acha zako mkuu,nyie wabongo tatizo lenu munataka faida mara tatu,huduma zenu mbovu jeuri mumejaa ninyi,hamutaki kushusha nauli hata mafuta yashuke vipi,bora hao wachina wana wasikilza raiaNdg zangu naombeni kuhoji kupitia jamvi hili ili na nyie mnisaidie
Mimi ni mdau wa biashara ya usafirishaji kwa njia ya barabara.
Tumevamiwa na tena tunakandamizwa hatupumui hata kidogo na hawa wawekezaji wapya WACHINA.
Nikizungumzia mabasi, leo hii kuna wachina wanapeleka mabasi route zote kutoka Dar. Na wako radhi kupakia abiria kwa bei wanayopenda wao, na kuondoa gari na abiria hata watano.
Ikumbukwe hao wachina ndio mawakala wa mabasi ya Yutong na Zhongton ambayo yako kwenye chart sasa.
Je isingekuwa vyema kwa hawa wachina kuwa restricted kwenye kutuuzia tu mabasi na sisi tufanye biashara ya usafiri?
Kumbuka mchina mmoja ana mabasi zaidi ya 150.
Wale watanzania tunaojenga uwezo na vibasi vyetu viwili, vinne hadi kumi je tuta-survive?
Kwa uelewa wa kawaida pale ubungo kwa siku yanatoka mabasi yasiyopungua 200. Katika hayo wamiliki ni zaidi ya 100. Maana yake ni kwamba uchumi umesambaa mikononi mwetu wenyewe. Je tukimwacha mchina atoe mabasi 50 peke yake akaja ma mchina mwingine tena, wamiliki watanzania tutapona? Mbaya zaidi ni kuwa mchina anaweza kuweka basi mpya kila mwezi, sisi tunaweza?
Kwa wale msiofahamu, wachina wanauza mabasi ambayo wameshatumia yenye namba B na C yote kwa bei punguzo. Na mimi nimenunua hapo kadhaa. Lengo lao ni kuhakikisha wanaendesha mapya kila wakati na sisi yetu yanaendeshwa miaka mitano. Ndiyo uwezo wetu kitanzania.
Hawa wenzetu wana access to capital huko kwao. Sisi kama yatima tunapambana tangu mavumbini hadi tulipopata cent ya kununua kamoja. Je ni halali kutufutilia mbali kwa namna hii?
Hii sera yetu ikoje? Serikali iko wapi? Mbona mnatufanya kitu mbaya hivi?
Kwenye Malori hali ndiyo mbaya zaidi. Inaogopesha mno. Kuna kampuni 4 za wachina kila moja ina zaidi ya malori 400. Wanaenda mipaka yote ya nchi kwa bei punguzo.
Halafu hao hao wachina wamenunua kampuni za clearing. Kwa hiyo wanatoa mizigo wenyewe na wanagawana wenyewe. Ukifanya sensa ya watanzania wenye gari moja hadi 20 ni wengi mno tumetapakaa nchi nzima na uchumi unasambaa. Je huyu mchina akichuma hapa anatuachia nini sisi wa matombo, ileje,masasi,na kwingineko nchini? Kodi zenyewe hawalipi wanaingiza magari kwa msamaha wa kodi. Huu usingizi wa serikali utaisha lini jamani???
Ziko bank za kitanzania nazifahamu zimekopesha wachina malori yasiyohesabika. Leo hii wewe mtanzania ukitaka moja process itachukua miezi sita na unakata tamaa hata hulipati.... ! Agha! Basi bana siendelei .... 😡
Hizo ngarangara zenu, siti zake ndogo na zimebanana, ziko fixed hauwezi kuadjust, ukifika mwisho wa safari duuu, ni kama ulikuwa unaendesha baiskeli ya Anita. Zile siti ziko kama EXCUTION CHAIR, na madirisha kufungua au kufunga mpaka muwe wanaume wawili! Mi nitapanda basi lenye ubora hata kama anamiliki SHETANI.
hivi wakati ule ninyi mnapopandisha nauli wakati wa xmass huwa mnafikiria wagonjwa, watu wanaosafiri kwenda kuona wagonjwa, misiba na mwingien kakopa nauli? huwa mnakuwa wazalendo kweli, nini huwa mnakuwa watz? hakuna watu wabaya kama TABOA hao wamiliki, kwanza mnawanyonya sana madereva wenu wanapata stress hadi wanadondosha magari, dereva akipata ajali akifa familia zao hamzijali, ninyi mnajali pesa tu. unafikiri ninyi ndio wazalendo? ninyi ndio mashetani wa nchi hii. bora wachina waje.
hahahaha haiseeeNAWAUNGA MKONO WACHINA KUJA KUWEKEZA,WATANZANIA WANAMARINGO NA HAWAJUI CUSTOMER CARE,hutoa Lugha Chafu Kwenye Magari Yao,huduma Mbovu, Wachafu Wananuka Vikwapa,magari Yao Mabovu Na Yanakunguni Ndani.
Hute#
Uzalendo umekutoka kabisa. Hizo ajali zinasababishwa na vichochoro vya nchi hii. Hiyo imani ya kafara unayo wewe! Hujui tu ni kwa kiasi gani unanufaika na uchumi kurudi mikononi mwetu wenyewe.
Nikukumbushe tu kabla ya wachagga kushika hatamu kwenye maduka walikuwepo wahindi tu kwenye biashara zote. Kariakoo kiatu kilikuwa hakishikiki, nguo balaa. Mhindi alikuwa hana lugha mbili.
Na magofu yalijaa miji yote.
Leo hii maduka yanamilikiwa na watanzania kwa kiasi kikubwa.... unaona miji inavyopendeza? Magofu yameisha kariakoo. Hata kule mkoani kwako bobobo kuna ghorofa zimejengwa na wafanyabiashara wazawa.
Tahadhari, wachona nao wamevamia tena biashara ya maduka! Endelea kuwasifia. Utawaona hapo ofisini kwako wanafanya kazi ya cashier.
TRA tayari wameingia... ndiyo systems administrators (Tancis)
Guys tuache ushabiki, back to our senses, tuzungumze hawa mchwa wawekewe ukomo. Watatumalizaaaa
Mleta mada unanishangaza sana! Tena umesema wewe ni mdau wa usafirishaji. Unalalamika mchina kutoza nauli ndogo,ni soko huria mlivyokuwa mnachaji nauli kubwa mbona hukusikia kilio cha abiria?!
Pili unalalamika mchina anauza gari za zamani ili anunue mpya na bado wewe no mnunuzi! Sasa si uache kununua ukanunue mpya?! Hivyo wanavyofanya ndio inatakiwa sio mnakaa na mabasi mpaka yaue watu kwa ubovu.
Na kuhusu kuondoa basi na abiria watano tu hivyo ndivyo inavyotakiwa,kama unaendesha kampuni inavyotakiwa muda ukifika basi linatakiwa kuondoka hata likiwa na abiria mmoja au muombe umlipe apande basi lingine.
Naona hao wachina watawanyoosha sasa na msipoungana na kuwa professionals watawatoa barabarani.
Mtoa mada: na bado sasa waruhusiwe kumiliki banks.
Wewe kwanini ununue kukuuu kwa mchina? mejaa wivu wa kike na hata ukipata kuwa konda wa mchina utaidhi wateja kwa kuwa watz hamjui business...unalalamikia wachina kushusha nauli? Wao wanaweka maji ya diesel? Hebu acha utoto ingia kwenye soko la dunia uongeze uelewa. Kwanini msiungane watu 5 mnanunua jipya