senkoP
Senior Member
- Aug 28, 2017
- 180
- 207
Ni kwanini watu wachawi huwa wanajifanya wana upendo sana? Utakuta kama ni kanisani/ Msikitini wao ndio mstari wa mbele kuhudhuria ibada zote, kutoa michango mbalimbali , kukarimu wageni hapa kwenye kukarimu wageni huwa mstari wa mbele hata kama kumeshapangwa Shekhe au Mchungaji atakula wapi utakuta yeye anasema jambo hilo niachieni mimi nitalimaliza na kweli ana maliza, kukitokea msiba huwa wanaahirisha mambo yao na kuwa karibu na mfiwa na hata kujipenyeza kwenda kuosha maiti.....yaani sielewi ni kwanini?