Lupatu: Kinga dhidi ya wachawi na uchawi

Kitoabu

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
10,333
10,950
Boa tarde camaradas.

Tembea uyaone, zunguka ujifunze.

Hivyo ndivyo ninavyoanza kwa leo.

Mara nyingi nimekua msomaji tu humu ndani, ila leo kuna topic nimeisoma humu ndani iliyo nishawishi na mimi leo niandike.

Katika harakati zangu za kutafuta maisha nilijikuta naangukia Mocambique. Mocambique sikwenda kuajiriwa bali ni kuchimba madini (Ruby).

Nakumbuka huku nilikutana na Rafiki yangu anaeitwa Carlos. Mshikaji tulijuana kutokana na kufanya nae kazi (kuchimba) mara kwa mara.

Katika harakati zetu mara nyingi tulikuwa watu wa kuporora (hatupati madini)

Siku moja Carlos akanishauri twende kijijini kwao Shapa (wilaya ya Mueda, mkoa Cabo del Gado) kuna mzee ni mganga anaweza kutusaidia katika haraka zetu. Carlos yeye ni Mmakonde chale.

Baada ya kufika kijijini Shapa, Carlos akinichukua mpaka nyumbani kwa mganga (Mzee LUPATU)

Tulifika kwa mzee, tukamueleza shida yetu, na mzee akakubali kutupa dawa (ya madini). Siku ya tatu tukageuka kurudi mgodini (Nanhupo, wilaya ya Montepuez, mkoa Cabo del Gado)

Hatukumaliza wiki mbili, tukapata Gram moja na point saba (Ruby) tukaenda kulitikisa (kuuza) kwa Mtailendi.

Tukapata mgao kila mtu $17,500. US dollar. Kwa muda huo nilijikuta na Milioni thalathini sita na usheee hivi.

Baada ya mgao wetu, tukaamua kwenda kumpa shukrani yake mzee wetu (Mzee LUPATU) tena ukizingatia kutoka Mueda kwenda Namatili (boda) sio mbali, na ndio njia ambayo ninaitumia kuvuka kutoka Mocambique kuja Tanzania.

Tulifika kwa mzee LUPATU tukampa shukrani, na kila mtu akampa yule mzee 50,000 miticaish.

Baada ya shukrani, yule mzee akatuomba tulale pale kwake kisha kesho tuondoke, maana kuna kinga anataka kutupa.

Hakuna aliekataa, tulibaki pale kama alivyotaka babu yetu.

Kilipoingia kiza babu alikuja na ndoo iliyo jaa maji yenye dawa (niliona mizizi na majani ndani ya yale maji) akatuogesha kisha tukaingia kilingeni kwake. Akatoa vibao vidogo viwili, vye pembe nne, mfano wa kibiriti.

Vibao vile upande mmoja wa kibao kulikua kama kimechorwa msalaba kwa kuchongwa. Tukaamuliwa tuchanjwe damu, then damu ile ilipitishwa mule kwenye mistari iliyo chongwa kama msalaba.

Tulipomaliza zoezi lile, kila mtu akapewa kibao chake na kuruhusiwa kwenda kulala.

Kabla ya kwenda kulala mzee alitupa masharti ya dawa ile, akatuambia hii ndio LUPATU Wajukuu zangu, hamtarogwa na mtu yoyote kwenye dunia hii. Akatuambia lakini dawa hii ina masharti.

1 Usiende nayo kwenye shughuli yoyote ile, iwe harusi ama maziko.

2 Ukifika popote (ugenini) unatakiwa uwaambie wenyeji kuwa una kinga dhidi ya uchawi, hivyo hairuhusiwi kwa mtu yeyote kugusa uchawi mpaka utakapo ondoka.

3 Ukitaka kulala na mwanamke, iache nje (nje ya mlango)

Chengine, alituambia kuwa, hiyo dawa inafanya kazi umbali wa nyumba kumi kutoka kushoto, nyumba kumi kulia, nyumba kumi mbele ya nyumba, nyumba kumi nyuma ya nyumba.


Siku iliyo fuata mimi na Carlos tukaondoka, kila mtu akielekea kwao.

Carlos nilimuacha kwao Mueda, mimi nikavuka boda nikaingia nyumbani Tanzania. Nilipofika home, nikawaambia ndugu zangu hasa watu wazima. Pale home, mzee kuliko wote ni mama yangu mkubwa.

Hii ni nyumba ya familia (akina mama wamerithi nyumba ya baba yao) Kuna watu wengi sana.

Basi baada ya mapokezi, uchovu wa safari ilinibidi nipumzike kidogo (nililala)

Nilivyoamka jua lilikua limeshazama, hivyo jioni ilisha ingia.
Nikatumia muda huo kuwaambia wale waliokuwepo siku hiyo.
Nakumbuka alikua Mama mkubwa, dada yangu wa kwanza kuzaliwa, Mjomba pamoja na madogo walio kuwepo hapo.

Nilinza kwa kuwaambia kuwa nina dawa ya uchawi, hivyo kama kuna mchawi basi asichezee uchawi wake mpaka mimi nitakapoondoka.

Niliongea kimasihara kwakua nilitegemea nyumbani hakuna mchawi.

Mama yangu mkubwa akaomba nimuoneshe hiyo kinga (dawa).
Nikaingia mfukoni nikakitoa kile kibao. Kila mtu alicheka na kusema Mocambique wanaamini sana uchawi.

Usiku uliingia na kila mmoja akaenda zake kulala.

Siku ya pili palipokucha nikaelekea zangu Karikoo, kwenda kuchenji Dollar zangu. (Kariakoo Bazar )

Siku hiyo nakumbuka nilikula sana mtungi, nikarudi home usiku sana kama mida ya saa sita hivi usiku.
Nilipo fika home, kwa uchovu wa pombe nikajilaza kitandani, mara hazikupita dakika nyingi nikaanza kuona chumba kina mwekua mwekua, yani kama mtu kashika kioo anakizungusha mule ndani.

Nikaamka, mara ya kwanza nilidhani ni pombe labda, lakini jinsi muda ulivyokua unaenda ile hali ndio ilikua inazidi.

Ilipita kama dakika 20 hivi huku ile hali ya kumulika ikiendelea, mara nikasikia Pah! Yani kama mtu kapasua chupa ya bia vile.

Baada ya ule mlio, ule mwanga wa kioo mule ndani ukapotea.
Usingizi ulinichuka mpaka asubuhi.

Cha ajabu naamka asubuhi nakuta watu pale home wamejawa na huzuni, nilivyouliza naambiwa mama yako mkubwa kaanguka jana usiku mlangoni kwake akitokea chooni, hivyo kawaishwa hospital Temeke.

Samahani ndugu zangu.
Hii story nilipanga kuimaliza leo leo, ila kuna hudhuru imenikuta, hivyo nitaimalizia baadae ama kesho.
Naomba munisamehe.

Kwakua chenji nilikua

Kwakua chenji nilikua nayo nikaagiza tax ije ituchuku mpaka hospitalini, kutoka Tandika mpaka Temeke hospital jamaa akataka 8000, nikampa, na wanandugu tukaingia mle.

Tulipo fika hospital, kila mtu ali msalimu mama mkubwa, ilipo fika zamu yangu mamkubwa hakuitikia.

Sikujisikia raha, hata tulipo rudi nyumbani nikabaki na maswali kwa nini mama mkubwa hakunichangamkia pale hospital.

Siku ya pili yake mida kama ya saa mbili usiku nikaona watu wanarudi na mashuka kutoka hospital.
Mara zikaja taarifa kua mama mkubwa kafa.
Kwakua yule mganga sharti moja wapo ya ile kinga alisema haitakiwi kwenda nayo kwenye shughuli yoyote ile, iwe harusi ama maziko, hivyo ilinibidi niitowe ile dawa na kuipeleka kwa rafiki yangu Yombo dovya.

Nikaichukua ile kinga nikaitia ndani ya begi la nguo zangu nikaipeka kwa rafiki anaishi yombo, kisha nikarudi nyumbani mazikoni.

Kweli tulizika salama
Mara baada ya kuisha maziko na wageni kuondoka, mama yangu mzazi (yeye haishi nyumbani hapo) akaniita chemba nakuniuliza (hiyo ni siku mbili baada ya mazishi)"Mwanangu umerudi na nini kutoka huko Mocambique"?
"Mwanangu wewe ni mtoto hicho ulicho rudi nacho ni kikubwa utawamaliza watu"

Nilishindwa nimjibu nini bimkubwa. Nikafikiliaaa, nikamjibu "mama mimi nimerudi na Dollar kutoka Mocambique.
Na kwamkukata ngebe nikaingia chumbani nikatoka na Dollar 500, nikamkabidhi.
Nikamwambia "mama hiyo ni zaidi ya Milioni moja.
Baada ya maongezi yale bimkubwa akaondoka zake kwake, na siku kama ya tano kila mtu alisha izoea ile hali ya kuishi bila mama mkubwa.


Siku ya sita, nikatoka zangu mpaka yombo, (kwa rafiki yangu) niliko peleka begi langu, nipo fika nikamkuta rafiki yangu akanipa begi langu, nilipo muuliza kuhusu mama , (mama yake) akaniambia yuko msibani, nyumba ya jirani kuna msiba.

Sikutaka kufatilia sana, nikachuka begi langu nakurudi home. (tandika)


Kwakua maswala ya msiba, sikupata hata muda wa kutumia pesa zangu.

Nyumbani pale baada ya msiba kwisha na wageni kuondoka, tukabaki wenyewe kama zamani, kasoro mjomba flani kutoka zake kijijini (wana udugu nae tu akina mama) yeye hakuondoka.

Zikapita kama siku Kazaa hivi, siku hiyo nimelala, ghafla nikaamka, baada ya kuamka nikakuta chumba kizima kina mwekua mwekua kama mtu kashika kioo anakizungusha mule ndani.
Nika nyanyuka mpaka ditishani nikachungulia, sikuona chochote, nikarudi kitandani.
Hazikupita dakika nyingi mara nikasikia Pah (mlio ule ule wa chupa inayo pasuliwa)
Mara ule umweku mweku ukapotea na usingizi ukanipitia.

Hata lisaa naamini halikupita, mara nasikia naamshwa, nilipotoka nje nikakuta wanandugu wako nje sura zimejaa huzuni.
Nikamfuata dada yangu nikamuuliza kulikoni? Mbona sura za huruma?
Sister akanijibu kua mjomba kadanja, (kafa).

Harakati za kuipeleka maiti hospitalini usiku ule ule, mpaka kuna pamba zuka, sielewi.


Kilipo kucha kila ndugu zikawa zimemfikia habari zile za kifo.
Mazishi yakapangwa yafanyike kijijini,
Bungu.

Tukaenda wanandugu wote mpaka Bungu, tukazika, tulipo maliza kuzika, sikulemba nikachukua gari nikarudi home.
Siku ya tatu, mama yangu mzazi akaja home, akitokea msibani, alipo fika tu akataka tuongee chemba.

Kama kawaida yake mama, akaanza kuniuliza maswala yale yale.

"Mwanangu umerudi na nini kutoka huko Mocambique"?
"Ulicho rudi nacho hicho ni kikubwa utawamaliza watu wewe ni mtoto"



Tiripu hii uoga ukaniingia, nikazama ndani, nikaingia mpaka kwenye begi nikakitoa kile kibao, na kwenda nacho mpaka alipo kua mama na kumuonyesha.

DAHH , EBWANA EE KILA NIKI TAKA KUMALIZIA MAMBO YANAINGILIANA.
NISAMEHENI KUNA JITU NA MALIZANA NALO KWANZA. NITARUDI.

Mama alikitazama kile kibao muda kama dakika 5 hivi, mpaka nikajistukia na kumuuliza mama, mbona anakiangalia sana?
"Mwanangu hichi kitu ni kikubwa wewe bado ni mtoto, kitupe kitakuletea madhara"

"Hiki ndicho kilicho waua dada yangu na kaka yangu"
Mama aliendelea kuongea huku machozi yakimtoka, mpaka mimi mwenyewe nikashikwa na wenge.
Aliendelea kuniambia, mpaka Kule kijijini watu wamesha jua kua ni mimi ndie nilie sababisha vifo vya Mama mkubwa na mjomba.

Hata watoto wa mjomba wamechukizwa na kitu hicho.
Basi mama akiniomba nikitupe kile kibao.


Mama hakukaa akaondoka kwake, huku nyuma akiniacha na mawazo kibao kichwani.


Kwa kweli nilikaa kama wiki mbili tu lakini nikawa tayari nisha sababisha vifo zaidi ya saba.
Maana ukiachilia kifo cha mama mkubwa pamoja na mjomba, pia hapa mtaani kuna vifo vitatu vya majirani, na vyote vina fanana.

Maana wote kabla ya kufa hutokwa na damu sehumu zote za siri, na wote wamenitaja kwamba chanzo cha kifo Chao ni mimi.

Siku moja nilitulia sehem peke yangu nikajiuliza maswali, nikaona ngoja niende kwa rafiki yangu Yombo dovya (huyu jamaa tume maliza wote yombo dovya primary school)

Nilivyo fika kwake, sikumficha, nimamweleza mkasa mzima, chakushangaza na yeye akaniambia hata hapo kwao kuna vifo vya wazee wawili viliongozana kipindi nilipo peleka begi langu kwao.


Nikarudi home, nakukata shauri kwamba lazima hiki kibao (kinga) nikitupe.

Siku moja, mtaani hapo kulikua na kigodoro, nikala mtungii nikasema leo lazima nikitupe hiki kibao.
Mala baada ya kukubali mtungi nikaongoza mpaka lelini, nikakitoa kile kibao nakukirusha kwa mbali.

Nikarudi zangu home na kujilaza kitandani na usingizi ukanipitia.

Asubuhi nilipo amka, nishaoga maji yangu nikatoa suruali nyingine nikavaa, nikaitoa ile suruali niliyo ivaa jana nakuanza kutoa vitu muhimu.

Nikazama mfuko wa kwanza nikatoa simu, mfuko mwengine nikatoa waleti, sasa nikawa nacheki mifuko ya nyuma ili nicheki kama kuna chenji chenji, katika angaika angaika zangu nakitoa tena kile kibao (ile kinga niliyo itupa jana yake kwenye kigodoro) kwanza nilipagawa nusu ya kudata.


Nakumbuka hiyo siku, nilipanga na mtu (dalali) niende nikaangalie kiwanja Mbande, lakini kutokana na tukio hilo ilinibidi nimpigie jamaa simu nakumuomba aniwie radhi kwa siku hiyo, kwani nilishindwa hata kutoka nje kwa siku hiyo.


MUENDELEE KUNI SAMEHE, MAMBO NI MENGI MUDA NI MDOGO. HATA KESHO NAWEZA NIKAMALIZIA. NITARUDI.

Siku nzima nilibaki ndani nikiki tafakari kile kibao (kinga). Kuna wazo likanijia, nikaona sehem pekee pakwenda kupatupa ni baharini.
Kwakaribu nikaona ni Kurasini.
Ilipo fika jioni nikatoka nje, mpaka Chihota, nikachuka boda boda mpaka kurasini beech, kwakua sikutaka jamaa (boda boda) anigande nikamuomba aniache relini nikampa chake akarudi.


Nikaenda mpaka beech, maeneo flani hivi kitambo walikua wanauza ganja, nikawaacha kama hatua flani hivi wale jamaa (wala bange) hapo nikavua viatu vyangu nakuingia kwenye maji.

Maji ya mafutini, nikageuka nyuma kucheki kama kuna mtu ananitazama, nikagundua kila mtu anahabari zake.

Nikaingia mfukoni nikakitoa kile kibao (kinga) na kukirusha kwenye maji.


Sikutaka kuchelewa, nikapanda juu (relini) nikachukua tonda nakurudi mtaani.

Siku hiyo sikutaka hata pombe nikawai kuingia chumbani mapemaa nakujilaza.

Katika safari zangu zote ninazo kujaga Tanzania, safari hii sikuifurahia kabisa.

Japo nilikuja na pesa lakini nilijikuta niko bize hata muda wakutulia na washkaji sikua nao.
Nilisha zoea nikija na Mkwanja, humchukuaga rafiki yangu Dsalu nakumuomba anitembeze jijini, lakini safari hii hata yeye mwenyewe alikua akinishangaa.

Nakumbuka hata lile dili la kununua kiwanja Mbande lilikufa, dakika ya mwisho familia iliamua kuni nunulia chamanzi na kujenga kipindi mimi mwenyewe nisha kimbia.

Usiku wa siku hiyo kwangu ulikua mkubwa sana, sababu nililala mapema na kichwa kulikua hakija beba alcohol, ivyo nili lala kidogo, linipoamka sikupata usingizi kwa haraka.

Mida kama ya saa tisa usiku, mara nikaanza kuona ule umweku mweku mule ndani, chumba kizima kina mwekua mwekua, nikanyanyuka kitandani, nikaisogelea switch ya taa na kubonyeza.
Taa ikawaka lakini ule umweku mweku bado upo tu, nikaona ngoja nilipue chiga kwanza, nikatoa sigara mfuko wa shati, kibiriti huwa napenda kukiweka mezani, nilipo ikalibia meza, niki cheki mezani nakiona kile kibao pale mezani, sigara yenyewe nikairusha niliko itoa.

Nilitulia pale nikiki angalia kile kibao, mara nikasikia ule mlio Pah (kama chupa ya bia iliyo pasuliwa)
Zilipita kama dakika kazaa ule umweku mweku ukapotea na usingizi ukanipitia.


Asubuhi nilipo amka nyumba ya jirani nasikia kilio watu wanalia, nikajua tayari kuna mtu kesha jipiga.

Jirani alikua maarufu kiasi msiba wake watu walijaa sana.
Mpaka mama yangu nae akaja, mimi mwenyewe nilihudhuria mazishi.

Pale msibani niligundua watu wengi walikua wananiangalia sana, hasa wazee.
Hata tulipo kua makabulini, niliwaona wazee flani kama wananioneshea kidole.


Maziko yaliisha nikarudi nyumbani.
Mama na yeye nilimkuta yuko nyumbani teyari kesha rudi msibani.

Siku hiyo mama ali lala hapo hapo nyumbani, ilipo fika usiku, mama aliniita tena chemba.
Tilipu hii mama aliniomba niondoke, nirudi nilipo toka, (mocambique) ama nitokomee popote tu.

Mama aliniambia niondoke nisije kuuawa, maana story zangu zina vuma mtaa mzima.
Watu (wazee wa mtaa) wamejua kua nina kitu kinacho wadhuru wachawi.

Sikutaka nimfiche mama, nili muhadithia story nzima jinsi nilivyo jaribu kukitupa kile kibao (Mala mbili) lakini bila mafanikio.

Basi mama akaniambia, nakupenda mwanangu sitaki uu wawe, ondoka, nenda popote tu.

Siku kama mbili nilizimaliza nikiwa chumbani peke yangu, nikitoka nae kibaa cha jirani, nachukua Konyagi zangu na kujimiminia.
Kwa kweli maisha siku ya furahia kabisa.

Nikaona sio poa wacha nisepe zangu, maana sasa mpaka dada na yeye alikua haishi kunihimiza niondoke.
Kabla ya kuondoka, nikaona ngoja nikamtembelee babu yangu (mzaa baba) yeye huwa nampenda sana.

Yeye ndio alie ni rithisha Jina, huwa siwezi kuja Tanzania bila kumtembelea.

Babu yangu yeye anaishi Hanga, njia ya kwenda nyamisati.

Nilifika kwa babu, na kweli nilimkuta.

BADO KIDOGO NIMALIZIE, JAMBO LINAINGILIANA.
TUSAMEHANE JAMANI NITARUDI KUIMALIZIA.

Nilifika kwa babu na kweli nilimkuta.
Wenyewe tunapenda kuitana somo.

Kwakua nikisafiligi huchukua hata miaka mitatu bila kuja Tanzania, hivyo somo wangu alikua na ham kinoma na mimi.

Tulisalimiana, akaniuliza kuhusiana na harakati zangu, nakuniuliza nimerudi lini kutoka Mocambique.
Nikamjibu nina kama week mbili hivi, ila hii safari anayo iona ni ya kurudi Mocambique.

Babu alishangaa, sababu sio kawaida yangu, maana nikija Tanzania hukaa hata miezi mitatu, tena zaidi nikirudigi na mgao mkubwa.

Baada ya story mbili tatu, kama kawaida nikamwambia babu kama masharti ya dawa inavyo takiwa.

Kwamba mi nina dawa ya uchawi, haitakiwi mtu kuchezea uchawi mpaka mimi nitakapo ondoka.

Babu yangu siku hiyo alichukia, na kuniambia kua mjukuu wangu hiyo ni shirk, wewe bado mdogo hayo mambo yatakudhuru.

Sikutaka hata kumuonyesha wala kumsimulia kilicho nikimbiza Dar, nikatulia kimya.

Usiku ukaingia nikaenda zangu kulala.
Kama kawaida yake, ilipo fika usiku mnene chumbani kukaanza kumwekua mwekua, yani nilijifunika shuka gubi gubi lakini ule umweku mweku niliendelea kuuona.

Hazikupita dakika nyingi, kama kawaida yake nikasikia Pah (ule ule mlio wa chupa iliyo pasuliwa) nikajua leo nime muua babu yangu kipenzi.

Siku lala nikawa nasikilizia kuitwa tu nipewe habar za kifo.
Nilisubilia kimya, siku sikia chochote, usingizi ukanipitia.

Asubuhi nilipo amka nikaenda mlangoni mwa chumba anacho lala bubu nikaita, mala bibi alitoka uwani akaniambia kuwa babu yako anaswali, nikashusha pumzi.

Nilikaa chumbani, sikutaka kuamini mpaka nimuone babu.
Dakika kama tano babu alimaza kuswali na kuniita.
Sijataka kulemba kabisa nikazama mfuko wa begi nikampa pesa babu yangu nakumuaga.

Kutoka Hanga mpaka Bungu, nilitumia kama dakika 20 tu kwa boda boda.
Nilivyo fika Bungu hata dakika hazikupita mara gali la IBRA hilo, nikadandia mpaka Newala.

Niko mnazi mmoja nikampigia simu babu, simu iliita bila majibu, nilirudia kama mala tatu hivi, bila mafanikio.

Newala nikaingia mida kama ya saa tisa ama saa kumi hivi jioni.
Nikicheki simu nakuta miss call ya babu.
Nika mpigia safari hii akapokea, kabla ya kuongea chochote nikamuuliza, Ulikua mazikoni? Babu akajibu ndio.

Tukaongea mambo mengine nikawa na muhadithia kuhusu shimo la Mungu lililopo hapa newala.
Mwisho wa maongezi akaniuliza nimejuaje kama alikua mazikoni?

Sikumpa jibu la maana zaidi ya kumzingua tu (huyu babu yangu ni zaidi ya rafiki yangu, ata jando, kanitairi yeye mwenyewe)

Nilikaa stendi kungojea boda boda, mala boda boda hiyo nikapanda.

Boda boda ile ilikua mizinguo kila tunapo kwenda inazima, nilifika boda saa moja usiku.

Kwa mida hiyo Magresheni upande wa Tanzania alikua kesha funga ofisi na kurudi Newala mjini, hivyo ilinibidi nilale pale.

Kile kijiji huwa nakisahau jina, ila kwa wenyeji wa Newala, ni kijijini chamwisho Tanzania kama unavuka njia ya Namatili.

Yeni ukiushuka mlima wa Nkunya, kuna kijiji hapa nimekisahau jina.

Basi pale kijijini nikapata u wenyeji, (tulio zoea safari hatulali nje) Kuna mshikaji ana kiosk chake, basi tukaanza kufamiana.

Na vijiji vingi vya mipakani hawamshangai mgeni, jamaa tukazoena ghafla, ukizingatia nina pesa ndio usiseme.

Jamaa alifanya biashara zake alipo funga akanichukua mpaka kwake, kwakua ilikua usiku basi alinitambulisha kwa mkewe tu, maana watu walikua wamesha lala.

Shemeji akaleta ugali, tukaugonga me na jamaa.
Tulipo maliza kula, kama kawaida yangu, nikampa maelezo yale ya ile kinga (Kinga)

Nikamwambia kua nina dawa ya uchawi, kwahiyo hatakiwi mtu kuchezea uchawi mpaka mimi nitakapo ondoka.
Mwenyeji wangu akuchukulia maanani.

Akanichukua mpaka chumba flani akanionyesha sehem ya kulala.

Siku mnene, chumba kukaanza kumwekua mwekua kama kawaida yake, kwakua nilisha zoea nikatulia kimya, huku nikijisemea kua lazima kesho niokote Kigomba.

Kama kawaida, nika sikia ule mlio Pah, nikajua tayari kesha nasa.

Nilivyo usikia ule mlio na dakika kupita na ule umweku mweku ukapotea, nausingi ukanipitia.


Hakukucha mara nasikia sauti ya shemeji akiongea na mumewe (mwenyeji wangu) waende wakamuite mzee gani sijui hapo jirani.
Mara nasikia sauti kibao hapo nje, kumbe hii nyumba wanaishi watu wengi.

Mwenyeji wangu yeye na kijana mmoja, inaonyesha ni mdogo wake ama shemeji yake, wakatoka kwenda kumuita huyo mzee, hazikupita dakika nyingi wakawa wamerejea na yule mzee.

NDUGU ZANGU KUANDIKA HABARI NDEFU NAKWAO KUNA CHOSHA. NIACHENI KWANZA NITARUDI.

ILA NAKARIBIA KUIMALIZA.

Walipo rudi na yule mzee, hata mimi nilikua tayari nisha toka nje, tayari kusaidia kazi za hapa na pale.
Nakumbuka mimi na jamaa flani tuliingia alipo lala maiti nakuanza kutoa vitu vilivyo mle ndani.

Yule mzee alipo fika akaingia mpaka chumba alicho lala maiti, (nahisi kuna mila zilifanyika humo.
Kama dakika 30 yule mzee akatoka mle ndani.

Shauku yangu kubwa ilikua ni kujua kua mwenyeji wangu yuko nae vipi yule malehemu?

Nilitamani kumuuliza lakini nilishindwa kutokana na hali aliyo kua nayo.

Mala, kukaanza kupambazuka, nikashukuru.

Nikajifanya kama nakwenda dukani kununua sigara, lakini akili yangu ili niambia niwahi kugonga paspoti yangu nitembee.
Nilivyo fika pale magresheni, kalibu kuna kiduka, nikanunua sigara nikalipua.

Kipindi naendelea kuvuta sigara, mala kaja mteja pale dukani, nakuanza kumpa habari za msiba yule muuza duka.

Nasikia, "malehemu kafa kwa kujipiga uchawi" nikaona ohooo, ngoja niingie kwa afsa uhamiaji nikagonge mie.

Nilipo gongewa tu paspoti yangu nikachukua tonda safari ya kwenda mtoni (Ruvuma)
Kuna kitu kilikua kinaniuma sana moyoni mwanangu.
Kitendo cha kuondoka bila kuaga, ukizingatia jamaa alini karimu kama ndugu yake, njia nzima nilitembea nikiraani.

Nilivuka Ruvuma, nikaenda mpaka magresheni ya Mocambique nikagonga paspoti yangu na kuingia ndani ya gari tayari kuitafuta Mueda.

Kama mida ya saa 6 mchana nikawa nishaingia Mueda.
Siku chelewa nikachuka gari iendayo Montepuez nikashuka Shapa.

Nilivyo shuka Shapa, (nyumba ya mzee LUPATU ipo barabani kabisa) nikaingia mpaka ndani na kumkuta mzee.

Mzee alipo niona alifurahi sana, akaniuliza maswala ya Tanzania, na kunitania hapa na pale (Wandengereko & wamakonde ni watani )

Nilijiuza naanzaje kumwambia kua nimekuja kuirudisha ile kinga?

Lakini nikikumbuka yale matukio, niki kumbuka mama yangu alivyo nihusia niirushe nilipo itoa, nika jipa moyo kumkabili huyu mzee.

Nikamwambia " babu nimeirudisha dawa yako, nitawamaliza Wandengereko"
Kwakua ni mtani alicheka na kuniambia, "unge wamaliza kweli, nyinyi Wandengereko ni wachawi sana".

Nilitulia pale mpaka jioni.
Kiza kilipo anza akaniita uwani na ndoo ya maji (Dawa) akaniogesha kama mwanzo.

Akanichukua tena mpaka kilingeni, nakuniamuru nikirudushe kile kibao kwenye ungo.

Kwenye ungo nilivikuta vile vibao vingii, na mimi nikakiacha humo kwenye ungo.

Kwakua ni usiku nili lala mpaka hasbuh.
Palipo kucha nikamuaga mzee kuwa naondoka.

Kwa mas hara yule mzee akaniomba anipe dawa nyingine.
Hii sio kinga, bali ni ndago ya utajiri (chuma ulete)

Yani aliniambia anipe nyoka atakae kuwa na uwezo wa kuingia madukani na kichota pesa na kuniletea.
Tena mpaka dawa yenyewe alinionyesha, yani ni kama kamba, lakini aliniambia kuna maelekezo akinipa basi hiyo kamba inaweza kugeuka nyoka na kuingia duka lolote na kuniletea pesa.

Siku taka hata kumchelewesha, nilimkatalia, na kumwambia mimi bado ni mdogo, sintaweza kuvitumia vitu hivyo.

Mida ya saa 2 asubuhi, gari ikapita nikaingia nakurudi zangu mgodini.

MWISHO.
 
Kwa kuwa umepata udhuru bora tu ungeghairi moja kwa moja ili ukipata nafasi utuletee nzima maana sis ni watu wazima hatutaki hadithi nusu nusu!
Mkuu hii sio story ya kutunga kama Eric Shigongo.

Baada ya kusoma post ya mshikaji, nikaamasika kuandika kisa kilicho nikuta maishani mwangu (kutokana na mashwala ya nguvu za kiza) mara kipindi naandika katokea mshikaji kaanza kuni bughudhi (kaja na dali za kitaa) nika shindwa kumalizia.
 
Back
Top Bottom