lugoda12
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 313
- 647
Jamani naomba kuuliza maswali kidogo!
Hivi ni nani ambaye anahusika kuwapangisha au kuwauzia Wachina katika maeneo ya akiba ya barabara ya Morogoro Road jijini Dar es Salaam baada ya bomoa bomoa ya 2019 kuanzia Kimara hadi Mbezi Louis?
Je, Serikali inatambua uvamizi huo wa Wachina na inanufaika vipi au ni pesa ambazo zinaishia katika mifuko ya watu wachache?
Ikumbukwe maeneo hayo yalikuwa yanatumika na Watanzania ambao waliweka bidhaa mbalimbali kama mama lishe, car wash bubu na wengine kutunzia maua ya gadeni ili kujipatia kipato cha kila siku. Hadi sasa watu hao wamefukuzwa kibabe bila fidia ili kuwapisha Wachina.
Je, Serikali hili suala linalichukuliaje?