata likiwa na abiria mmoja au muombe umlipe apande basi lingine.

Naona hao wachina watawanyoosha sasa na msipoungana na kuwa professionals watawatoa barabarani.
hawa jamaa wametunyanyasa sana, halafu huyo inaonekana sio mfanyabiashara mwenye akili ya biashara, ndio maana anaogopa ushindani. hao ndio wale wafanya biashara wa magari ambao wanategemea uchawi tu na kutoa makafara hawatumii akili ya biashara. mkipata hela muwe mnaenda hata semina za ujasiriamali walau kidogo ili muwe ana akili ya ushindani, machina akileta basi zuri wewe pia lete zuri na toa huduma bora uone.

kuna wabongo fulani wanayo mabasi yanaenda mbeya, inaitwa JM, wale waanatoza garama kubwa kuliko new force za wachina, lakini watu wanajaa lile bus. mabasi ya JM wanatoa lugha nzuri, wanajali sana abiria, wanaenda mwendo mzuri, ndani kusafi kila kitu kisafi lakini ni basi lilelile la kichina ambalo hata huyu jamaa anaweza kuwa nalo lakini ameweka vivutio vya kibiashara kuanzia customer care hadi mazingira na watu wanalipenda sana.

wewe pia weka vivutio vizuri, scandnavia zamani watu tulikuwa tunapanda tu kwasababu wanaenda mwendo safi na wanagawa soda...hahaha, kumbe ile soda imewekwa kwenye nauli mlemle. ndio maana huwa nasema bora mataifa mengine yaje tz yachangamshe watu kama huyu jamaa wanaotaka ufanya biashara kama wako pemba, kwao mteja sio mfalme na wakipata nafasi ya kupandisha nauli wanapandisha bila huruma. hawajui kuwa abiria wanaopanda asilimia 90 ni masikini kuliko wao.
 
Na kweli hatushindwi ! Lakini hatujafikia hapo na wala hatuwaxhukii watanzania kwa kiwango hicho!

Ila najiuliza, hivi nyie mnaosupport wachina ni watanzania Kweli?

Si support wachina. Na support fair trade,kwa wafanyabiashara na wateja! Wachina,wahindi,waarabu etc wote wanahaki kufanyabiashara nchi hii. Kama wangekuwa wanafanya kitu illegally ningeku support we we,lakini kuwa na mtaji mkubwa sio kosa lao.

Unganeni la sivyo watawatoa barabarani.
 
Na kweli hatushindwi ! Lakini hatujafikia hapo na wala hatuwaxhukii watanzania kwa kiwango hicho!

Ila najiuliza, hivi nyie mnaosupport wachina ni watanzania Kweli?
hivi wakati ule ninyi mnapopandisha nauli wakati wa xmass huwa mnafikiria wagonjwa, watu wanaosafiri kwenda kuona wagonjwa, misiba na mwingien kakopa nauli? huwa mnakuwa wazalendo kweli, nini huwa mnakuwa watz? hakuna watu wabaya kama TABOA hao wamiliki, kwanza mnawanyonya sana madereva wenu wanapata stress hadi wanadondosha magari, dereva akipata ajali akifa familia zao hamzijali, ninyi mnajali pesa tu. unafikiri ninyi ndio wazalendo? ninyi ndio mashetani wa nchi hii. bora wachina waje.
 
Back
Top Bottom