Wachina kuvamia usafirishaji ni Halali?

Wachina kuvamia usafirishaji ni Halali?

wewe mwenyewe sio mzalendo, mngekuwa wazalendo msingewanyanyasa abiria kwa bei mtakavyo. kumbuka mnachofanya siku za mwisho wa mwaka na sikukuuu. sisi wasafiri ndio tunaojua uchungu, wewe mwenye gari unayetaka tuwe wazalendo kwako tumefaidika nini toka kwako? kama usafiri hata mchina atatupatia, usijefikiri kuleta magari yenu mnatusaidia msaada. mbona maduka ya wachina bidhaa zao ni bei nafuu, hata tukijumua sisi wengine kwenye maduka ya jumla tunaona faida. kwenye biashara, wako

Uzalendo tunaouangalia ni serikali kupata kodi yake . Kama kodi inalipwa na Sheria hazivunjwi amna uzalendo zaidi ya huo mengine ni blablaaa
 
Kayaman asante .....
Watu wanasahau huyu mchina yeye ana msamaha wa kodi... kwa hilo tu ..the moment anaweka gari barabarani tayari ana unafuu mkubwa sana.... sisi wavuja jasho tutashindanaje nao?

Shida yetu ni mazingira yaliyojengwa na serikali kuwajali wawekezaji bila mipaka na kutusahau sisi wazawa tuliohangaika na hili taifa tangu uhuru hadi leo.
Tumewavusha wakati wote barabara zikiwa vumbi hadi leo kuna unafuu.

Je hizo youtong zingewapeleka mwanza enzi zile tunapiga shimo mwanzo mwisho siku tatu? Tulivumilia tukawafikisha watanzania wenzetu. Tulindwe basi twende na moderate speed kukua kufikia huko waliko wenzetu.

Mtaji wa ghafla hivyo kwa Tz hii tutapata wapi?

Unaweza kuthibitisha wanamsamaha wa kodi
 
Watanzania tunapenda kulalamika sana,,ivi kunamfanyabiashara anaweza kufanya biashara isiyolipa? Unaposema mchina kashusha nauli kwamaana hiyo hapati faida ila nyie mnaopandisha nauli ndo mnaopata faidi? Mimi kama mteja nikiingia pale ubongo huwa sifuti basi la kampuni ya mchina bali natafuta basi zuri na kwa bei nzuri,,kwann huwa mnapandisha bei ya nauli wakati wa sikukuu za mwisho wa mwaka? Mtu unapanda basi ukifika chalinze limebuma abiria mnaambiwa subirin tunaleta basi jingine,hapo mtasubiri siku nzima kama siyo kulala kabisa,unapanda basi umekaa nyuma mkikaribia mizani unaambiwa sogea katikati,,mnafanya biashara kihuni alafu unaogopa ushindani...Huwezi kuepuka kufanya biashara na mchina kwenye dunia ya leo,,mchina yupo kila kona ya dunia hii,mmarekani mwenyewe kazima fegi hakuna namna wana capital,technology na man power ni kukomaa nao tu...nichukue nafasi hii kuwapongeza wafanyabiashara wa mabus wazalendo wa kampuni ya Kilinanjaro Bus,Mtei,Dar Express,Shabiby ambao kwakweli hawana tamaa za kupandisha nauli wakati wa sikukuu na wamejitahidi kufanya biashara ya kiungwana na ya kisasa..!
 
Uzalendo tunaouangalia ni serikali kupata kodi yake . Kama kodi inalipwa na Sheria hazivunjwi amna uzalendo zaidi ya huo mengine ni blablaaa

Acha porojo...kisa umelipa kodi ndo umkandamize abiria? Kodi unayolipa imewekwa kulingana na gharama za uendeshaji na nauli zilizopangwa,unapopandisha nauli kihuni maana yake mnawanyonya abiria..huu ni uzalendo?
 
Acha kulalamika wewe hebu boresheni hizo huduma zenu mshindane na hao Wachina katika soko hilo la usafirishaji...

Miaka yote kumekuwa na huduma mbovu za usafirishaji abiria ukiacha enzi za uwepo wa Scandinavia...
 
Ndg zangu naombeni kuhoji kupitia jamvi hili ili na nyie mnisaidie

Mimi ni mdau wa biashara ya usafirishaji kwa njia ya barabara.

Tumevamiwa na tena tunakandamizwa hatupumui hata kidogo na hawa wawekezaji wapya WACHINA.

Nikizungumzia mabasi, leo hii kuna wachina wanapeleka mabasi route zote kutoka Dar. Na wako radhi kupakia abiria kwa bei wanayopenda wao, na kuondoa gari na abiria hata watano.

Ikumbukwe hao wachina ndio mawakala wa mabasi ya Yutong na Zhongton ambayo yako kwenye chart sasa.

Je isingekuwa vyema kwa hawa wachina kuwa restricted kwenye kutuuzia tu mabasi na sisi tufanye biashara ya usafiri?

Kumbuka mchina mmoja ana mabasi zaidi ya 150.
Wale watanzania tunaojenga uwezo na vibasi vyetu viwili, vinne hadi kumi je tuta-survive?

Kwa uelewa wa kawaida pale ubungo kwa siku yanatoka mabasi yasiyopungua 200. Katika hayo wamiliki ni zaidi ya 100. Maana yake ni kwamba uchumi umesambaa mikononi mwetu wenyewe. Je tukimwacha mchina atoe mabasi 50 peke yake akaja ma mchina mwingine tena, wamiliki watanzania tutapona? Mbaya zaidi ni kuwa mchina anaweza kuweka basi mpya kila mwezi, sisi tunaweza?

Kwa wale msiofahamu, wachina wanauza mabasi ambayo wameshatumia yenye namba B na C yote kwa bei punguzo. Na mimi nimenunua hapo kadhaa. Lengo lao ni kuhakikisha wanaendesha mapya kila wakati na sisi yetu yanaendeshwa miaka mitano. Ndiyo uwezo wetu kitanzania.

Hawa wenzetu wana access to capital huko kwao. Sisi kama yatima tunapambana tangu mavumbini hadi tulipopata cent ya kununua kamoja. Je ni halali kutufutilia mbali kwa namna hii?

Hii sera yetu ikoje? Serikali iko wapi? Mbona mnatufanya kitu mbaya hivi?

Kwenye Malori hali ndiyo mbaya zaidi. Inaogopesha mno. Kuna kampuni 4 za wachina kila moja ina zaidi ya malori 400. Wanaenda mipaka yote ya nchi kwa bei punguzo.
Halafu hao hao wachina wamenunua kampuni za clearing. Kwa hiyo wanatoa mizigo wenyewe na wanagawana wenyewe. Ukifanya sensa ya watanzania wenye gari moja hadi 20 ni wengi mno tumetapakaa nchi nzima na uchumi unasambaa. Je huyu mchina akichuma hapa anatuachia nini sisi wa matombo, ileje,masasi,na kwingineko nchini? Kodi zenyewe hawalipi wanaingiza magari kwa msamaha wa kodi. Huu usingizi wa serikali utaisha lini jamani???

Ziko bank za kitanzania nazifahamu zimekopesha wachina malori yasiyohesabika. Leo hii wewe mtanzania ukitaka moja process itachukua miezi sita na unakata tamaa hata hulipati.... ! Agha! Basi bana siendelei .... 😡
usilalamike hii ndo maana ya biashara huria.ushindani ni muhimu.ukiwa na huduma nzuri utapata abiria.hawa wachina wana huduma nzuri sana ktk mabasi yao nilishasafiri nao kutoka kahama hadi dar.boreshen huduma na sio kulalamika.
 
Pambafuuuhawa namgome tena kumbemgomowenu sababu yawachina. Mtajibebaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Biashara siomabasii njoomuuze. condom nazo zinalipaaaa wapiidinaaaaa werraaaaweraaaa mzeematolaaaaa kijanaaaa wa panda ya.....
 
Nasikitika kusema amna adabu wala shukrani labda niwajulishe wapendwaa asilimia 80.yamabasi yakichina awamajitu yamepewa kwamkopo sasa unapokuja kutaka numuaibisha anaekupamkopo wote m nonekana. Mazuzu jipangen
 
Na zis taimu tumejipanga mkileta ukonyo wakugoma et tunaweka yu tong mbezipost. Mbagala mtaisomanamba mwakahuuu harooooooooooooooooo mlipotakaaa uria mlihisj biashara za sinza pekeee komaeni mtatoka peleken. Hata. Mabasiyenu dar et mlandizi. Siolazima kwenda anapoenda mchina
 
Na kweli hatushindwi ! Lakini hatujafikia hapo na wala hatuwaxhukii watanzania kwa kiwango hicho!

Ila najiuliza, hivi nyie mnaosupport wachina ni watanzania Kweli?

Ndiyo ni Watanzania, kwani kuna mchina jf, watanzania ni shida sana hasa customer care, abiria akibanwa haja hamjali, hata kama kuna vituo maalumu vya kusimama lazima mzingatie kuwa kuna dharura wakati mwingine, lugha chafu kwa abiria ndo jadi yenu, acha mpate lesson kidogo. Unapokata tiketi unaonyeshwa picha ya basi zuri, kesho yake sasa wakati wa safari ndo utaisoma namba unapandishwa basi kama banda la kuku na huna la kufanya... pia mnaamini sana uchawi, wapuuzi sana nyie.
 
hata wewe mwenyewe ni jeneza linalotembea kwasababu mwili wako umejaa vitu vya kichina vitupu kuanzia nywele, heleni, makalio, nguo, viatu kila kitu hadi vyakula vipo vingine unakula vya kichina. mbona bado unaishi sasa
umebuuuuuugi,pole mimi sinunuagi mchina kilichopo Africa,nanunua mchina aliyepo USA NA ULAYA MAGHARIBI
 
Ba Brio

Bora wachina mara mia, kwasababu mabasi yao ni bora, yana kiyoyozi, bei nafuuu na hawachinji kutoa makafara kama ninyi wabongo na mibasi yenu takataka mliyotengeneza bodi kenya. mmetunyanyasa vya kutosha na kwa miaka mingi sana mkipandisha bei mpendavyo, soko huria linaendelea itafika kipindi mtapaki hayo mangarangara yenu garage.

sisi abiria tunachohitaji sio basi la mtanzania, tunachohitaji ni usafiri bora, hatujali ni wa mtz au mchina au mzungu, na hata wewe ukipata hela yako mimi hainihusu ni yako wewe na watoto wako hivyo niko radhi hata kuungana na mchina ili basi lako life kama kutakuwa na maslahi. kwendeni zenu huko chinjachinja ninyi. mlizoea biashara za mabasi kwa uchawi mchina amekuja kufanya biashara kwa kutumia akili, au naye kawazidi nguvu kwa dini yake ya Confucianism?

wewe jamaa umechanganyikiwa!yaani umeongea kijinga jinga sana.....hivi hujui watu weeengi mtaani wakipata ela inakuwa ni nafuu kwako wewe usiye na ela pia.
 
Last edited by a moderator:
Pambafuuuhawa namgome tena kumbemgomowenu sababu yawachina. Mtajibebaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Biashara siomabasii njoomuuze. condom nazo zinalipaaaa wapiidinaaaaa werraaaaweraaaa mzeematolaaaaa kijanaaaa wa panda ya.....

mh..........!!!
 
Tupo katika dunia ya utandawazi sasa. Lakini naona watanzania wanaomiliki mabasi bado akili zao ni za enzi za ujima. Sasa hivi tunaishi kwenye ulimwengu wa soko huria ambalo msingi wake mkubwa ni ushindani wa ubora wa huduma. Kwa hiyo kama huwezi kushindana utajiondoa mwenyewe na hii dunia sio mahala pako maana utaachwa sana.

Inasikitisha kuona unataka watanzania tuedelee kuunga mkono ujima wa karne ya 10 wakati sasa ni karne ya 21. Unataka tuendelee kusafiria hayo mabasi yako mikweche yenye madereva na makonda wenye lugha chafu za matusi, wanaotupiga na kutulangua nauli. kwanza wewe ni mbinafsi, unajifikiria wewe kupata pesa na sio huduma bora kwa abiria. Kama unataka kufanya biashara badilika uende na wakati. hakuna mtu wa kukuonea huruma kwenye hizo huduma zako mbaya.

Asante Mungu maana saa ya ukombozi imewadia. Sasa ni Muda wa hawa wachawi waliotuangamiza kwa ajali, waliosababisha uyatima, na ulemavu kwa sababu zao za kishirikina na uzembe kuondoka barabarani.

Na ukiona mtu anakuja JF kulialia ujue tayari hali yake ni mbaya. Mbaya ziadi unajieleza kwa watu ambao umekuwa ukiwanyonya na kuwanyanyasa. Sijui unategemea wakupe sapoti gani maskini. Uliyeshindwa biashara ya usafirshaji uwapishe wanaoiweza, wewe kafanye shughuli nyingine.
 
Uuuuuiiii.... mkuu ushindani hauwezekani bila governor kutoka serikalini. Level mbili tofauti sanaaaa.... sisi wa gari 5 na wa gari 150 tushindane kivipi? Wao wana access to capital..sisi je?

Wewe mwenyewe hapo kila siku unatamani upate mkopo ujikwamue lkn huna vigezo. Ndiyo tz yetu. Imebaki kulilia serikali tu.

Stop pretending guys. Dont take it so lightly, tutamalizwa. Hali ni mbaya... twaelekea pabaya...

Niambie mchina mwenye bus 150
 
Lazima na nyinyi mbadilike. Mnaendekeza kupandisha bei kiholela kwa ruti za kawaida, huduma mbovu kabla hata ya Wachina kuja, Mmewasumbua sana Sumatra. Bora walivyokuja hao Wachina ili abirie apate unafuu kutokana na ushindani baina yenu wamiliki wa mabasi.
 
Hakuna mchina mwenye bus 150 ,New Force na gari za kwenda Mbeya , Tunduma, songea na Kahama pekee. Labda malori kuna Sunshine anayo zaidi ya 200. All in all Wachina wameboresha sana usafiri nadhani ni kujitahidi kununua magar mapya na kuwa na huduma bora hakuna mtanzania aliyepo tayar kupanda gar bovu wakati yapo magari bora na mapya.

Mghosi
 
Back
Top Bottom