Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 2,231
- 7,513
Nimeona tunawachekea Wachina mno wanaingia TZ vibaya mno tena wapo wengi, Iko sio jambo la kushangaza mno, jambo la kushangaza je mamlaka zetu zinafahamu hata Chinese people ni wangapi hapa TZ? je wanafahamu kwamba wapo wachina wanafuga Bata na kuku? Je wanafahamu wapo wana maduka mtaani maduka ya kawaida? Je wameshapima athari za hawa jamaa nchini?
Nimeona sasaivi wanachimba dhahabu uko chunya, geita, brothers hiyo nchi yenu ni noma sana watu wanachukua chao mapema.
Nimeona jana Kwa bashasha viongozi wamefungua jengo la biashara la yiwu, yiwu ni mji mkubwa wa biashara Unajulikana duniani kama moja ya masoko makubwa zaidi ya jumla (wholesale markets) je mmeshapiga hesabu ya hasara zake? Watauza bidhaa zao Kwa bei ya hapa tena Kwa rejareja vipi kuhusu wafanyabiashara wa kariakoo? Kumbuka hawa wachina wana mtaji mikubwa, believe me wakipata pesa hawa jamaa sidhani kama inarudi kwenye mzunguko hapa, mission Yao ni kutafuta pesa tu matumizi ni huko kwao, basi pesa itapatikanaje kama wamiliki/watumiaji wamenyang'anywa?
Wameanza kushtuka kupata visa ya kwenda China ni mtifuano mkali na zakuvizia ila wao kuja uku visa ni kama oxygen, kumbuka sisi wabongo kwanza tuna roho mbaya hatupendani ukisema ulete huo mzigo ukiritimba ni wakutosha, ila sidhani kama inatokea kwao,
Kizazi iki na kinachokuja wajikite wapi kwenye uzalishaji au mashambani?
Anyways nobody care, taifa ni kubwa fursa ni tele pambaneni.